Hakuna kitu kizuri kama kuwa mwana kwa baba anayejielewa! Na hakuna kitu kizuri kuwa baba kwa mwana anayekusikiliza.
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
- Ni jukumu lako kuutumia huo uwezo, ili ufanyike mwana wa Mungu ( mtoto wa Mungu upendwaye )! Japo Mungu anataka wewe uwe mwana wake……..ndomana ameachilia huo uwezo.
Katika familia nyingi za kiafrika kunaaminika kuwa sherehe kuu mbili yaani kuzaliwa na kufa.
Japo sherehe kubwa ambayo mtu utegemea kuifanya kwa shangwe kubwa pasipo machozi ya ndani au ya nje ni sherehe ya kuzaliwa.
Kuzaliwa ni jambo lisilo na mpangilio katika akili ya mwanadamu, kwani ni swala lisilo na uchaguzi binafsi wapi uzaliwe na mzazi yupo? imetokea tu umekuta mama au baba kwahiyo wote mnaonana kwa mara ya kwanza inawezekana walikuwa wana utarajia ujio wako lakini wasijue kwa uhakika hasa ni mgeni yupi anayekuja.
Kwa mzazi/mlezi unaweza kuwa au kutambulikana kama mtoto tu au mwana ( kipenzi cha wazazi )!
Kama mzazi japo wote amewazaa lakini kuna mtu atafanya kwa sababu ni mtoto wake tu na kwakuwa yeye ndio muhusika mkuu hivyo anawajibu inabidi awajibike lakini kuna mtoto ( mwana ) huyu anaweza kuitwa jicho la mzazi au moyo wa mzazi mwenyewe hivyo atawajibika tofauti na watoto wengine hata namna alivyochukua nafasi katika mawazo yake au akili na moyo wake ni tofauti na watu wengine.
Moyo wake umejiungamanisha na huyo mtoto ( mwana ) kwa asilimia kubwa.
Japo wote ni watoto wake na wote anawapenda.
Hali hiyo ya mzazi kumpa nafasi kubwa katika moyo wake inawezekana imetokea tu katika hali ya moyo wake au ni kwasababu ni jinsia ya pekee katika watoto wake wote ( inaweekana kuwa ana watoto kumi lakini wote ni wanawake lakini mmoja ndio mwanaume ), hama namna anavyokuwa akizingatia maagizo ya wazazi wake huyo kupelekea mioyo ya wazazi kuvutiwa naye sana.
Hivyo katika maisha haya: mtoto mara zote uweza kupata kitu baada ya kuomba sana lakini kwa upande mwana anaweza kupata kitu hata bila kuomba kabisa maana jicho la mzazi linakuwa juu yake anapoona mapungufu yoyote juu ya mwana wake, ujitahidi sana kuhakikisha anamtimizia mahitaji yake hata bila ya kuomba na ikitokea mwana ameomba basi hilo ombi linazalisha deni ndani ya moyo wa mzazi na utafuta ufumbuzi wa haraka kwa hali na mali na wakati wote pindi anapomuona mwana kuwa na huzuni hata chembe hali hiyo inakuwa teso katika moyo wa mzazi.
Naam!
Mungu kama baba unaweza ukaishi naye kama mwana au mtoto! Uchaguzi ni wako,
Kwa kifupi, mwana ni mtoto aliyeubeba moyo wa baba yake, anayajua mapenzi ya baba yake na kuishi humo ili azidi kumfurahisha baba yake.
Matendo 13:22 Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.
Mtoto asiye mwana, ni kweli unaweza kuzaliwa na Mungu na kuishi huku mbingu inakutambua lakini ukawa unaishi kwa muono wako.
- Vile unavyotaka na vile unavyojisikia ikawa na nguvu katika maisha yako kuliko agizo ulilopewa.
Hatari inakuja pindi utakapoishi kama mtoto asiye mwana ukataka haki za mwana uzipate, hapo inakuwa sawa na kuhamisha bahari kwa kutumia kikombe.
Maisha ya kuwa mwana au mtoto haya ni maisha mawili tofauti kabisa ila yanabebwa na uchaguzi na mtu husika yanayo dhihirika katika maisha yake ya mtu binafsi japo inawezekana kwa kwa kujua au kuto kujua ila uchaguzi unakuwa umeshaufanya na matokeo ya uchaguzi uwezi kuyakwepa.
Inakupasa kujua kila haki ina sababu yake na pengine unapokosa ujue kunasababu inafanya uikose hiyo haki.
Kama ilivyo kwenye familia unaweza kubadilika kutoka katika mtoto asiye msikivu na kuwa mtoto msikivu ( mtoto kama mwana ), ndivyo hivyo ukitaka vitu vya mwana ni lazima uwe mwana nje hapo utaishia kuvitamani tu.
Mungu anaposema “ utafuteni kwana ufalme wa Mungu na haki yake na mengine yote mtazidishiwa “
Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Kwa lugha nyepesi hapo, Mungu anataka uwe mwana ili uvipate yale baba aliyo kuandalia, maana yeye anajua nini hasa unahitaji kuliko macho yako yanavyo kuonyesha.
Unahitaji sana kupambana kuwa mwana ili matunda ya kuwa mwana yaambatane nawe.
Kuwa mwana ni kumfanya Mungu kuwa tegemeo naye akutegemeze!
Nawezaje kuwa mwana:
i. Kuokoka
ii. Kukua katika wokovu
iii. Maongozi ya Roho mtakatifu.
INAITWA KESHO! BARIKI SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni