Ijumaa, 28 Juni 2024

INGIA NDANI

 



Kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayeongea mambo akiwa ndani na mtu anayeongea mambo akiwa nje! Ni sawa na mtu anaongea mambo anayojua na mwingine hasiye yajua hawa ni watu wawili tofauti na hata ujasiri wao ni tofauti kabisa.

Kitu chochote ili uwe na uhalali/ujasiri wa kukiongelea au kukisema ni lazima ukijue au uwe ndani ya hicho kitu….ndomana waswahili wanasema “ ukitaka kujua uondo wa ngoma uingie ndani na ucheze “

Kwa asilimia kubwa inaaminika mtu aliye ndani ya jambo anakuwa na ushawishi mkubwa wa kusikilizwa mathalani mtu aliyeko kwenye ndoa mwenye umri zaidi ya miaka 50 ndani ya ndoa na ndoa yake ikiwa bado imebeba ubichi/ ustawi mtu huyu anakuwa na nguvu kubwa ya kusikilizwa na watu wengi walio katika ndoa hata wale ambao bado hawajaingia ndani ya ndoa hata kama ataongea sio vitu vya msingi sana lakini yale maisha yake katika ndoa yata mbeba na kumpa ushawishi kwa maana mtu anaongea kitu anachokiishi.

Pia mtu aliye ndani ya huduma kwa muda mrefu na kustawi anakuwa na ujasiri pamoja na ushawishi katika kueleza hali ya huduma ilivyo sawasawa na Mungu alivyompitisha.

Ni muhimu uwe ndani ili uwe miongoni mwa wale unaowasema au kuwawazia yaliyo ndani yako.

Bila shaka hata fahari ya Mungu utaanza kuiona pale utakapokuwa ndani yake, kwakuwa Mungu hawezi kujifunua ukiwa nje yake bali ukiwa ndani yake japo ni Mungu asiye na mipaka.

-          Maana hata utendaji wa Mungu unaanza kuona tokea ndani yako ndipo udhihirike kwa nje.

Naam unapokuwa ndani ya mfumo na uka uelewa mfumo kuna namna sahihi utaongea mambo yanayo husu huo mfumo na hata mapengo yake utaanza kuyaona kwa uhalisia wake na kuweza kuyaziba.

Na unapokuwa ndani uwa utaongea kile unachopaswa kuongea na sio kile unachojisikia kuongea.

Na makosa mengi unaweza kuyaona/kufanya pale unapokuwa nje ya mfumo na pengine hata kuwaza kuona walitakiwa kufanya hili au lile basi mambo yangeenda vizuri.

Bila shaka unapokuwa ndani ya Mungu hapo unaweza kumtambua Mungu kwa mapana yake na yeye kukutambulisha kuwa wewe ni nani?

 Ni kama unaweza kuwa mchoraji au mcheza mpira usiojifahamu lakini watu wanaokuona wakaanza kuona uwezo wako pale unapokuwa uwanjani au katika kuchora na kuanza kukupa njia ya namna ya kufika mbali zaidi.

Jambo lolote utakalojiweka ndani yake ni wazi utalifanya katika usahihi na ufanisi mkubwa na hata kama utatoa hukumu bila shaka utatoa hukumu kama wewe ndo unahukumiwa.

Pindi utakapotokea kufanya jambo na wewe ukawa ndani yake ni vigumu tu kukata tama maana ukiwa ndani ya mazingira hayo kuna hali yako binafsi katika kutaka kufanikiwa kwa gharama yoyote hata pasipo kuvipa nafasi vipaumbele vipingamizi dhidi ya ndoto yako.

Ni muhimu sana jambo lolote unalolifanya uwe ndani yake ili uweze kupata matokeo unayopaswa kuyapata iwe ni kazi ulioajiriwa au uliojiajiri ili uweze kutumia uwezo wako wote na nguvu zako zote katika kuleta matokeo unayopaswa kuyaleta katika shughuli husika.

Mungu anapenda uwe ndani yake ili uweze kupata uwezesho wa kufanya yake na kuwa kile kitu ambacho Mungu anatazamia.

Kufanya jambo ukiwa nje yake kuwa na mwenedelezo uliobora ni ngumu kwa kuwa uifanyi kuwa ni maisha yako/haipo mizizi ya kuimili kishindo cha dhoruba  na mafuriko yanayotaka kukuondoa hapo.

Unapokuwa nje sio rahisi kuwa na mtazamo sahihi!

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………………………………..0764 018535

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni