Moja ya sababu ya kutembea ni kusikia na ukisikia vizuri utatembea vizuri na ukisikia vibaya bila shaka utatembea vibaya.
Bila shaka mpaka umeamua kutembea basi kuna mahali unaelekea hivyo maelekezo sahihi yatakupelekea kufika katika hatua/mahali unapoelekea.
Pindi unapoanza kutembea bila shaka sauti nyingi utazisikia zikikupa maelekezo yake na zikiwa za maslahi yao binafsi.
Inakupasa kujua hakuna sauti isiyokuwa na maana na lengo, ila wewe binafsi unaweza usiijue ila tambua kila sauti imebeba maana na kusudi fulani.
Mambo mengi kabla hujaanza kuyafanya mara nyingi kunakuwa na sauti inasema toka ndani yako ikiambatana na sauti nyingi utazisikia , na baadhi ya sauti zinakuwa na nguvu ndani yako hata kama hazina hoja za msingi uweze kufanya maamuzi hayo.
Wakati mwingine unapoanza safari/ jambo panakuwa na ushwari lakini pindi panapotokea mawimbi katika bahari na chombo kikianza kupoteza muelekeo hapo utaanza kuzisikia sauti nyingi zikiongea kwa lengo lake.
Mathalani pale biashara inapoanza kwenda kombo hapo sauti nyingi unaweza kuzisikia:
a) Funga biashara
b) Tafuta biashara nyingine
c) Ongeza bidhaa zingine
d) Hama mtaa
Na ujue maamuzi utakayo ya chukua yana matokeo yake!
Na kumbuka kila sauti ina ushawishi wake na ladha yake unaweza kusema uongo au kweli.
Unapaswa kujua sauti unayoisikia inaweza kuharibu hatma au kuitunza.
Unapaswa kuwa makini sana na sauti gani unapaswa kuisikia katika kule unako taka kwenda au kuelekea inaweza kujikuta kadili unavyoendelea ndivyo nguvu zako zinaisha.
Ni vizuri sana utake kuisikia sauti ya Mungu, maana kuifuata sauti na kuikubali basi umemkubali mwenyewe.
Unapaswa kujua sauti ya Mungu imebeba uzima na hatma njema kwa ajili yako japo kuna wakati unaweza usiione kama ya kweli au utakuwa kama vile ulivyosikia.
Ni muhimu udhihirishe sauti gani unaifuata hata katika mazingira yanayopingana na sauti hiyo.
Tabia ya sauti ya Mungu:
a) Inapingana na matakwa ya mwili
b) Inapingana na uhalisia wa dunia
c) Hahitaji uelewa sana wa akili yako
d) Hahitaji maandalizi ya mwili ili utekeleze makusudi yake.
Kama haufuati sauti ya Mungu basi hauwezi kumfuata Mungu na hauwezi kumpendeza Mungu.
- unapaswa kuifuata sauti yake ili uwe vile sauti yake inataka uwe.
Ndani ya kutembea katika sauti yake hapo ndipo unaweza kumjua Mungu na uweza wa nguvu zake.
Unapaswa kujua pindi unapoikubali sauti yake kuna vitisho vingi vitaibuka kama sauti ya wageni ili vikutoe katika njia sahihi.
Unapaswa kuipenda na kuijua sauti yake ili uwe salama.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………………………………….0764 018535