Ijumaa, 17 Oktoba 2014

MSAMAHA NI SIFA YA MKRISTO



MSAMAHA NI SIFA YA MKRISTO;




Japo mkristo anasifa nyingi ambazo biblia inaeleza kama tabia za rohoni, kila sifa aliyonayo mtu ina sababu yake na ina kazi yake. Na utajua umuhimu wa sifa hiyo endapo tu itakapoitajika na ikawa haunacho hicho kitu.japo zipo sifa nyingi na muhimu sana lakini mimi nitaangalia upande wa sifa hii ya MSAMAHA.

Kila sifa ni muhimu sana hasa msamaha ni wazi kuna mahali utashindwa kufikia kwa sababu unakuwa ujakidhi vigezo, hivyo unaweza ukapoteza muda wako na nguvu yako katika maombi na bidii katika kusoma neno la Mungu pasipo kujua msamaha kama moja ya kukupa wepesi kufika kule unakotaka.

Kibinadamu kuna hali ya ubinafsi inayoambatana na kiburi, majivuno na kujihesabia haki na katika hali hii utapenda kisasi kiwafikie wale unaona maadui zako na waabike na wakurudie kwa magoti lakini shida pale vile unavyofikiri isiwe vile ikawa tofauti na vile unavyo tamani. Ni meshuhudia watu wengi wakipata tabu magonjwa mathalani kupooza, vidonda vya tumbo na hata shinikizo la damu.

Ni kweli kusamehe sio jambo ambalo la kawaida ni lazima upate wepesi wa kusamehe na penda kutofautisha vitu viwili hivi mtu kusamehe na mtu kukaa kimya kwa maana katika hali ya ukimya kuna wakati tu italipuka tu na mlipuko wake unaweza ukawa mbaya zaidi. Japo watu wengi usema kusamehe mtu ambaye amekuumiza/amekujeruhi inawezekana kwa kusudia au kutokukusudia shida inakuwa namna gani inakuwa msaada kwangu.

Ni vizuri kutambua usipojenga jenga tabia(mazoezi ya rohoni) katika kusamehe ni wazi unajirudisha nyuma tena katika mtego mkubwa kuwa maisha yako kabla ya wokovu kwamba na wewe unahitajika ufanye jambo ili Mungu apate kukusamehe kwa maana nyingine tunasema unajirudisha katika hali ya kifungoni na inasubiriwa ulipe faini ili uweze kutoka gerezani.

Kukubali kuishi maisha ya kutokusamehe ni kukubali kuishi maisha mbali na Mungu na huku ukitegemea yeye ahusike na maisha yako, sawa na kuvunja ushirika na mtu halafu ukategemea yeye ahusike na maisha yako kwa ukamilifu. Hivyo kukubali kuishi maisha ya kutokusamehe ni kukubali kuishi nje ya utawala wake kwakua yeye ni Mungu anayesamehe na kusahau.

Lazima uchukulie hali yoyote ya kutendewa kinyume na ulivyotegemea ni hali ya wewe kujifunza watu halisi wakoje na sio kuanza kuwachukia kwakua hiyo sio maana ya Mungu ya kuruhusu kukupitisha hapo kwani Mungu analengo la kukuumiza bali anataka matengenezo yake yafanyike ndani yako.

Makwazo yapo ilikuzidi kujisimika na Mungu zaidi na sio kisilani na mtu yeyote Mungu anataka umfanye yeye kuwa ni kila kitu kwako na umuone yeye kuliko chochote  na umweke kuwa tofauti na watu wengine katika utekelezaji wake katika ahadi zake na maamuzi yake.

Msamaha ni ishara ya kumpenda Mungu zaidi ya chochote na ndani ya moyo wako hautaki mtu mwingine au jambo lolote ulipende na likafanye kuwa katika maisha yako kwakua unaweza ukaipenda chuki nayo ikawa sehemu katika maisha ikasababisha Mungu akatoka akaiacha chuki itawale kwakua Mungu achangamani na kila kitu bali Mungu anaheshimu maamuzi yako kwakua yote ameyaweka mikononi mwako uzima na mauti.

Msamaha ni ishara ya kuwa wewe ni mtoto wa Mungu uliyebeba tabia zake kwa ukamilifu wenye ubora uliostahiki, kwakua kigezo cha wewe ni mtoto wa Mungu ni mfanano wa tabia zake na zako na moja wapo Mungu angalii ukubwa wa kosa bali yeye ujua ni kusamehe na kusahau tu na sio linguine na wala kisasi sio mategemeo yake.


Imeandaliwa na ;
                           Cothey Nelson, 0764018535, cotheyn@yahoo.com


PENDO LA MUNGU LITAWALE NDANI YA MAISHA YAKO!

Alhamisi, 2 Oktoba 2014

ZAWADI ILIYOJIFICHA



ZAWADI ILIYOJIFICHA;


Hakuna mtu ambaye apendi kupewa zawadi na mtu anayempenda, kwakua wakati mwingine utumika kama mwendelezo mwema wa mausiano. Lakini inakuwa tatizo pale tu usipoielewa au kutoiona, wakati mwingi haina ya zawadi itakuwa inaashiria mustakabali wa mausiano yenu.

Kwa Yule aliyekupa zawadi kwa dhamiri iliyo njema uona fahari sana kama utaitumia vizuri kwakua ana amini hiyo zawadi itakusaidia kwakua mpaka amekupa anaamini ni njema na inakufaha, tatizo inakuja pale tu ile zawadi usipoijua ni ya kwako na matumizi yake yaliyo sahihi.

Ni jambo la kawaida sana endapo usipoielewa namna ya kuitumia haita fanyika Baraka bali itakuwa ni mzigo badala ya kuwa burudiko ambayo ndio hasa kusudi la zawadi.

Kila mwanadamu ndani yake kapewa zawadi na Mungu ili imsaidie katika maisha yake duniani iwe Baraka kwake na kwa wale watakao mzunguka. Kwakua chochote ambacho Mungu anakupa wewe ni kwa ajili ya kufaidiana ili muishi kama familia moja yenye upendo na mshirikiano wa kweli.

Huwezi ukaitambua zawadi aliyokupa Mungu halafu ukawa namna ambayo Mungu ajaikudia iwe katika maisha yako, lakini wanadamu wengi wanapata tabu sana ni kwa vile hawajajua hadhina iliyo ndani yao na namna ya kuitumia.

Ukiona mtumishi wa Mungu kafanikiwa kihuduma sana katika kuimarisha roho zatu kujenga misingi imara ya kumpenda Mungu isiyotingishwa ujue amitambua zawadi/hadhina ambayo Mungu amempa na kuitendea kazi katika hali stahiki.

Ni wazi kuwa hauwezi kufika tu kwa njia nyingine ila ni kwa kuitambua zawadi ambayo Mungu amekupa na kuifungua na kuanza kuitumia.

Baadhi ya vikwazo vya watu kutoitumia zawadi aliyowapa Mungu!

Ni wazi tu usipotambua wapi umeanguka uwezi kusimama katika hali stahiki isiyotoa taswira ya kuanguka tena. Kujua tatizo ndio hatua ya kwanza ya kuondoka mahali ulipo pasipo kijua basi utakuwa unazunguka hapohapo siku zote pasipo mafanikio ya kutoka mahali ulipo.


i.watu hawajipendi

watu wanapenda wafanane na mtu mwingine na sio watu wao wafanane na yeye japo yote yanawezekana watu wakaitambua nafasi yako na hata kujifunza kupitia wewe.

Watu wamekuwa hawishi maisha yao bali upenda kuishi maisha yaw engine ambao hawajui chimbuko lao wapi limetoka na ustahimilivu wake umejengwa na nini nay eye kufika pale ili mgharimu nini na nani aliyekuwa karibu yake.

Hauwezi ukawe wewe kama tu mfumo wa maisha umebeba ramani ya watu wengine mwelekeo wako umebebwa na maisha ya watu wengi.


ii.mafanikio yasiyo ambatana na usahihi wake
kufanikiwa sio tatizo bali unafanikiwaje na katika misingi hipi ilichimbuko ndani ya moyo wako au ilichumbuko kutoka kwa watu wengine.

Mafanikio haya kulupukiwi bali ni mikakati na maongozi sahih neon lake Mungu. Na katika mafanikio utakiwi uchoke au uone kuwa haustahili kwa mapungufu yeyote yaliyo ndani yako.

Usione kitu kizuri basi ukawaka tama na ndipo ukaanza mikakati ya kupata yale uliyoyaona ka kutumia utundu wa akili tu bali lazima ujue vitu vya muhimu ni vipi! Na nawezaje kuvipata! Na je! Kwa wakati gani ni sahihi wa mimi kuvipata.


Imeandaliwa na ;
                           Cothey Nelson, 0764018535, cotheyn@yahoo.com


NIKUTAKIE KILA LA KHERI NDUGU!!!