Ijumaa, 13 Septemba 2024

UPEKEE WAKO

 

Kitu pekee kinachofanya mtu huyu achukuliwe na huyu asichukuliwe na wakati wote wanaweza kuwa na sifa zinazolingana ni UPEKEE WA MTU HUSIKA, unafanya huyu kuwa na mvuto zaidi kuliko mwingine/wengine.

Naaam hata katika mazingira ya kazi au katika kuoa/kuolewa, hali hii inaweza kutokea maana wote wanaweza kuwa na muonekano mmoja na sifa zinazofanana lakini unaweza kukuta kwanini wewe unachukuliwa/ unachaguliwa na huyu anaachwa.

Bila shaka upekee wako ndio silaha yako au mvuto wako ama ndio kinga yako.

Japo katika dunia wako watu wanaishi wanajiita fungu la kukosa, hao wanasema kwao riziki zimewapitia kushoto lakini kama wakijiangalia vizuri wanaweza wasione kama wanasifa hizo mbaya.

Unahitaji kuutambua upekee wako katika kuishi ili uwe na matokeo chanya katika maisha yako.

Vile ulivyo unapaswa kujua Mungu ameona kuna sababu ya kukuweka hivyo haijalishi picha gani watu wanaiona kwa ajili yako, vyovyote vile ulivyo  Mungu anaweza kukufanya kitu bora katika jamii husika.

Ni wewe tu, vile unaweza kuona kuwa sio kitu bora ukatamani vitu vya wengine au ukasubiri mtu aje akuambie upekee wako mathalani usiwe kama jamii ya afrika hapo awali, walikuwa wanachezea madini pasipo kujua thamani yake na muda unapopita ndipo wanaanza kutambua thamani yake wakati wameshachelewa.

Unahitaji kujua upekee wako ndio hazina yako mathalani unaweza usiwe na miguu lakini Mungu amekupa akili na unaweza usiwe na hivyo lakini Mungu akukupa nguvu ambayo inaweza kufanya mambo ambayo wengi hawawezi kufanya.

Yakupasa kujua kwamba Mungu apendelei hawa na hawa hawapendelei bali uwa anafanya mambo kwa ajili ya faida yako na kwa utukufu wake.

Unahitaji kumwamini Mungu kupitia upekee wako ili uyaone matunda ya Mungu.

Moja ya kitu kinachoweza kufanya ujione katika upekee wako ni vile /kutambua kuwa hakuna aliyebora mbele za Mungu wote mko sawa mbele zake maana mmetoka kwake kwa namna tofauti tofauti sawa apendavyo yeye.

Unahitaji kujua Mungu anampango kamili na wewe kama alivyo na mpango na wengine wale unao watamani, maana ni Mungu awezaye kufanya mambo yote pasipo kupendelea.

Pindi utakapo jikubali na kuanza kuishi katika upekee wako hapo bila shaka utaanza kuona/kutambua kwanini Mungu alifanya hivyo na hakufanya vile.

Unahitaji kuwa imara katika kusimamia upekee wako maana kwa huo ndio Mungu hujitukuza sana.

Unapowatamani wengine ni muhimu ujue nao walijikubali katika upekee wao na Mungu akawagharisha katika yale wanayo yafanya hivyo nawe ukitembea katika upekee wako basi nawe utakuwa mfano kwa wengine.

Unapotembea katika upekee kuna nguvu inazaliwa hapo katika kukusimamisha na kuwa na mwendelezo mwema katika ubora unaoimarika siku hadi siku.

Unapaswa kujiamini katika upekee wako ili kudhihirisha Mungu hakosei na anafanya yale anayo yakusudia sawasawa na mapenzi yake.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni