Tatizo linakuwa tatizo pale unapokosa ufumbuzi lakini pindi unapo pata ufumbuzi linakuwa sio tatizo tena, mathalani. Unapokuwa na gari ukahisi mafuta uliyonayo hayatoshi kukufikisha katika safari yako na uko katikati ya safari pindi unapokosa uhakika wa kupata mafuta hapo linakuwa tatizo lakini pindi unapo pata uhakikia wa kupata mafuta basi hapo linakuwa sio tatizo tena.
Karibu!
Majira ni vipindi mbalimbali vinavyo kamilisha mzunguko wa kitu/ jambo fulani:
Katika upande wa mimea kuna majira makuu mawili:
a) Kuoza baada ya kufukiwa - mbegu ( kipindi kigumu, kufinyangwa,kuandaliwa kuwa mtu mkuu ).
b) Kuchomoza kutoka ardhini ( kuinuka kwako ).
Moja ya kitu kinachoweza kusababisha taharuki, mfadhaiko au mshangao ni hali ya kukosa uelewa sahihi juu ya jambo/ hali husika.
Maana utakapo tambua haya ni majira ya joto hauta pambana kutafuta makoti mazito ili uwe nayo wakati unajua yatakuumiza na sio kukusaidia.
Katika maisha ya dunia tuliyonayo kuna majira ya kila jambo: kuna majira ya kulima na majira ya kuvuna na majira mengine katika dunia ya sasa.
Pia kuna majira ya kuwa na kitu/ vingi pia kuna majira ya kuwa na vichache vilevile kuna majira ya kulia, pia kuna majira ya kucheka pia kuna majira ya kuongea pia kuna majira ya kukaa kimya.
Hauwezi kuleta vichekesho/kutaka watu wacheke katika msiba, maana hayo majira ni ya utulivu na yana hitaji neno la faraja litakalo wafanya wafiwa waendelee mbele.
Vivyo hivyo kama mkristo/mtu aliye okoka kuna majira ya kuwa pekee yako kwanza ili uimarishe ushirika wako na Mungu upate maongozi ya kwenda mbele katika majira hayo usitafute kuwa na watu wa karibu ili uongee nao ili upate changamko la moyo, Mungu aliye ruhusu uingie katika majira hayo yeye peke yake anaweza kufanyika changamko la kweli na la kudumu katika moyo wako.
Pia kuna majira Mungu anaweza kukuonyesha uhalisia wa watu hayo sio majira / fursa ya kuanza kuwasema vibaya bali ni majira ya kuona watu hao na wewe wote mnamwihitaji Mungu kwa asilimia kubwa pia itakusaidia kufanya maamuzi sahihi ukitambua hao ni binadamu.
Pia yako majira ambayo Mungu ataruhusu watu wengi wasikuelewe kabisa, usitafute makundi ya watu watakao kuwa upande wako maana kwa asilimia kubwa makundi unayo yatafuta kwa akili zako mwisho wanafanyika maumivu na sio baraka bali Mungu akiona haja anaweza kuwaleta watu wenyewe watakao kuwa baraka kwako.
Baadhi ya mizigo katika moyo na akili yako itaisha pindi utakapo tambua kwanini huko hapo na kujua ni Mungu amekuweka na wala sio wanadamu hivyo utazidi kumwangalia Mungu zaidi ya kuangalia watu.
Natambua hakuna kipindi kigumu kama kipindi cha kutengenezwa hiki ni kipindi ambacho unaweza kuona nyekundu kuwa njano maana unaingizwa katika eneo lingine ambalo haujawahi kuwepo au haujawahi kutegemea.
Unapaswa kujua mawazo ya Mungu kwako hayawezi kukoma hata majira yakome, maana ni yeye aliyekujua kabla h ujaja ulimwenguni na akaruhusu kuwepo hata ukafika hapo ulipo sasa.
Kama aliweza kuruhusu ukazaliwa basi anao uwezo wa kukamilisha kusudi lake katika maisha yako.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni