Neno mipaka katika upande mmoja ni neno nzuri na ni kiashilio chema katika mazingira fulani na maisha ya mwanadamu kwa ujumla wake, maana ina aminika kuwa mwisho wa mpaka wako ndio mwanzo wa mpaka wa mwingine hivyo unavyoishi katika mipaka yako ina maana unaheshimu mipaka ya mwingine.
Kuna mipaka katika vitu vingi mathalani mipaka ya maeneo na maneno, lengo la mipaka ni kutoa muongozo wa nini cha kusema na cha kufanya naam wewe kama binadamu uwa hupaswi kuongea chochote tu bali katika kila jambo kuna mipaka yake mathalani unapoongea na mtu aliyekuzidi umri kuna namna ya kuongea naye na pia kuna maneno ya kuongea naye na unapozingatia mipaka ina maana unamuheshimu yule unayeongea naye hata bila kumwambia shikamoo.
Kama hautazingatia mipaka yako usitegemee wengine wakaiheshimu/kuizingatia, mara nyingi vile unavyoiheshimu mipaka yako ndivyo hivyo wengine watafuata.
Katika maisha tunayoishi kuna hali mbili zinazodhihirika katika maisha ya watu, kuna hali ya kujiwekea mwenyewe mipaka na kuna hali ya kuwekewa mipaka nje ya ridhaa yako, unaweza kuwa unapenda au haupendi hama unajua au haujui lakini unakuwa kifungoni katika maisha usiyoyapenda.
Pia kuna mipaka uliowekewa katika ulimwengu wa roho ambayo inadhihirika katika ulimwengu wa mwili. ( kwa asilimia kubwa mipaka mingi wanadamu wanayotembea nayo huwa imeanzia rohoni ).
Moja ya athari kubwa ya kuishi katika mipaka uliyowekewa ni kuishi katika maisha uliyoamriwa na sio yale unayotaka au kukusudia.
- Hakuna jambo utapanga likaenda, vikwazo vitakuwa ni maisha yako!
Bila shaka unapoishi nje ya wewe basi utakuwa unaishi kwa kujitahidi sana ni sawa sawa na kutaka kuku aishi kama bata au nguruwe aishi kama mbuzi.
- Unaweza kuwa nyima uhuru kuishi katika asili yao lakini baadae watarudi katika asili yao pindi watakapotoka kifungoni.
Kuna mipaka inayotawala maisha yetu:
- Inayotokana na;
a) Wazazi wako
- Kazi gani ufanye?
- Nani umuoe/ uolewe naye?
b) Ukoo
- Yapi yasiyofanyika katika ukoo wako? -Hutayafanya hata kama ni mazuri kiasi gani?
- Yapi yanayofanyika katika maisha yako? -Utayafanya hata kama yanagharimu maisha yako.
c) Binafsi
- Ni kile ulichokikubali na kukifanya kuwa ni maisha yako.
Haya yote yanaweza kukusaidia katika kujifungia geti na kujiwekea kufuri na kuona kuwa ni sawa tu na ndivyo hivyo unapaswa kuishi.
Wakati mwingine mtu h upenda kuishi humo katika simulizi na kuamini kuwa hiyo ndio njia sahihi ya kuishi na wakati mwingine huo mtindo wa maisha unaweza kumweka katika mazingira magumu hata kupelekea kutofurahia maisha yake.
Pia kuna mipaka iliyojitokeza katika maisha yako kutokana na matokeo ya hofu, ulivyofanyiwa na matendo uliyofanya au uliyo yaona kwa macho yako hivyo hali hiyo ikampelekea mipaka katika utendaji wake.
Kuna baadhi ya watu huwa hawaamini kuwa na maisha mazuri, ni mpaka uwe mshirikina au uwe mwizi ndivyo uweze kutoboa/ kushamiri, mbaya zaidi hali hiyo inajijengea hata kwa mtu aliyeokoka na kujazwa na Roho mtakatifu bado haoni hayo maisha yana mhusu au yanawezekana kwake bali hujiweka na kuona ni maisha ya watu wengine.
Kuna baadhi ya watu hawawezi kulala peke yao usiku wanahisi kuna kitu kigumu/kibaya kitatokea au yatamrudia baadhi ya matendo aliyofanyiwa nyuma hivyo huona kulala peke yake ni adhabu.
Pia kuna watu wengine huwa hawanatabia ya kusema kitu hata kama wakishuhudia kwa macho yao ubaya unafanyika au watu wanafanyiana ama yeye binafsi anafanyiwa hata nyamaza kimya hata pale madhara makubwa yatakapojitokeza kwake au kwa jamii husika lakini yote inatokana na mipaka aliyowekewa/ kujiwekea kuwa hatakiwi kusema kila kitu katika maisha yake.
- Unaweza kuwa ni utumwa wa kisakolojia.
Ni muhimu kutambua kuna mipaka ya Mungu na mipaka ya dunia lakini usiruhusu mipaka ya dunia kutawala maisha yako na kukuendesha japo unapaswa kuiheshimu na kuizingatia ila isichukue nafasi ya Mungu katika utendaji wake.
Ni muhimu ujue mipaka yako imebebwa na neno la Mungu sio maneno ya watu ( wakubwa au wadogo )!
Inakupasa kujua neema ya Mungu ipo ili kukufanya uwe bora sio uwe mnyonge.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson……………………………………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni