Ijumaa, 25 Oktoba 2024

MUACHE AISHI NDOTO YAKE

 



Moja ya vitu vinaweza kusababisha kuwepo na uhai katika vionjo vya mwili wako ni hali ya kuishi katika ndoto yako.

Unapoishi katika ndoto yako uhai wa mwili wako unakuwa mkubwa hasa katika hali ya kufurahia pasipo kuangalia hasa nini unapata.

Kuna wakati mwingine ndoto ya mtu inaweza kupingana na uhitaji uliopo kwa sasa,unaweza ukapenda kitu au kukifurahia nje ya undani wako.

Unapokuwa na watu waliochini yako inawezekana ni mtoto/kijana wako wa kumzaa au kumlea kuna namna unapenda wawe ( ndoto yako ) pasipo kujua uchaguzi wako ni tofauti na uchaguzi wake/wao vile unavyoona wewe ni tofauti na wao wanavyoona japo kuna wakati unaweza kuwa sahihi lakini sio wakati wote.

Mara nyingi unaweza kutumia gharama kubwa katika katika kumwandaa mtoto kuingia katika uwanja ambao yeye binafsi hayuko huko,

Gharama zozote utakazo zitumia kumpa maarifa ambayo kwake hayaongezi kitu katika ndoto yake.

Bila shaka mtu anapofanya kitu ambacho sio ndoto yake makosa yanaweza kuwa ni mengi kuliko ufanisi katika jambo husika.

Japo katika ndoto ya mtu husika anaweza kuona kuwa kuna ndoto anayoiyona pia kuna ndoto iliyo ndani yake inayomuongoza.

Na ndoto tunajua ni kile kitu alichowekewa kukifanya ndani yako katika akili na nyama zake ni kitu alichopewa kuja nacho hapa duniani.

Ni ukatiri mkubwa wa kumnyima mtu asiweze kuishi katika ndoto yake,  huu ni ukatiri unaomtesa mtu katika kiroho,kimwili na kihisia.

Mtu hawezi kuwa salama pindi atakapoishi nje ya ndoto yake maana anaweza kutumia nguvu nyingi au muda mrefu ili jambo litokee.

Haupaswi kutumia nguvu ya fedha au nafasi katika kuharibu ndoto ya mtu.

Kwa mtu anayeitambua ndoto asilimia kubwa unaweza kuizuia kwa muda kwa muda sio kuizuia isitokee/kutimia.

Kumwacha mtu kutimiza ndoto yake sio kusema mwache afanye mwenyewe tuone atafika wapi? Bali ni kuhakikisha kile alichonacho kinafanikiwa na kuwa kitu bora katika ulimwengu.

Japo kwa asilimia kubwa kitu kichowekwa ndani ya mtu huwa kinaatamiwa na Mungu kwa kuwa yeye ndiye aliyekiweka ndani yake.

Huwezijua Mungu anapokupa mtu katika kumlea ili aweze kuishi ndoto yako, kwa yeye kuishi katika ndoto yake kunaweza kuleta mwanga katika maisha yako, maana kuwa kama mtu anaye kumulikia taa ili wewe uweze kuona na kupita.

Japo kuna wakati unaweza usielewe sana lakini unahitaji kumuacha ili aweze kuishi kesho na kuifurahia.

Hauhitaji kuelewa kila kitu bali unahitaji kutambua na kuheshimu hiyo nafasi ambayo Mungu amempa.

Matokeo ya mtu kushindwa kuishi ndoto yake ni magumu/ mabaya wakati mwingine anaweza sema ni heri asingezaliwa.

 

Muache aishi ndoto yake kwa furaha ya maisha yake!

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

 

Imeandaliwa na:

 

Cothey  Nelson………………………………………………………………………………….0764 018535

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni