Alhamisi, 12 Septemba 2013

NGUVU YA MUNGU NDANI YA MWAMINI



NGUVU YA MUNGU NDANI YA MWAMINI;

Siku zote mtu ufanya jambo kutokana na nguvu yake kwahiyo mwisho wa nguvu zako ndio mwisho wa utendaji wako.kwakua hauwezi fanya jambo ambalo litakuwa zaidi ya nguvu yako

Hivyo nguvu zako ilivyo ndivyo usalama wako ulivyo na ndivyo utanuzi wako ulivyo kwahiyo nguvu uliyonayo ndiyo inaamua wewe uweje?

Kila mtu anacho kitu kinachomfanya ajivunie wako watu wanajivunia PESA,MALI na hata wengine wanajivunia WATU.

Kwa hiyo kila mtu anachojionea fahari na sio kitu kibaya kwakua kila jambo limebeba furaha ya mtu husika kwa sababu ni mmiliki wake.

Duniani ili uishi vizuri lazima kiwepo kitu ambacho kinacho kupa nguvu ya wewe kuendelea kuwepo la sivyo utaishi hauwezi kuyafurahia maisha ya dunia.

Japo zipo nguvu mbalimbali ambazo wanadamu uzitumia katika kufanikisha mambo yao wapo watu wanatumia nguvu za giza(makabulini,bahari,miti na mizimu) na wengine hali ambayo Mungu amewajalia na wapo ambao wame mweka Mungu katika utendaji wao.

Nguvu ni mahali ambapo maisha yako yameegemea ambayo kwa hapo unapata faraja,amani na mwendelezo mzima wa maisha yako.

Ni kweli kuna nguvu nyingi ambazo kila binadamu wanazo ziamini na kwa hizo wamezielekezea maisha yao LAKINI sio kamwe kama mtu ambaye ndani yake kuna nguvu ya Mungu.

Hii ni nguvu ambayoikiamua kufanya jambo hakuna nguvu yeyote ambayo inaweza kuzuia au kushindwa kutokeza. Hii ni nguvu ambayo ndani yake kunakuwa na MUNGU mkamilifu pasipo kupungua,

Hii nguvu ndiyo kwahiyo dunia ilipata kuwepo,mbingu ikafunguka,kuzimu kukataharuki,wafu wakafufuliwa na mengine hata usiyo waza lakini Mungu anatenda.

Hii nguvu haibahatishi bali inapotumwa lazima ikayatimilize yale yaliyo tumwa kwa ukamilifu wake na hakuna ambalo litashindikana kwake.

Unapo mwamini Mungu lazima uziamini nguvu zake ambazo kwa hizo zina kuwa na nguvu katika utendaji wake.
Namna ya kuwa na nguvu ya Mungu ndani yako;

Hii ni nguvu ambayo haina mashariti katika hali ya kukuganamiza bali katika hali ya kuinua maisha yako kuwa katika hali njema zaidi.

                                                   I.Neno la Mungu ndani yako.

Waebrania 4:12

Nguvu ya Mungu hiko ndani ya neno lake mahali ambapo kuna neno lake basi kuna mamlaka yake,utoshelevu wake.

Kwahiyo ndani yako kama hakuna neno lake usitegemee ukapata hiyo nguvu kwa kuombewa au kwa namna nyingine yoyote. Kwakua nguvu yake inaingia ndani yako kupitia neno lake.

Katika kujenga nguvu ya Mungu kuzidi kutawala ndani yako ni muhimu sana ndani yako pawepo kuwa na hali ya neno la Mungu ndani yako siku zote.

Wakolosai 3:16

Lazima uamue katika kujaza neno la Mungu ndani yako katika hali stahiki kama inavyotakiwa katika ufasaha zaidi ndani yako ili nguvu ya Mungu izidi kuimarika ndani yako pasipo kuchoka ndani yako.

Mathayo 7:24-27

Hakikisha neno la Mungu linazidi ndani yenu kwa ubora na nguvu zake kila siku hakikisha neno la Mungu linakuwa la pekee ndani yako na pia uhakikishe unalipa nafasi katika ukamilisho wake.

Unapoamua kulisoma neno ni kuamua kumsikiliza Mungu hii hatua ya muhimu lakini ni muhimu kutafuta utendaji wa lile ulilolisikia toka kwake.

Pasipo hilo hakuna maana yoyote kwako ya wewe kuwatayari kumsikiliza lakini usiwe tayari  wa kutenda katika yale aliyokuagiza.

Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                  
                     Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com

                                                                                                                                              

BARIKIWA RAFIKI………………

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni