Moja ya mategemeo makubwa kwa watu wengi ni baada ya kupanda kupata kuvuna!
Kwa maana rahisi wasingeweza kuona umuhimu wa kupanda kama hakuna uhakika wa kupata mavuno.
Kwa kusema hivyo basi mtu asiyepanda akitegemea kuvuna ni sawa sawa na mtu asiye kula akategemea kushiba.
Kama binadamu, wema tunao hufanya kwa watu tunategemea mrejesho mzuri kutoka kwao au watu wakaribu yao.
Laiti tunge jua kuwa wema wowote unaoufanya kwa wanadamu kuwa unalipwa na Mungu tu basi baadhi ya matukio mabaya yangepungua kama sio kuisha kabisa mathalani visasi, magomvi, kuuana na hata magonjwa yange pungua kama sio kupotea kabisa.
Ni sawa na wewe binafsi unaonyesha/ unatoa tabasamu lote kutoka moyoni alafu mwenzako anaonyesha kukudhihaki nini kitaendelea hapo? Utaendelea kutoa tabasamu???.
Wako watu wengi waki wafanyia watu wema alafu wakalipwa mabaya, mara nyingi huishia kwa kusema “ kama ningelijua nisingefanya haya yote “
Najua inauma sana katika kuvuna kitu usicho kipanda maana ni kama mtu ulipanda mahindi ukajikuta unavuna pilipili.
Hauhitaji kuweka matumaini kwa watu ( maana hao wanahitaji mahali pa kuweka tuamini kwao ) haijalishi umefanya kitu gani? Muhimu utambue kuwa ulipata fursa ya kutenda wema na ukaitumia vizuri mengine unamuachia Mungu yeye anaeona sirini ambako hakuna mtu awezaye kuona wala kutambua.
Ni vizuri wema wowote unaoufanya kwa mtu ni ishara ya wewe pia kutambua wema alioufanya Mungu kwako hivyo unarudisha shukrani kwa Mungu kwa wewe kuwatendea mema wengine.
Ni seme tu kutenda mema kwa wengine ni kutii sauti ya Mungu au maagizo yake na pia utakapoitii sauti ya Mungu mema yake yataambatana na wewe.
Hauhitaji kufanya mambo ili upate bali ni kama ishara ya kumrudishia Mungu heshima na shukrani kwa yale aliyokufanyia.
Unapaswa kutambua ni neema kubwa ya wewe kupata kibali cha kushiriki kazi yake pamoja na Mungu.
Unahitaji kumjua Mungu kwa namna alivyo na sio kumsikia tu pasipo kumthibitisha katika hali sahihi ya moyo wako.
Unahitaji umwangalie Mungu sana unapofanya wema wowote ili jambo lako lipate kibali kwa Mungu lasivyo utakuwa unafanya hili watu wakuone wewe zaidi ya Mungu.
Hali hii inakuondoa katika uvumilivu wa kutaka kumuona Mungu zaidi ya chochote na kukosa hali ya subira katika kupokea jambo jema kutoka kwake.
Ni lazima uwe katika hali ya kumsikia kutoka kwa Mungu ili wewe ufanye jambo na sio wewe kupokea/ kutaka malipo.
1 Wathesalonike 5:18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni