Ni muhimu kutambua kila mtu ana kona yake ( mahali alipowekwa/alipojiweka ) hivyo anapaswa kuliendea ili aweze kulitumikia hilo eneo.
Unapozungumzia kona unazungumzia mahali unapotoshea, mahali unapofanya jambo huku mwili wako ukiwa unajua kwanini unafanya au nao unaoshughulika ( mahali unapo pafurahia )!
Kona ni mahali ulipokusudiwa kuwepo au uliandikiwa kuwepo ni kamavile samaki kona yake ni mahali penye maji ambapo anapafurahia na wala hajuti kuwepo hapo hata akikaa siku elfu moja katika maji hayo bado furaha yake haipungui.
Kuipenda kona yako ni kujipenda vile ulivyo pasipo kuangalia muonekano gani unakuvutia zaidi, maana wapo baadhi ya watu wakiangalia viungo vyao wanaona kama wameonewa na wengine wakijiangalia katika viungo vyao wanaona kama wamependelewa, kwa wale wanaojiona hawako vizuri huwa wanajiona wametengenezwa pasipo kuwepo kwa umakini mathalani wako watu wakiangalia pua zao, midomo au kosogo chao wanakuta wanajichukia na watu wengine huishia katika mawazo yao mabaya.
Ni lazima uipende kona yako ili uweze kuifaidi na kujisikia vyema katika hali hiyo, pindi utakapo amua kuipenda au kuifurahia kona yako bila shaka utaanza kunawiri na kuwa kivutio kwa watu wengi.
Hauhitaji kuzielewa sana kona za wengine kuliko kona yako, kwakuwa thawabu yako hutegemea katika kuitumikia kona yako.
Ni muhimu kuelewa mahali popote unapowekwa basi ujue baraka zako zimeelekezwa hapo katika kona hiyo sio sehemu nyingine ni lazima uwe hapo ili uweze kupata baraka zako maana zitakuja katika njia hiyo na kukupata endapo zitakukuta katika njia hiyo na ukiwa nje ya kona hiyo hauwezi kuzipata hizo baraka.
Ni muhimu utambue kuwa nyumba inakuwa imara kwakuwa kila kitu kipo kwenye mahali/kona yake, hivyo vitu vinavyokuwa sawa basi hapo utaanza kuona ubora na uzuri wa nyumba, hitilafu yoyote itasababisha kushindwa kuhimili vishindo na kutokaa kwa muda mrefu.
Unapokuwa katika kona yako bila shaka kuna mtu mmoja atakuwa salama kwa wewe kukaa katika kona yako kama vile ambavyo mbao zinapokaa katika namna yake basi mabati huweza kukaa katika namna nzuri na iliyobora.
Unapojikita zaidi katika kuijua kona yako unawezesha na kuimarisha utendaji wako uliobora katika wewe kutoka na mapana, ukubwa na nguvu ya uelewa ulionao.
Hauhitaji kujifananisha au kutamani kona ya mwingine hata kama ukiona kona yako haina mng’ao / kushamiri kama wengine.
Unapaswa kujua kuwa hupo hapa dunia kwasababu ya kuishi katika kona hiyo na sio kutazama au kupongeza kona za watu tu.
Wakati mwingine unaweza kuwa unapitia kipindi kigumu na ukaona wale walioshamiri hawakupitia kipindi hicho bali ni muhimu kujua wako wengi walipitia kipindi kigumu kuliko wakati ulionao wewe, ni muhimu ujue kama Mungu amekuweka hapo atakupa mng’ao wake kwa majira yake.
Yakupasa kujua muunganiko wako mkubwa na Mungu upo kwa wewe kuishi katika kona yako nje ya kona yako utendaji wa Mungu utakuwa mdogo wako kuuona.
Yakupasa kujua KONA YAKO ndio maisha yako hivyo yakupasa uipende kwa ustawi wa maisha yako.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni