Ijumaa, 11 Oktoba 2024

MFANYE AWE RAFIKI YAKO KWANZA:

 



Hakuna kitu kizuri kama kufanya jambo na rafiki yako ( mtu unaye mpenda na kumthamini ), kila kitu akikifanya kwako tabasamu halikauki sio la nje bali ni lile lililoshika moyo wake, hapo tahadhari inapotea na hali ya kuamini katika hali ya juu uweza kuchukua nafasi.

Kuchoka au kukelwa ama upweke  hutoweka kabisa kadili mnavyozidi kuwa pamoja, ndivyo unatamani aendelee kukaa nae maana kadili anavyozidi kukaa nawe ndivyo kiu ya kuwa nae inazidi.

Kama ni ulimwengu mzuri basi ni kuishi na rafiki yako katika hali zote njema na zisizo njema.

Unahitaji kumpata rafiki ambaye anatambua maana ya URAFIKI NA SIO UNAFIKI. ( ni mtu anayejiona yeye ndani yako )!

Karibu!

Sote tunajua urafiki hauna kanuni ya kulazimisha bali ni swala la uhiari na utayari unaounganishwa na sababu zilizo nje ya uwezo wenu ( sababu zisizopanga bali zilizojipanga )!

- Ni swala la makubaliano la uhiari na kila mtu akiwa na deni na mwenzake.

Kila mtu ni lazima aone umuhimu wa kuwa na urafiki huo na aufurahie kwa dhati ( kutoka moyoni mwake ).

Na moja ya kitu kinachoweza kukupa wepesi kupata uhitaji wako kutoka kwa mtu ni lazima awe rafiki yako kwanza.

Urafiki ni njia rahisi ya kuingiliana na mtu na kuupata moyo wake.

Inakuwa ni rahisi sana kwa mtu kufungua moyo wake kwa mtu akitambua huyu ni rafiki yangu atanistili na kunisaidia kama sio kwa kitu basi hata kwa ushauri tu maana anajua katika kila jambo kuna mazingira yaliyo zungukwa na pendo la dhati ( Mungu ).

Watu wengi wanakosa kupata kile wanachokihitaji kutoka kwa mtu iwe ni fedha au hali ya moyo wake kwa kutumia nguvu au ushawishi mwingine lakini hauna tija au matokeo chanya.

Hii kanuni ya kumfanya awe rafiki yako haijawahi kushindwa katika kile unachokitaka.

Kama unataka kuvipata vitu vya mtu hakikisha unakuwa na urafiki na mtu kwanza kabla ya kuwa na urafiki na vitu alivyo navyo.

Mithali 14:20 Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi.

Japo kuna usemi “ tajiri anakuwa na marafiki wengi lakini maskini hana rafiki “

Mithali 19:4 Utajiri huongeza rafiki wengi; Bali maskini hutengwa na rafiki yake.

- Urafiki wa namna hii unakuwa sio wakudumu maana inakuwa ni swala la ubinafsi zaidi kuliko ustawi wa wote.

Mahali penye urafiki wa kweli hutangulizwa au huongozwa na upendo wa kujigharimu kwa wote.

Biblia inasema “ hakuna mwenye upendo kama huu wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake”

 Yohana 15:13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

“ siwaiti tena watumwa tena ninyi ni rafiki zangu “

Yohana 15:15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.

 16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

 Yohana 15:14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.

Yesu anaonyesha namna jicho lake linavyotafsiri urafiki.

 

Upendo wa kweli ndio sakafu ya urafiki wa dhati.

 

- kujiona yeye ndio wewe na wewe ukajiona ndani yake!

 

 Manenno ya jonathani akimwambia dauli.. “ roho yangu itaenda nawe popote utakapo kuwepo “

1 Samweli 18:1 Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.

Unapaswa kujua mtu mwenye akili anawekeza mahali ambapo atajua atapata faida/ matokeo mazuri, hivyo urafiki ( urafiki wa kweli usio na unafiki ndani yake ) ni sehemu sahihi kwa mtu kuwekeza ili kupata matokeo mazuri.

Unapokuwa na urafiki na mtu hauhitaji kutumia nguvu nyingi ili kupata kile kinachoendelea katika moyo wake maana katika mazingira hayo mtu huweza kuwa wazi hata kama hujamuuliza hali yake kwa kuwa yeye mwenyewe hujisikia kuwa mdeni kukuambia chote kinachoendelea ndani yake.

 

Ndio maana katika taasisi za ulinzi zenye weledi pindi wanapotaka kujiridhisha uharifu wa mtu hutumia mtu katika kuanzisha mahusiano naye ili kujua yote yanayoendelea katika maisha ya mtu pasipo kutumia njia ngumu katika kubaini uharifu unaofanywa na mtu husika.

 

Ni chizi tu ndiye anayepewa upendo wa dhati ( sio lazima awe mpenzi ) akashindwa kuupokea kila mtu mwenye akili ni lazima apokee pendo la dhati maana pendo la dhati ni kama maji kila mtu ni lazima atatumia tu maadamu anaishi tu.

 

Urafiki wa kweli ni hatua nzuri wa kutimiza mafanikio yako.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………………………………..0764 018535

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni