Jumatatu, 19 Agosti 2024

DUNIA ISIKUANDAE

 v>


 

Dunia ni sehemu salama sana, endapo ukiijua mifumo yake na namna inavyotenda kazi. 
 
Mambo mengi katika hii dunia yanaweza kufanikiwa katika viwango vya juu au vya chini
ni kutokana na maandalizi yake, kwa kiasi kikubwa vile maandalizi yalivyo ndivyo
matokeo yatakavyokuwa nje ya hapo inakuwa bahati tu. 
 
Na kwa asilimia kubwa maandalizi ndiyo yanaamua matokeo yaweje? Mazuri au
mabaya yanategemea maandalizi yake. 
 
Naam hata chakula kiwe kizuri au kibaya vipi kinategemea na umakini katika maandalizi,
hivyo huna haja ya kulaumu chakula bali ujue hiyo ladha ni matokeo ya maandalizi ya
chakula. 
 
Hapa duniani hasa katika nchi zilizoendelea hii dhana ya maandalizi imepewa
kipaumbele sana na katika umakini wa kiwango cha juu sana, kwa kutambua faida
zilizopo katika maandalizi mazuri ili kuendelea kuwa bora katika Nyanja zote za
maendeleo: kiteknolojia, michezo katika ujumla wake, jeshi na hata katika mambo ya
kijamii. 
 
Nchi zilizoendelea huwa haziangalii gharama zinazoingia katika kuandaa vizazi vyao
katika kushika mifumo mbalimbali katika nchi zao, hapo utaifa unakuwa na nguvu kuliko
maslahi binafsi ya watu wachache. 
 
Ni ukweli usiopingika kuwa ili uweze kupata kitu kizuri ni lazima ukiandae vizuri, ukubwa
wa matokeo hutegemea gharama ulizoingia katika maandalizi? 
 
Huwezi kupata matokeo nje ya maandalizi yake! 
 
Huna haja ya kupania kuwa na matokeo mazuri kama maandalizi yako sio mazuri,
( maandalizi ambayo hayasadifu matokeo ). 
 
Naam katika maandalizi ni kitu kizuri sana kama endapo ukawa tayari kuandaliwa,
pindi utakapokubali kuandaliwa basi utakuwa kile kitu kilichokusudiwa kwa uharaka na
wepesi zaidi……katika hali hiyo ya utayari wa kuandaliwa pindi utakapo kuwa unaandaliwa kuwa mtu mzuri bila shaka utakuwa mtu mzuri sana na pindi ukiandaliwa
kuwa mtu mbaya bila shaka utakuwa mbaya sana na ajabu sawasawa na maandalizi
yalivyokuwa. 
 
Katika majira mengine unaweza kukuta mtu anaandaliwa pasipo kujua kama
anaandaliwa na anaweza kuona ni maisha ya kawaida tu baadae hali hiyo inaweza
kuwa sumu polepole katika mwili wake na hatimaye kuwa kile kitu ulichokusudiwa.
 
Dunia ni sayari pendwa, kwani ni moja ya sayari ambayo maisha ya wanadamu uweza
kuwepo na kuendelea kuishi na mwanadamu kuona fahari ya yeye kuwepo hapo.
Kwa kiasi kikubwa dunia inaweza kukuandaa na kuweka sumu katika maisha yako na
hata kukuonyesha njia mbalimbali za kukidhi mahitaji yako kwa njia rahisi sana lakini
imebeba uharibifu mkubwa wenye kuua hatma yako. 
 
Ni hatari sana mtu mwenye maumivu au kusudi lisilo jema anapomuandaa mtu/kitu kwa
ajili ya kulipa kisasi….unaweza kuona unapendwa sana na kupewa kila unachokihitaji
ila ni kwa ajili ya maangamizi yako. 
 
Kwa kiasi kikubwa dunia imebebwa na utawala wa nguvu za giza na yenye kisasi na
Mungu hivyo haitaki watu wamsikilize Mungu na kuandaa mambo mengi mazuri kwa
ajili ya uharibifu wao. 
 
Dunia haina mabaya tu bali ina mema pia kwa baadhi mazuri unayoyaona kuna
mabaya yanapitishwa na wakati mwingine hata wewe pasipo kujua, mathalani misaada
ambayo nchi zinazoendelea zinapokea kutoka nchi zilizoendelea kuna uharibifu mwingi
unapenyezwa kwa mfano kuna nguo au dawa za mswaki zinawekwa homoni za kike na
kupewa wanaume hasa vijana hivyo hukuta hizo homoni zikuwa na nguvu katika miili
ya wanaume na hatimaye kukuta wanapendelea mambo ya kike zaidi kuliko jinsia yao
vile ilivyokuwa mwishowe ushoga huanza kushamiri. 
 
Na unaweza kukuta binti anaolewa na mtu na yeye anajua ni mwanaume kumbe ni
shoga!Pia katika maandalizi ya sayansi na teknolojia unaweza kukuta watu wanajifunza
mambo yaliyo kinyume na maadili: kulawitiana au kusagana kwa kuangalia pia nao
kuiga kujaribu hayo mambo pasipo kujua hatima ya uharibifu uliobebwa na hali hiyo.
Kwa asilimia kubwa mambo mengi unayoyaangalia na kusikiliza toka katika mifumo ya
dunia huwa inakuandaa wewe uje uitumikie dunia kwa kujua au kutokujua. 
 
Usielewe dunia kuliko kumwelewa Mungu maana Mungu atakupa kupambanua hila za
dunia dhidi yako. 
 
Usipojua hauwezi kuwa salama. 
 
Unaweza kukuta watu wengi hawajibidiishi katika shughuli za uzalishaji bali muda
mwingi hutumia katika kubeti na kuangalia series pasipo kujua huo muda wanaoutumia
kufanya hayo mambo yanakutengeneza katika uharibifu wa dunia. 
 
Usipojijali dunia haiwezi kukujali! 
 
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
 
Imeandaliwa na:

            cothey Nelson………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni