Ni jambo linalojulikana kuwa kila tendo unalolifanya linaashiria maamuzi uliyoamua ndani yako, na hayo maamuzi yanaweza kuwa ni mabaya au mazuri, na hiyo hali udhihirika katika matokeo ya matendo yako kama yalikuwa mabaya basi matokeo yake yatakuwa hasi…!
Maamuzi ni kitu ambacho mtu ukifanya karibia kila siku ambayo Mungu anampa uhai, maana nje ya uhai hakuna maamuzi yako binafsi bali unaamliwa na wengine ila unapokuwa na uhai unakuwa na uhuru wa kuamua nini ufanye na nini usifanye.
Ni ukweli kabisa kuwa unaweza kubadili maamuzi lakini sio rahisi kubadili matokeo ya maamuzi mathalani unapopata mawazo ya kuua na ukaamua kufanya hayo maamuzi pindi utakapo maliza hilo tukio la kuua bila shaka hautakuwa na nafasi ya kurudisha uhai wake yule uliye muua.
Bila shaka unapokuwa na mawazo sahihi unakuwa na raha na changamko la kweli katika moyo wako au changamko la kudumu katika maisha yako, japo kuna wakati unaweza ukawepo mahali fulani iwe ni kazini au katika hali ya mahusiano au ndoa hata rafiki tu wa kawaida ukajikuta anakushurutisha kufanya mambo ambayo yanatia doa ndani ya moyo wako kwa mfano katika ndoa mara nyingi mwanamke anapojua ameshika mimba uwa anajisikia vizuri sana maana anaona anaongeza heshima yake katika jamii na familia yake husika lakini pindi inapotokea mume wake kusema yeye hayuko tayari kulea kwa sasa bila shaka inakuwa ni huzuni katika moyo wa mwanamke na anaona kama huyu mwanaume amekuwa katiri na wakati mwingine anaweza kukushurutisha ukatoe huo ujauzito hali hiyo inaweza kumfanya kuwepo mahali pasipo kuwa na furaha ya kweli na majuto yakaanza kuchukua nafasi ndani yako.
Lakini hali hiyo ikiendelea na usipopata maamuzi sahihi ya kutoka hapo bila shaka unaweza kufunikwa na giza ukakosa nuru na hatimaye hata kupelekea kuibuka magonjwa ndani yako yasiyo kuwa na tiba.
Unapaswa kujua maamuzi sahihi ni kitu muhimu sana katika maendeleo yoyote maana bila kuwa na maamuzi sahihi kukamilisha ndoto yako ni kitu kigumu maana unaweza kwenda usijue unakwenda wapi?
Ili ujikomboe katika hali yoyote unahitaji kufanya maamuzi yaliyo sahihi yatakayokupa mwanga katika safari yako haijalishi hata kama yatakugharimu kiasi gani au muda gani ili mradi ni sahihi basi utakuwa salama.
Maamuzi sahihi ni kwa ajili yako wewe na maisha ya kizazi chako hata utakapo ondoka hapa duniani kizazi chako kitafurahia kwa maamuzi sahihi uliyo yafanya.
Pia maamuzi hautufanyi tu kwasababu tunataka kufanya maamuzi bali tunafanya kwa ajili ya ustawi wetu wa kesho japo wakati mwingine unaweza usieleweke vizuri na watu, lakini la kuzingatia hayo maamuzi ni lazima ya bebe nia njema kwa watu sio kwa ubaya.
Yakupasa kujua maamuzi sahihi yanaweza kukutambulisha wewe uliye kamili katika hazina ambazo Mungu aliziweka ndani yako, na zile hazina zinapoanza kushamiri ndivyo hivyo wewe unaanza kushamiri.
Katika lugha ya dunia wanasema umejipata au umejivumbua!
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………
…………0764 018535