Ijumaa, 22 Novemba 2024

USALAMA USIOTIKISIKA

 



Usalama ulivyo ndivyo utendaji unavyoweza kuwa, usalama ukiwa wa kusuasua hata utendaji utakuwa hivyo.

Hauhitaji kuwa na usalama tu unaonekana kwa kuridhisha macho bali unahitaji kuwa na uhalisia huo unaondoa mashaka yote.

Jambo la Mungu sio kuona watu wakifurahia usalama bali ni wewe binafsi uweze kuona fahari ya huo usalama.

- shule inaposherekea kuwa na matokeo mazuri haina maana na wewe ufurahi pasipo kwanza kuangalia matokeo yako. ( unaweza kukuta wote wamefaulu ila wewe umefeli ).

Moja ya fursa inayotazamwa kwa watu wengi ni usalama unao kidhi matakwa ya mtu husika sio usalama uliopo.

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiingia gharama kubwa kwa ajili ya kuhakikisha usalama wao kwanza kabla ya kuangalia vitu vingine.

Maana katika usalama ndipo hapo unaweza kukifurahia kitu ulichonacho au kitu unachokifanya.

Wako watu wako radhi wasile vizuri au kulala sehemu nzuri kama tu ulinzi usipoeleweka.

Na kanuni kubwa ya mtu kujipenda mwenyewe ni uhakika usalama anaupa kipaumbele kwake sio ulinzi wa mwili tu bali hata afya yake anakula nini na kwa ajili ya nini?

Bila shaka tunajua thamani ya kitu ndicho kitaamua ulinzi utakuwa wa namna gani? Mathalani unapozungumzia ulinzi wa Rais,usalama wake ni mkubwa kutokana na thamani yake katika taifa husika.

Mbali na usalama wa mwili unao haribika pia kuna usalama wa muhimu zaidi katika roho yako, unapaswa kujua pindi ya roho yako inapokuwa salama basi maisha yako yako salama.

Maana kwa kiasi kikubwa roho inapovamiwa basi matokeo yake yataonekana katika mwili wako.

Watu walio na mawazo ya kufanya maono makubwa huhakikisha wanakuwa na ulinzi zaidi ya mwilini,huwa wanakuwa na kinga kubwa katika ulimwengu wao. ( roho )!

Unapaswa kujua moja ya kitu muhimu sana katika maisha ni kuwa binafsi katika ulinzi wako.

Kwasababu asili ya binadamu ni ubinafsi hivyo usitegemee usalama wa mtu mwingine utakusaidia na wewe haijalishi anakupenda kiasi gani?

- katika usalama ni muhimu ujiangalie wewe kwanza unaimarika kabla ya usalama mwingine.

Hatua ya kuwa na usalama wa kiungu ni lazima umpokee yesu katika maisha yako ili awe bwana na mokozi ili neema ya Mungu iweze kujifunua kwako.

Hakuna ulinzi mzuri kama Mungu kuwa katika maisha yako yeye anaweza kulinda roho na mwili wako kwa ujumla.

Ulinzi mwingine hauwezi kutoa mwanga au nuru katika maisha yako,maana ulinzi wowote mwisho umebeba giza katika kesho yako zaidi sana unakuwa mwisho wa mateso na usiotamanika.

Mungu pekee ndiye anayejua utakapokuweko na ndio maana upo ili udhihirishe utendaji wake katika maisha yako.

Upande mwingine unatoa ulinzi kwa ajili ya maangamizo yako na sio kuleta ustawi wa maisha yako.

 

“ usalama upo kwa mwenye usalama “

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

 

Imeanddaliwa na:

 

Cothey  Nelson………………………………………………………………………………0764 018535

Ijumaa, 8 Novemba 2024

NGUVU ( GHARAMA ) YA UCHAGUZI



Mafanikio kwa asilimia kubwa hutegemea njia gani uliyo ichagua kuifuata?

Watu wengi wameweza kufanikiwa na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na uchaguzi walioufanya.

Hivyo wakati mwingine hautakiwi kuwalaumu watu au Mungu bali katika uchaguzi uliofanya ndio umekuweka katika hali hiyo.

Na Mungu ni mwaminifu sana anakupa sawa na uchaguzi wako wala habadilishi uchaguzi,

“ Mungu ni mwaminifu chochote upandacho ndicho utakachovuna “

 Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

Unapochagua kulala sana usitegemee kupata matokeo tofauti na hali uliyoichagua bila shaka utapata matokeo yatokanayo na usingizi: uvivu, kuahirisha, kufanya chini ya kiwango na umasikini kupiga hodi.

Ili uchaguzi ukupe matokeo ni lazima ukubali gharama zinazotokana na uchaguzi ulioufanya.

Kumbuka una uchaguzi wa kuamua kufanya jambo lakini matokeo ya kufanya jambo hauwezi kuchagua mathalani unapoamua kupanda mahindi hauwezi kutegemea kuvuna maharage.

Kila hatua au aina ya maamuzi /uchaguzi kuna gharama zake, bila shaka maamuzi madogo hujumuhisha gharama ndogo na maamuzi makubwa hujumuhisha gharama kubwa.

Ili upige hatua kubwa ni muhimu ufanye uchaguzi au maamuzi makubwa, na unapotaka kuwa na ustawi mkubwa  au mavuno makubwa bila shaka unahitaji kulima katika mawanda mapana ukifanya kilimo bora na cha kisasa ukihusisha sayansi na teknolojia ili kuimarisha ndoto yako.

Hauwezi kutegemea matokeo zaidi ya uchaguzi ulioufanya na utakapotaka kufanya maamuzi/ uchaguzi usipokaa na kutafakari gharama utakazo ingia mathalani unapoamua kulima basi ujue kuna gharama utakazo ingia:kutumia muda wako, fedha na vitu vingine vingi na pindi utakapochagua kutolima basi ujue njaa na ukame vitakuwa ni maisha yako.

Moja ya kitu kinachochelewesha mambo kutokea ni pale utakapochagua kuingia katika hatua fulani lakini usiwe tayari kuikabili gharama, na watu wengi wamekuwa na mtazamo usio sahihi katika hatua wanayoipiga mathalani mtu anaweza kuamua kufuga wanyama( mbuzi, kondoo n.k ) pasipo kujua misukosuko utayoipata katika kuwatunza magonjwa, wizi na athari/ matokeo ya tabia nchi tetemeko la ardhi.

 

Ndio maana watu wengi hawadumu katika eneo husika baada ya kuona hali ya kuchafuka hushindwa kuhimiri hicho kishindo na kujikuta kuishia njiani.

 

Mathalani watu wanaweza kuingia katika ndoa na pindi dhoruba inapotokea watu huweza kutoka katika safari ya ndoa, japo kwa asilimia kubwa watu wanapoianza safari uwa wanakuwa na furaha sana lakini machafuko yanapoanza taflani inaanza kutokea mathalani watu/wana ndoa kutoelewana zinaweza kuwa ni sababu za msingi au zisizo za msingi ( inategemea ufahamu wa mtu ): kuchelewa kupata mtoto au kuharibika kwa mimba, mawifi au mama mkwe katika kuonyesha utawala wake katika madhaifu anayoyaona.

 

Unapopenda kitu au kuchagua maamuzi fulani hiyo ni ishara ya kukubali gharama zote kwa kile unachokiendea na kinakupa ujasiri na uhakika wa kile ulichokiiamua.

Yesu alipochagua kutukomboa sisi wanadamu alipotambua/alipofunuliwa mateso yatakayo mkabili lakini alipo yakubali yote hayo yote alidhihirisha yale maamuzi na uchaguzi alioufanya tangu mwanzo hadi mwisho na kusababisha ukombozi uliokamilika/ukamilifu.

Ni kama mwanamke anapokubali kubeba ujauzito anakubali katika hali zote anazozijue au asizozijua ila zinaweza kutokea katika mabadiliko ya mwili wake na hatimaye kumzaa mtoto atakaye ongeza.

Furaha yake katika changamoto alizozipitia au kukabiliana nazo hata kupata kile anachokitaka.

 

Hauwezi kukimbia gharama na huku ukitaka kitu bora.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

 

Cothey Nelson………………………………………………………………………………0764 018535