Ni rahisi kutulia katika mazingira yanayo ruhusu kutulia lakini ni vigumu kutulia katika mazingira yasiyo ruhusu utulivu kuwepo!
Ni rahisi kutulia katika mazingira ya utulivu.
- sio rahisi kutulia mahali penye vita.
“ nguvu ya kutulia “ ni nguvu ikuwezeshayo kutulia mahali ambapo hata hakuna sababu ya kutulia.
Hivyo unahitaji hiyo nguvu ili uweze kutulia.
Moja mahali ambapo panazaliwa majibu mazuri na yenye nguvu ni mahali pa utulivu.
Inaaminika ni ngumu sana kukosea pindi unapoamua maamuzi katika utulivu na sio katika mihemko.
Kuna mambo ya kitokea watu hata waongee nini? Wakupeleke wapi? Wakitafuta kukupatia raha au kuhakikiksha unapata utulivu mzuri lakini katika hayo yote kuna uwezekano mkubwa usipate utulivu unaoutaka.
Kwa asilimia kubwa kuna uwezekano uko pekee yako na mambo makubwa yamekufika lakini pindi nguvu ile itakapo dhihirika utaona utulivu wenyewe unaanza kuchomoza ndani yako.
Yako madhara mengi tunaona yanatokea katika dunia ya leo ni matokeo ya watu kufanya mambo pasipo kuwa na hali ya utulivu.
Kuna baadhi ya matukio yakitokea unaweza kusema haya mambo yanawezekana? mathalani unaweza kukuta mtu kamchoma moto mke wake wa ndoa mpaka majivu.
- haya ni mambo yanayoweza kukuacha katika maswali zaidi kuliko majibu.
Utulivu sio mmea unajiotea wenyewe tu bali kuna mazingira yakiwepo yanazalisha utulivu ndani yako.
² Mambo yanayoweza kuzalisha utulivu ndani yako:
I. Maarifa uliyonayo na juu jambo husika
II. Imani yako kwa Mungu
I. Maarifa uliyonayo juu ya jambo husika
Moja ya kitu kinachoweza kufanya uendelee kuwepo sehemu husika ni hali ya ufahamu iliyo njema iliyo ndani yako.
Unaweza kukuta watu wote wakimuona simba wanakimbia lakini wewe unaweza kumshika manyoya na hata kucheza naye hata kama ana njaa kiasi gani?
Maarifa sahihi ni kinga nzuri dhidi ya uharibifu wa kimwili na kiroho.
- maarifa sahihi hukupa mwanga katika jambo/giza lolote linalo kukabili.
- kuna baadhi ya mambo hautashtuka kama wengine sio kwasababu hayatishi bali kwasababu unayo maarifa sahihi.
Ujinga ni uwanja mzuri wa shetani/watu kukuharibu ama kushindwa kwenda mbele.
Kuna baadhi ya mambo unahitaji maarifa tu ili ushinde na sio kitu kingine.
- unaweza kupewa maji na ukaambiwa hii dawa inayotibu maradhi mengi sana kumbe ametumia ujinga wako/hali ya kutojua ili kukuangamiza.
Ii. Imani yako kwa Mungu
“ imani “ ni kitu pekee kinacho jaribiwa na sio kitu kingine.
- shetani akifanikiwa kuipindua imani yako wewe hauwezi kumsumbua tena.
Mambo yanapokuwa tafrani hapo kinachopimwa ni imani yako imeungamanika na nini?
² Ayubu
Ayubu 1:6 Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.
7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.
8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.
9 Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure?
10 Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.
11 Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.
12 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.
Wako wengine imani zao zimeungamanika na shughuli zao/ mahusiano yao hivyohivyo mambo yaki yumba mtu huyu anakosa mwelekeo.
Yakupasa kujua imani yako kwa Mungu ni kitu muhimu sana, maana huo ndio mkono wa Mungu katika kukupatia utulivu.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni