Ijumaa, 23 Mei 2025

AKILI YA MUNGU

 


Kitu pekee kinachoweza kumtambulisha mtu na hata kumweka katika nafasi ya ustawi wake ni MATUMIZI SAHIHI YA AKILI YAKE.

Hivyo akili yako inaweza kukutambulisha katika mazingira ya juu au ya chini.

Hivyo watu wanapoyaangalia mazingira yako inatoa tafsiri ya maarifa uliyo nayo yanayopelekea matumizi ya akili yako.

Kinachoonekana kinaongea zaidi kuliko kile unachokiongea.

Naam sote tunajua……Akili ya Mungu haiwezi kushindwa wala haina tabia ya mashindano.

Pia moja ya sifa kubwa ya akili ya Mungu ni KUTOCHOKA.

 Warumi 12:2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Namna unavyoendesha mambo inatoa tafsiri juu ya akili yako jinsi ilivyo.

Katika dunia ya leo kuna mifumo mingi……Mfumo unaweza kukutengeneza na kukupa akili yake nawe ukakuta unatembea humo kwa kujua au kutokujua.

Bila shaka unapopata kuielewa akili ya mtu ndivyo unavyoweza kumwakilisha vyema, kwa kuwa utafanya sawasawa na matakwa ya akili yake naye atakuwa wewe.

Unapoivaa akili ya mtu basi unabeba na utendaji wa mtu, ndo maana unaweza kusikia mtu akisema “ jinsi anavyofanya ni kama mjomba wake alivyokuwa akifanya”

Akili ya mtu imebeba utendaji wa mtu husika.

Na maajabu ya mtu katika utendaji utegemea uwezo wa akili yake.

Katika akili ya Mungu unapopata tabia za Mungu ambazo unadhihirika katika utendaji wako.

Tabia za akili ya Mungu:

(a) Haina tafsiri/ maana ya kushindwa

(b) Ina matumaini yasiyozuilika

(c) Mashaka/ hofu/ wasiwasi haupo ndani yake.

Unahitaji kuamini kuwa unaweza kufanya mambo mengi pindi utakapotembea kwenye akili ya Mungu.

Tuna pozungumzia akili ya Mungu tunazungumzia ni upeo ambao Mungu anakupa katika kufanya mambo mbalimbali ili kuleta ufumbuzi katika jamii yako unaweza kuwa umeokoka au hujaokoka.

Lakini akili ya Mungu kwa uhalisia tuna maana ni ROHO MTAKATIFU yeye huyu ana magawanyo mengi lakini moja wapo ni kukupa akili ya Mungu ili uweze kufanya yale uliyopaswa katika kiwango cha Mungu.

Ili upate matokeo ya KIMungu ni lazima utembee katika akili yake, maana ndani ya akili ya Mungu kuna maajabu yake.

Hauwezi kutembea katika akili ya Mungu alafu ukawa mtu usiye na athari katika ufalme wa giza.

Akili ya Mungu inakupa kuishi katika yale unayopaswa/ ulivyo kusudiwa kuishi,kwa kuwa ndani yake kuna kujitambua na hatimaye kuwa kile Mungu anachokitaka.

Ili umuone Mungu katika maisha yako ni lazima utembee katika akili ya Mungu na sio yako.

Natembeaje katika akili ya Mungu:

i. Ni lazima uwepo katika mazingira ya yeye yuko ili afanye mageuzi ya akili yako na kukupa akili yake.

ii. Ni lazima uonyeshe kuwa unahitaji akili ili uweze kuishi, maisha yako yanaanza pale akili ya Mungu inapoanza kufanya kazi.

Yohana 15:5b…maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.

iii. Ni lazima uipe nafasi ya utendaji kuliko akili yako ili ianze kuimarisha utendaji wake.

Maana unapoipa nafasi ni kuruhusu ifanye kazi hata kama akili yako haielewi kumbuka hapo ndio mchakato wa wewe kuzaliwa kiumbe kipya.

 2 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Unapokuwa na akili ya Mungu hapo sasa unaweza kuwaza, kuongea na kutenda kama Mungu.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

 

Imeandaliwa na:

 

Cothey  Nelson……………………………………………………………………………..0764 018535

Ijumaa, 9 Mei 2025

WEMA UNALIPWA NA MUNGU

 



Moja ya mategemeo makubwa kwa watu wengi ni baada ya kupanda kupata kuvuna!

Kwa maana rahisi wasingeweza kuona umuhimu wa kupanda kama hakuna uhakika wa kupata mavuno.

Kwa kusema hivyo basi mtu asiyepanda akitegemea kuvuna ni sawa sawa na mtu asiye kula akategemea kushiba.

Kama binadamu, wema tunao hufanya kwa watu tunategemea mrejesho mzuri kutoka kwao au watu wakaribu yao.

Laiti tunge jua kuwa wema wowote unaoufanya kwa wanadamu kuwa unalipwa na Mungu tu basi baadhi ya matukio mabaya yangepungua kama sio kuisha kabisa mathalani visasi, magomvi, kuuana na hata magonjwa yange pungua kama sio kupotea kabisa.

Ni sawa na wewe binafsi unaonyesha/ unatoa tabasamu lote kutoka moyoni alafu mwenzako anaonyesha kukudhihaki nini kitaendelea hapo? Utaendelea kutoa tabasamu???.

Wako watu wengi waki wafanyia watu wema alafu wakalipwa mabaya, mara nyingi huishia kwa kusema “ kama ningelijua nisingefanya haya yote “

 

Najua inauma sana katika kuvuna kitu usicho kipanda maana ni kama mtu ulipanda mahindi ukajikuta unavuna pilipili.

Hauhitaji kuweka matumaini kwa watu ( maana hao wanahitaji mahali pa kuweka tuamini kwao ) haijalishi umefanya kitu gani? Muhimu utambue kuwa ulipata fursa ya kutenda wema na ukaitumia vizuri mengine unamuachia Mungu yeye anaeona sirini ambako hakuna mtu awezaye kuona wala kutambua.

Ni vizuri wema wowote unaoufanya kwa mtu ni ishara ya wewe pia kutambua wema alioufanya Mungu kwako hivyo unarudisha shukrani kwa Mungu kwa wewe kuwatendea mema wengine.

Ni seme tu kutenda mema kwa wengine ni kutii sauti ya Mungu au maagizo yake na pia utakapoitii sauti ya Mungu mema yake yataambatana na wewe.

Hauhitaji kufanya mambo ili upate bali ni kama ishara ya kumrudishia Mungu heshima na shukrani kwa yale aliyokufanyia.

Unapaswa kutambua ni neema kubwa ya wewe kupata kibali cha kushiriki kazi yake pamoja na Mungu.

Unahitaji kumjua Mungu kwa namna alivyo na sio kumsikia tu pasipo kumthibitisha katika hali sahihi ya moyo wako.

Unahitaji umwangalie Mungu sana unapofanya wema wowote ili jambo lako lipate kibali kwa Mungu lasivyo utakuwa unafanya hili watu wakuone wewe zaidi ya Mungu.

Hali hii inakuondoa katika uvumilivu wa kutaka kumuona Mungu zaidi ya chochote na kukosa hali ya subira katika kupokea jambo jema kutoka kwake.

 

Ni lazima uwe katika hali ya kumsikia kutoka kwa Mungu ili wewe ufanye jambo na sio wewe kupokea/ kutaka malipo.

 

1 Wathesalonike 5:18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

 

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………………………………………….0764 018535