Jumapili, 29 Septemba 2024

KUMWAMINI MUNGU

 



Moja ya swali kubwa katika dunia ya leo ni nani ni MWAMINI?

Na ambaye nitamwamini naye akadumu katika kuaminika pasipo kukengeuka au kurubuniwa na kitu chochote.

Naam kama binadamu wote wangekuwa wa kweli na wa kuaminika basi swali hili ni mwamini nani? Lisingekuwepo ama lisingekuwa na nguvu katika jamii ya leo.

Wako baadhi ya watu katika dunia ya leo wanaogopa kuanzisha biashara kwa kuhofia kupoteza mtaji na nani nitasimama naye ,tukawa na lengo moja, pia wako wengine wamekuwa waoga kutoa mioyo yao kwa mtu maana wanahofia kunaweza kusiwe salama kule anakouweka au kwa yule anaye dhamiria kumkabidhi moyo wake.

Naam neno hili” kuamini” limekuwa adimu katika dunia ya leo! Maana mtu ili aamini kuwa mtu au kitu chake hakitakuwa hasara bali kitakuwa faida imekuwa ni mtihani sana.

Wako watu waliamini watu na kujiachia kwao na kuamini wako salama lakini mwisho ikawa ni kilio na machozi.

Na wako wafanya biashara waliweka imani zao kwa watu wengine na kuweka fedha zao katika biashara zao  katika biashara waliokubaliana wanaweza kuanza vizuri lakini mwisho akakuta ameanguka mahali asipopategemea.

Na wako watu kutokana na mikasa ya maisha waliyopitia kutokana na kuwaamini watu na kuangukia katika madhara makubwa ikapelekea hali ya kukosa imani na mtu yeyote hata mzazi wake bado ana mashaka naye.

Tunaweza kukubaliana kuwa kumwamini mtu imekuwa bidhaa adimu kiasi cha kupoteza radha ya wewe kuishi na kufurahia maisha na watu wengine, maana wako wanakutwa katika maangamizi au kufilisiwa na mtu wa karibu yake ama mtu asiyemdhania kabisa.

- Maana unaweza kukuta umenyweshwa sumu na rafiki yako kipenzi.

Katika hayo yote pia tunakubaliana kuwa kadiri unavyo mwamini viambaza vilivyo ndani ya moyo wako vinazidi kuvunjika vikiwemo hofu na mashaka vinakuwa mbali nawe.

Pia ni dhana ya kawaida pindi utakapoamua kuishi na mtu ndivyo unaweza kujikuta una muamini au kutomwamini.

Maana katika kuishi na mtu unaweza kumpa mitego mbalimbali itakayokupa uhakika na kama aliweza kufanya jambo hili basi atakuwa ni mtu wa namna hii na unaweza kuona kuwa anaweza kuwa anakufaa au kutokufaa.

Hii njia haina uhakika wa asilimia zote kwani wakati mwingine mtu uweza kubadilika kutoka na mazingira husika na aina ya watu anaokutana nao ( maana watu unaowakuta unaweza kuwabadilisha au kubadilishwa ).

Kuamini imekuwa ni mtihani katika dunia ya leo kwakuwa unaweza kuanza kuamini na hata kujivunia kwa watu lakini ukakuta mwisho amekuacha njia panda na hata ukakosa nguvu ya kuendelea.

Hali imepelekea hata kuwa na maisha ambayo yako tayari kwa lolote kupata faida au hasara atakuwa anafanya mambo yote kama kucheza bahati nasibu.

Hali hiyo ilivyo changamoto kwa wanadamu katika kuaminiana ndivyo hivyo ilivyo changamoto kwa mwanadamu mbele za Mungu katika kuishi imani.

Maana Mungu anapomchagua mtu na kumwamini kwa ajili ya kazi yake huwa anatoa muongozo mapema ili ujue kila maamuzi utakayofanya ni matokeo gani utayoyapata?

1 wafalme 2:1 Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema,

 2 Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume;

 3 uyashike mausia ya Bwana, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;

Torati 30:17 Lakini moyo wako ukikengeuka, usipotaka kusikiza, lakini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia;

 18 nawahubiri hivi leo hakika mtaangamia; hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi, uivukiayo Yordani, uingie kuimiliki.

Hivyo upande wa Mungu yeye habadiliki bali ni wewe ndio unabadilika na matokeo yatafuatana nawe pasipo kukupendelea au kukuonea.

Unapaswa kujua kumwamini Mungu ni kinga tosha katika maisha yako ya sasa na maisha yako ya baadae.

Unapaswa kujua unapofanikiwa kumwamini Mungu basi hapo ni hatua nzuri katika kutembea katika njia yake na akiwa upande wako unakuwa mshindi.

- Hapo furaha, nguvu na ushindi wake unakuwa juu yako, kwa kuwa katika maisha ya kumwamini basi vitu vyake vinakuwa vyako kwa kuwa yeye anaishi ndani yako.

 

KUMWAMINI MUNGU NINI MAANA YAKE?

- Ni hali ya moyo wako kuishi katika neno lake Mungu,

Mithali 7:1 Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako.

 2 Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.

 3 Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

Maana nje ya neno lake hakuna kumwamini.

Maana ili umwamini ni lazima umjue Mungu katika ufunuo wake na sio kusoma biblia tu pasipo kuwa na matokeo.

Mungu ndiye anakuandaa ili umwamini nawe ndipo hapo unaweza kumwamini.

Pia ni muhimu kuzingatia ili umwamini Mungu ni lazima uwe kwenye fundisho sahihi la Mungu na sio maneno yenye ushawishi wa wanadamu.

Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.

Unapofanikiwa katika kumwamini basi hapo Mungu anakukutanisha na watu sahihi nao watakuwa Baraka kwako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni