Uwa njia inatengenezwa na mtu au watu na wala haijitengenezi yenyewe! Ni lazima awepo mtu na aamue pawepo njia ndipo njia utokea,
Na katika utendaji wa Mungu tunaona kuwa ni tabia ya Mungu kufanya njia pasipo na njia! Kwakuwa uweza wake hauna kikomo/hauzuiliki.
Kutoka 14:10 Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia Bwana.
13 Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
- Ni maneno ya musa akiwaambia Israel yakionyesha kuamini neno la Mungu na uweza wake!
Kama binadamu unayeishi katika dunia hii kuna majira unafika unaweza kuona kukumbana na mazingira ambayo sio rafiki/kandamizi unaweza kuona nyuma maadui na mbele bahari ya shamu hapo ni lazima patokee njia ili uweze kupita la sivyo unaweza kuangamia,
Ni kweli watu upenda kupita njia ambayo ipo tayari inatumika pasipo kujua hiyo njia mpaka imekuwa njia kuna mtu ili mgharimu kuifanya ili wengine wafaidike kwa kuitumia, waswahili wanasema “mwanzo ni mgumu”,
Unapopita katika njia ambayo wengine imewagharimu hata ikawepo basi hapo jua nawe unadeni katika kutengeneza njia ili wengine wapite.
Usiogope kuandaa njia kwa ajili ya wengine ili wapite lakini tambua kama na wenzako wangeamua kuogopa wewe leo usingeijua njia unayoipita leo.
Na tambua kupita katika hali ngeni (experirnce) mpya iliyo katika changamoto kwakuwa uwezi kujua hasa matokeo yake yatakuaje! Na hata kama ni jambo ambalo wengine wamepitia na wako salama lakini swali litakuwa kwako ni kweli matokeo aliyoyapata mwingine nawe utayapata au itakuwa tofauti na ikiwa tofauti utakuwa katika hali gani? Mathalani unaweza kuwa muathirika wa ukimwi na ni kweli unaweza kuwa na shuhuda za watu waliopona ukimwi lakini ikija upande wako ni kweli utapona au utakufa? ( maana tunajua sisi tuna amini lakini muamuzi ni Mungu ).
Ni kweli unapopita mahali akili yako inapo kosa mwanga au matumaini basi machozi hapo yanakuwa ni fungu lako.
Niseme tu inaweza ukalia baada ya kujitambua kuwa umekosa au kupoteza matumaini kwani hata yesu mwenyewe alilia hata akatokwa na machozi ya damu lakini lile chozi alikumfanya ashindwe kukamilisha kusudi lake alilopewa na Mungu hapa duniani.
Tatizo sio kulia bali nikuendelea kulia katika hali ya kukosa muelekeo matumaini tena,
Ni muhimu kuwa na fikra pana na usione katika dunia ni wewe pekee ndio mambo yanakusonga kana kwamba jicho la Mungu liko mashariki nawe uko magharibi kwahiyo Mungu haoni kile kinachoendelea katika maisha yako.
Usilie kwa sababu ya kutoa uchungu moyoni kwani baada ya kulia na kama hali haijabadilika basi hapo kilio kitaendelea pasipo kukoma lakini itakuwa tofauti tu mara tumaini jipya litakapo chipuka ndani yako.
Mruhusu Roho mtakatifu alete mwanga au tumaini katika akili yako iliyo na giza maana ni yeye tu awezaye kuifanya njia nawe ukaiona kisha ukachukua maamuzi ya kupita, na lazima uione kutokea ndani yako! Maana ni yeye anayekuonesha njia ambayo wengine hawawezi kuiona mpaka pale umepita ndipo wengine waione njia wapite kwasababu wewe umepita.
Kuna raha sana baada ya wewe kupita na wengine wakaona njia nao wakaanza kupita unakuwa kama mtu aliyejigharimu kujenga nyumba nzuri japo aliteseka lakini furaha yake inakuwa pale atakapoona watu wengine wanakaa humo na kupafurahia yeye uwa furaha yake inazidi hasa akikumbuka namna alivyokosa usingizi na kujinyima ili akamilishe jambo hilo japo anaweza jua kuwa ile gharama aliyoingia kuna mtu anafurahia.
Ni kama yesu furaha yake uwa inaongezeka japo ili mgharimu kufa na kufufuka, ila anapoona kuna watu wanaokolewa yaani wanaifuata njia ambayo yeye aliitengeneza.
Ni sawa na mama mjamzito uwa furaha yake inakuwa nyingi pindi anapo mpakata mtoto wake katika mikono yake japo inawezekana alipita katika hatua ngumu tangu ujauzito hadi kujifungua!
ISHI ILI WENGINE WAISHI!
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni