Wanasema kizuri kina gharama au kina gharamikiwa!
Inasemekana ukisasa ni mzuri na sikatai ila unagharama yake.
Kwenda na wakati ni jambo jema sana kwakuwa lina mazuri yake mengi lakini vilevile usipouelewa vizuri unaweza kufanyika kuwa teso kwako hata ukawa mtumwa wake badala wewe kufaidika nao.
Mabadiliko katika mambo mengi uwa ni jambo la heri, kwa maana kwa kiasi kikubwa mabadiliko mengi uchochea maendeleo kwa jamii au taifa kwa ujumla wake.
Tatizo linakuja katika jamii tuliyo nayo, ni jamii kubwa imekuwa ikiteseka sana na ukisasa tulionao kuliko kufaidika nao watu upenda kujaribu kila kitu hatimaye kupelekea matatizo mengi; katika upande wa afya, watu wamekuwa wakitengeneza miili yao au kutumia vitu hata kwa namna ambayo haiongezi tija kwao zaidi ya matokeo yake kudhoofisha afya zao mathalani watu wengine uona fahari kuvuta sigara muda wote lakini mwisho wake uweza kusababisha kansa ya mapafu na magonjwa mengine mengi.
Naam watu wengine wametumia ukisasa katika kuharibu jamii badala ya kuwa saidia: mathalani sasa tunaongezeko la mashoga, watu kujiunga na makundi mabaya ( kigaidi, ujangiri n,k), watu kutekwa hasa watoto na wanawake.
Ukisasa umetoa njia rahisi ya kuwafikia watu hao na kufanikisha matendo yasiyofaa kufanyika katika jamii zao.
Na watu wengi kuingia uingia katika ulimbukeni katika mitandao na kukuta wanatumia muda mwingi katika mitandao kuliko shughuli zao au watu wawapendao/wanaowategemea familia na watu wengine.
Viko vitu vingi vipya vinavyotambulishwa katika ulimwengu wa sasa kila siku baadhi yao vikiwa na lengo la kuwa na msaada katika jamii husika ziko dawa zimekuwa zikisemekana zina nguvu ya kuongeza nguvu ya kiume na kwasasa soko lake limekuwa kubwa pia yako madawa mengine yanasemekana yanaweza kupunguza unene/matumbo, miguu na hata maziwa kuwa makubwa na hivyo jamii imejiingiza katika maisha hayo wakiamini ukisasa unalipa,
Na hali hiyo kupelekea kuharibiwa zaidi kuliko kusaidika! Wakati mwingine mtu anagundua kuwa alikosea akiwa katika madhara makubwa, na wakati mwingine inakuwa ni ngumu kutoka hapo.
Na kutokana na ulimbukeni wa wengi imepelekea watu wengi kuamini hata taarifa zisizo kuwa sahihi au za kweli na baadhi ya watu wamepoteza maisha yao kwa kuamini taarifa zisizo sahihi na kuacha pengo katika jamii au familia husika.
Ukweli ukisasa ni kitu kizuri hata kupelekea mambo yote kupatikana kwa urahisi hasa yale yaliyo ya kweli na kusaidia jamii husika, wako watu wamejifunza mambo mbalimbali mitandaoni na kuwa na matokeo chanya mathalani mkimbiaji mmoja toka aliweza kujifunza namna ya kurusha mkuki kwa kasi kupitia mtandao na hatimaye hata kupelekea kuiletea medali ya dhahabu nchi yake kutokana na ushindi alioupata kutokana na mashindano hayo.
Na wengine imepelekea kujifunza mambo mbalimbali na kufaidika na maarifa wanayoyapata kutokana na mitandao mathalani wako watu wamejifunza namna nzuri ya upishi kupitia mitandao na wengine kupata masomo yao kupitia mitandao na mengine mengi.
Ni kweli kabisa maadamu unaishi katika jamii ya kileo uwezi kujitenga na usasa ambao dunia inaenda nao maana kuna baadhi ya watu wanajiingizia fedha nyingi kupitia mitandao kwa halali kabisa,
Ukisasa ( teknolojia) katika dunia ya sasa uwezi kuukwepa ili uyafikie mambo mengi kwa haraka unahitaji kuwa na maarifa sahihi ya hicho kitu ili kikusaidie kuongeza maarifa kwa yale unayoyajua na hata usiyoyajua ili ikusaidie kufanya jambo lilelile katika ubora zaidi wenye tija kwako na jamii kwa ujumla.
Ukisasa umepelekea familia kusambalatika, ndugu kutoelewana kutokana kupenyeza taarifa zisizo sahihi katika fahamu za watu mathalani itikadi kali na imani potofu hata kusababisha kila mtu aamue vile anavyoona sawa pasipo kujilizisha kwa umakini yeye anaamini na kukiishi kile anachoambiwa.
Mahusiano mengi yamekuwa ya kidumu kwa muda wa kitambo na mengine yamekuwa yakivunjika hata kabla ya ndoa na mengine yamevunja baada ya ndoa kutoka na mmoja au wote kutaka kuenenda kama ukisasa unavyotaka ufanye mathalani kutaka kufanya mapenzi kinyume na maumbilena mengine mengi.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni