Ijumaa, 8 Novemba 2024

NGUVU ( GHARAMA ) YA UCHAGUZI



Mafanikio kwa asilimia kubwa hutegemea njia gani uliyo ichagua kuifuata?

Watu wengi wameweza kufanikiwa na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na uchaguzi walioufanya.

Hivyo wakati mwingine hautakiwi kuwalaumu watu au Mungu bali katika uchaguzi uliofanya ndio umekuweka katika hali hiyo.

Na Mungu ni mwaminifu sana anakupa sawa na uchaguzi wako wala habadilishi uchaguzi,

“ Mungu ni mwaminifu chochote upandacho ndicho utakachovuna “

 Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

Unapochagua kulala sana usitegemee kupata matokeo tofauti na hali uliyoichagua bila shaka utapata matokeo yatokanayo na usingizi: uvivu, kuahirisha, kufanya chini ya kiwango na umasikini kupiga hodi.

Ili uchaguzi ukupe matokeo ni lazima ukubali gharama zinazotokana na uchaguzi ulioufanya.

Kumbuka una uchaguzi wa kuamua kufanya jambo lakini matokeo ya kufanya jambo hauwezi kuchagua mathalani unapoamua kupanda mahindi hauwezi kutegemea kuvuna maharage.

Kila hatua au aina ya maamuzi /uchaguzi kuna gharama zake, bila shaka maamuzi madogo hujumuhisha gharama ndogo na maamuzi makubwa hujumuhisha gharama kubwa.

Ili upige hatua kubwa ni muhimu ufanye uchaguzi au maamuzi makubwa, na unapotaka kuwa na ustawi mkubwa  au mavuno makubwa bila shaka unahitaji kulima katika mawanda mapana ukifanya kilimo bora na cha kisasa ukihusisha sayansi na teknolojia ili kuimarisha ndoto yako.

Hauwezi kutegemea matokeo zaidi ya uchaguzi ulioufanya na utakapotaka kufanya maamuzi/ uchaguzi usipokaa na kutafakari gharama utakazo ingia mathalani unapoamua kulima basi ujue kuna gharama utakazo ingia:kutumia muda wako, fedha na vitu vingine vingi na pindi utakapochagua kutolima basi ujue njaa na ukame vitakuwa ni maisha yako.

Moja ya kitu kinachochelewesha mambo kutokea ni pale utakapochagua kuingia katika hatua fulani lakini usiwe tayari kuikabili gharama, na watu wengi wamekuwa na mtazamo usio sahihi katika hatua wanayoipiga mathalani mtu anaweza kuamua kufuga wanyama( mbuzi, kondoo n.k ) pasipo kujua misukosuko utayoipata katika kuwatunza magonjwa, wizi na athari/ matokeo ya tabia nchi tetemeko la ardhi.

 

Ndio maana watu wengi hawadumu katika eneo husika baada ya kuona hali ya kuchafuka hushindwa kuhimiri hicho kishindo na kujikuta kuishia njiani.

 

Mathalani watu wanaweza kuingia katika ndoa na pindi dhoruba inapotokea watu huweza kutoka katika safari ya ndoa, japo kwa asilimia kubwa watu wanapoianza safari uwa wanakuwa na furaha sana lakini machafuko yanapoanza taflani inaanza kutokea mathalani watu/wana ndoa kutoelewana zinaweza kuwa ni sababu za msingi au zisizo za msingi ( inategemea ufahamu wa mtu ): kuchelewa kupata mtoto au kuharibika kwa mimba, mawifi au mama mkwe katika kuonyesha utawala wake katika madhaifu anayoyaona.

 

Unapopenda kitu au kuchagua maamuzi fulani hiyo ni ishara ya kukubali gharama zote kwa kile unachokiendea na kinakupa ujasiri na uhakika wa kile ulichokiiamua.

Yesu alipochagua kutukomboa sisi wanadamu alipotambua/alipofunuliwa mateso yatakayo mkabili lakini alipo yakubali yote hayo yote alidhihirisha yale maamuzi na uchaguzi alioufanya tangu mwanzo hadi mwisho na kusababisha ukombozi uliokamilika/ukamilifu.

Ni kama mwanamke anapokubali kubeba ujauzito anakubali katika hali zote anazozijue au asizozijua ila zinaweza kutokea katika mabadiliko ya mwili wake na hatimaye kumzaa mtoto atakaye ongeza.

Furaha yake katika changamoto alizozipitia au kukabiliana nazo hata kupata kile anachokitaka.

 

Hauwezi kukimbia gharama na huku ukitaka kitu bora.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

 

Cothey Nelson………………………………………………………………………………0764 018535

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni