Usalama ulivyo ndivyo utendaji unavyoweza kuwa, usalama ukiwa wa kusuasua hata utendaji utakuwa hivyo.
Hauhitaji kuwa na usalama tu unaonekana kwa kuridhisha macho bali unahitaji kuwa na uhalisia huo usalam unaondoa mashaka yote.
Jambo la Mungu sio kuona watu wakifurahia usalama bali ni wewe binafsi uweze kuona fahari ya huo usalama.
- shule inaposherekea kuwa na matokeo mazuri haina maana na wewe ufurahi pasipo kwanza kuangalia matokeo yako. ( unaweza kukuta wote wamefaulu ila wewe umefeli ).
Moja ya fursa inayotazamwa kwa watu wengi ni usalama unao kidhi matakwa ya mtu husika sio usalama uliopo.
Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiingia gharama kubwa kwa ajili ya kuhakikisha usalama wao kwanza kabla ya kuangalia vitu vingine.
Maana katika usalama ndipo hapo unaweza kukifurahia kitu ulichonacho au kitu unachokifanya.
Wako watu wako radhi wasile vizuri au kulala sehemu nzuri kama tu ulinzi usipoeleweka.
Na kanuni kubwa ya mtu kujipenda mwenyewe ni uhakika usalama anaupa kipaumbele kwake sio ulinzi wa mwili tu bali hata afya yake anakula nini na kwa ajili ya nini?
Bila shaka tunajua thamani ya kitu ndicho kitaamua ulinzi utakuwa wa namna gani? Mathalani unapozungumzia ulinzi wa Rais,usalama wake ni mkubwa kutokana na thamani yake katika taifa husika.
Mbali na usalama wa mwili unao haribika pia kuna usalama wa muhimu zaidi katika roho yako, unapaswa kujua pindi ya roho yako inapokuwa salama basi maisha yako yako salama.
Maana kwa kiasi kikubwa roho inapovamiwa basi matokeo yake yataonekana katika mwili wako.
Watu walio na mawazo ya kufanya maono makubwa huhakikisha wanakuwa na ulinzi zaidi ya mwilini,huwa wanakuwa na kinga kubwa katika ulimwengu wao. ( roho )!
Unapaswa kujua moja ya kitu muhimu sana katika maisha ni kuwa binafsi katika ulinzi wako.
Kwasababu asili ya binadamu ni ubinafsi hivyo usitegemee usalama wa mtu mwingine utakusaidia na wewe haijalishi anakupenda kiasi gani?
- katika usalama ni muhimu ujiangalie wewe kwanza unaimarika kabla ya usalama mwingine.
Hatua ya kuwa na usalama wa kiungu ni lazima umpokee yesu katika maisha yako ili awe bwana na mwokozi ili neema ya Mungu iweze kujifunua kwako.
Hakuna ulinzi mzuri kama Mungu kuwa katika maisha yako yeye anaweza kulinda roho na mwili wako kwa ujumla.
Ulinzi mwingine hauwezi kutoa mwanga au nuru katika maisha yako,maana ulinzi wowote mwisho umebeba giza katika kesho yako na zaidi sana unakuwa mwisho wa mateso na usiotamanika.
Mungu pekee ndiye anayejua utakapokuweko na ndio maana upo ili udhihirishe utendaji wake katika maisha yako.
Upande mwingine unatoa ulinzi kwa ajili ya maangamizo yako na sio kuleta ustawi wa maisha yako.
“ usalama upo kwa mwenye usalama “
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeanddaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………………………………0764 018535