USILIE;
Usilie ni neno muhimu sana mtu uhitaji kulisikia
pindi anapokuwa katika majonzi ndani moyo wake na mateso ya jumla katika maisha
yake kwa ujumla.
Watu pindi wanapo umizwa uwa wanalia kwa sababu
mbalimbali moja kati ya sababu hizo ni kuondoa kitu ndani ya moyo wake hivyo
uamini pasipo kulia lile jambo litazidi kumsumbua ndani ya moyo wake mathalani
misiba,kusalitiwa na kutengwa.
Na njia ya kulia imekuwa ikitumika siku hadi siku
katika kuleta pumziko ndani ya moyo wa binadamu, japo sio wote wamekuwa
wakihitumia lakini siku baada ya siku hii njia imezidi kuwa katika nafasi ya
juu.
Hivi sasa mtu akiwa analia sio swala la ajabu kwani
katika jamii watu washazoea kuona watu wanalia ila imebaki kama kielelezo cha
kumtambua mtu mwenye shida.
Ni kweli njia hii kutokana na imani zetu njia hii
imekuwa ikitumika sana japo matokeo yake yamekuwa ni madogo tofauti na lile
lengo lililokusudiwa. watu wamekua wanalia sana wakitegemea yatakwisha lakini
badala yake yamekuwa yakinyamaza mambo ndani ya moyo kwa muda halafu baadae
mambo yakaendelea kuwa magumu.
Hivi sasa imefika kipindi katika jamii yetu usipolia
katika tukio la kulia jamii inaweza kukushangaa kwa kuona kwamba swala hili
alijamgusa kwahiyo ishara ya wewe kukuguswa ni kulia.
Kwanini tusilie wakati
yanayotokea yanaumiza moyo!!!!!!!
Ni kweli kila binadamu anayomachozi ndani yake na
udhihirisho wake utokwa na machozi katika kipindi kigumu na kama yasipotoka
hapo yatoke wapi?
Ni kawaida mtu anapolia kuna mambo mengi yanaendelea
ndani ya moyo wa mtu na akili ya mtu uwa katika hali isiyoelezeka ni ishara ya
kumpenda sana mtu ambae ametengana nae,aliyemsaliti au aliyetoka duniani(kufa).
Wakati mwingi sana mtu ulia sana kwakua pindi
anapofikiri uwepo wa mtu huyo aliyetengana naye yako mambo angeyafanya kwake na
hivyo kutoweka kwake kunaleta pengo ambalo hakuna mtu anaweza kulijaza.
Lile tumaini alilokuwa nalo kwa mtu husika ndicho
kiwango cha maumivu atakayomuachia maumivu ndani ya mtu husika.
I.ulimtambue baada ya
kutambulishwa:
Unaweza kutambulishwa na Mungu au mtu mwingine pia
ata wazazi wako uliwatambua baada ya kutambulishwa.
Mtu yeyote uliyempenda kiasi gani ni pale tu ambapo
ulipotambulishwa na yeye kukuonyesha upendo wake kwako.
Kulia ni jambo la kawaida sana lakini kubwa sana
lazima utambue yuko ambae alikukutanisha nae ambae anaweza kutimiliza hisia
zako na kukufanya kuwa bora kuliko wa leo na siku nyingine.
Bado mambo mengi utafanya hata pasipo yeye kwakua
ata yeye alikuwa ana mambo yake ambayo yanamkabili hivyo sio kila kitu mtaona
mko sawa.
Japo ungependa hata usikie ushauri wake katika mambo
yako ambayo unafurahia kukutana nae mkashirikiana kwa pamoja.
Tambua bado kuna nafasi ambayo yeye aliruhusu
litokee anayo njia nyingine iliyo bora kwako jua nina aliye fanya mkawa pamoja
kama bado yupo jua kuna nafasi iliyo njema sana.
II.itambue nafasi ya
Mungu ndani ya maisha yako
Mtu yeyote yule hakikisha achukui nafasi ya Mungu
ndani yako bali nafasi ya mtu mpe nafasi yake na Mungu anayo nafasi yake ndani
yako.
Lazima uwe na uelewa kuwa ni Mungu pekee ambae
hawezi kukuacha ila wengine wote wanaweza kukuacha katika mazingira ya
kuwapenda au kuwachukia.
Katika yote hakikisha kuwa Mungu anabaki kuwa na
nafasi ya kwanza ndani ya maisha siku zote kwa kua ni yeye pekee ambayo
anayeijua kesho yako na baada ya hiyo kesho(hatima yako).
Lazima utambue kuwa anajua kila kitu kinahusu wewe
hata kama bado ujamwambia na antambua mahitaji yako kuliko vile wewe
unavyofikiria.
Siku zote Mungu ndiye pekee ambaye anawatosheleza
watu wote kwa kadili uweza wake ulivyo na yeye ndiye akulindiye kesho yako, mtu
anaweza kukuahidi lakini asitimize kwa sababu mbalimbali moja wapo ni kifo.
Unapotambua nafasi ya Mungu ndani yako ndipo hapo machozi
yako yanakuwa na matumaini na sio kukata tamaa.
Kilio mara nyingine kinaonyesha hali ya kukosa
mwelekeo lakini pindi utakapo tambua kuwa unaye Mungu ambaye kwa yeye umetoka
na utalejea.
Ayubu 1:22
Unahitaji kumuona Mungu akiwa mwema sana ili usije
ukamkufuru yeye lazima katika hilo bado
Mungu bado mwema sana ila unahuzunika kwa vile ujajua kusudi lake kwa hilo.
Prepared by ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
HAKUNA SWALI GUMU LISILO NA JIBU KWA MUNGU!!!!!!!!!!!!!
Just believe him………
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni