Jumanne, 15 Desemba 2015

IRUHUSU JANA IPITE ILI LEO IJE!



ACHA JANA IPITE

Katika maisha ya kila siku ya mwanadamu kuna jana,leo na kesho na katika mfulullizo huu ndipo pazaliwa mwezi, mwaka na hata karne! Na kila siku inayoenda inakuwa na vionjo vyake zipo siku zitaanza na huzuni na baadae zitaenda katika furaha na zipo siku zitaanza na huzuni kuanzia mchana hadi jioni na siku chache sana kwa mwanadamu ambazo zinahesabika kwa mwanadamu kuwa na furaha kuanzia mwanzo wake na hadi mwisho wake.

Ni jambo halisi sana kwa baadhi ya watu katika maamuzi yao ya leo yalitokana na jana yao…mathalani siku moja nilimsikia polisi akisema kipindi sijawa polisi nikiwa mdogo nili nyanyaswa sana na polisi hivyo niliapa kuwa endapo na mimi nikiwa mkubwa lazima niwe polisi na hatimae akawa sawa na na lile kusudi alilowaza katika moyo wake na sio huyo tu bia hata mtu katika kusoma udaktari au sheria kuna mambo walio yapitia katika jana yao na kunuwia kusoma hiyo fani.
Japo ni kweli ni muhimu usome jambo ambalo liko ndani yako ambalo unalolipenda pamoja na hayo pia kuna ushawishi wa kimazingira ambayo yanaweza kusababisha kuingia katika fani hiyo, pia tukubaliane wako watu wengi wanasoma sasa sio kwasababu wanapenda au hiko moyoni ila inawezekana kutokana ndio nafasi iliyopatikana na hata wengine kuona ndio yenye mshahara mkubwa na wengine uweza kuona kuwa ndio fani rahisi katika kupata kazi na kuanza maisha yake binafsi.

Napia kunawakati unaweza ukupenda kuingia sehemu fulani au fani fulani lakini baada ya kuanza kufaidi matunda yake unaweza kusema hivi kwanini sikuwaza jambo hili kama kipaumbele changu cha kwanza kwani sasa nafaidi matunda yake! Inaweza kuwa vizuri ukaanza kuifurahia au kuwa vibaya hata ukaanza kuchukia wakati mwingine yote ni kutokana na matokeo ya hiyo fani katika kazi unayoifanya.

Acha jana ipite maana yake nini?
Ni kwali siku inaweza ikapita lakini wewe bado unaishi katika jana yako japo unahiita leo kutokana kuzama na kuchomoza kwa jua lakini ukweli wewe binafsi bado unaishi jana japo unaonekana leo, yale yote yalioendelea jana katika maisha yako yamekuwa ndio dira ya maisha yako ya sasa kama katika hali ya maumuvu ndio yamekuwa ndo maisha yako ya kujikataa na kuona ndio maisha Mungu alinichagulia ya mimi kuishi.

Mtu kama huyu anayeishi jana katika leo mtizamo wake haubadiliki kile alichojiaminisha ndicho kinachoendelea hadi leo na anakipenda kwakua amekipa nafasi katika maisha yake na kuwa hivyo ndivyo maisha yake.

Kuna watu wakikumbaka jana basi wanalia tu siku nzima inaweza kuwa ilikuwa nzuri kuliko leo mathalani mtu katika maisha yake ya awali alikuwa na kazi yake nzuri na kuishi maisha ya kifahari sana lakini kutokana kuachishwa kazi na ndipo maisha yako yakawa chini hata usijue lakufanya tena bali kilio chako kikawa ndio maisha yake.

Ni vizuri sana kuanza upya hata ukiona itachukua muda gani katika kutimiza malengo yako! Wako wengi wanajihukumu na kujilaumu sana kutokana na yale yaliyosababisha kuwa hapo tena,

Iruhusu jana ipite ili leo ije!
Hizi ni siku mbili tofauti na kamwe hauwezi ukazifananisha na kamwe haziwezi kuingiliana kama leo ipo basi jana ilishapita na kama jana ipo basi leo bado haijaja ziko hivyo hakuna mbadala wake tena hiko kama ilivyo, ndomana wako watu wengi wanatembea leo lakini ukweli hawaoni fahari ya leo zaidi yakujisikia vibaya kwa jana iliyopita.

Usipokuwa makini unaweza ukakuta unamlaumu Mungu muda wa wote kumbe wewe unaishi jana katika leo…………ukapoteza muda na hata kukata tama!

Ni vizuri kutatambua jambo likisha pita limepita hata kama ulikuwa hauamini lakini sasa inabidi uamini tu haijarishi ulikuwa unampenda kiasi gani? Ulikuwa unamwihitaji kiasi gani? Au alikuwa wa muhimu kiasi gani? Au kazi ilikuwa inakunufaisha kiasi gani? Au nyumba ilikuwa inakusitiri na kujivunia kiasi gani?  Lakini jua limeshapita kinachotakiwa hapo ni maisha yaendelee kwakua kwakua kesho itakuja na pindi itakapo fika hautaita kesho bali utaita leo.

Na kila siku kuna baraka zake na hili uzipate unahita uishi kama siku hiyo ilivyo kama ni  jana basi ishi kama jana na kama ni leo ishi kwa siku hiyo ukifuta yaliyopita yaani jana yako, na sio kwa upande wa ubaya tu watu wengine wanajisahau kwakua waliweza jana kufanya jambo fulani basi wanaamini pia hata kesho wataweza pasipo kujua kesho na jana ni vitu tofauti na kamwe haviwezi kulingana, maandalizi ya jana yanaishia jana na maandalizi ya leo yanaishia leo.

lazima uwe mwepesi katika kusoma mabadiliko ili uweze kuimarika na kuwa hodari.

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson……………………………………………0764 018535

Jumanne, 8 Septemba 2015

JANA SIO LEO



JANA SIO LEO


Hakuna leo bila jana na hakuna maana ya jana bila leo!!!!!!!

Jana na leo tunaita utofauti wa siku, kwa maana siku iliyopita tunaita jana na siku iliyopo aua inayoendelea tunaita leo!!

Kwahiyo unaposikia neno jana na leo sio kitu cha kukushtua au kukushangaza kwa maana umekuwa ukisikia na bado unaendelea kusikia na nzuri zaidi wewe mwenyewe umekuwa shuhuda ukiona jana ikibadilika na hatimae ikawa leo……..asante kwa hilo!

Tutakubaliana kwa dhati kabisa kuwa siku inapobadilika inabadilika na mambo yake na unaweza ukagundua sasa au baadae mathalani mtu anapokuwa akikua ni ngumu kutambua sasa mtu ndio ninakua katika kitendo kinachoendelea sasa bali baada ya muda ataona  mabadiliko ndipo unapotambua mtu huyu amekuwa hivyo inakuwa umeweza kuitofautisha jana na leo…..asante sana!

Hakuna kitu kizuri kama kuishi kwingi maana walimwengu wanaamini kuwa kuishi kwingi ni kuona mengi pasipo kujali hayo unayo yaona unakuwa katika nadharia hipi au katika wakati gani, na japo watu wengi wamekuwa wakijivunia katika ongezeko la miaka kutokana na vitu hivi viwili yaani jana na leo ndio maana watu wamekuwa wakifisha miaka fulani basi hapo uweza kufanya sherehe ya kuzaliwa (happy birthday) hasa watu wenye kutambua maana yake na mwenye uwezo huo na hasa mwenye nafasi hiyo.

Unapoangalia katika dunia ya sasa unaweza kushangaza sana watu wengi wanaolia wanasema jana yangu haikuwa hivi inaweza kuwa ilikuwa ni nzuri au mbaya lakini ni muhimu aitaje kuonyesha jana yake ilikuwa vipi ikaazaa leo yake………hivyo kucheka au kulia sio tatizo bali katika kuonyesha kuwa naye alipitia katika mwenendo wa siku.

Ni kweli mambo mengi yaliyofanyika kipindi cha nyuma ni tofauti kabisa na kipindi cha sasa japo watu wengi wanasema kuwa ni maendeleo lakini unaweza kujiuliza ni kweli yanaleta maendeleo hayo yanayosema au ni geresha tu.

Sikatai yako mambo ya jana ambayo leo yanaonekana kuwa hayana nafasi tena na hivyo imeweza kusababisha katika harakati za maendeleo kuongeza mwendo katika kufikia hatua bora zaidi kuliko ya awali mathalani kutokana maendeleo ya sayansi na teknolojia imesaidia kwa kiasi kikubwa  katika kuwasiliana kupitia hiyo watu wamekuwa wakiwasiliana katika njia ya sauti na hata ya video na hivyo kujenga ukaribu zaidi miongoni mwa watu na watu hama jamii na jamii.

Yapo mengi kutokana na maendeleo haya yameibua mausiano ya kujenga na mausiano ya kubomoa lakini yote ni matokeo ya haya maendeleo.

Katika dunia ya sasa kila kitu kimekuwa ni biashara hata vile haviuziki sasa vimekuwa na sokoni na vimekuwa na uwitaji mkubwa wa wateja, watu wamekuwa wakiuza kila kitu kinachoonekana katika macho ya nyama na hata kisichoonekana…………..sikuizi watu awajali nini wanauza bali wanchojali ni kiuza nitapata kiasi gani! Sasa sijajua kuwa hii ni dunia ya kibepari au mmomonyoko wa madili katika dunia ya sasa.

Samahani sana sipati picha dunia ya leo kama kusingekuwa na ukimwi sijui hali ingekuwaje na hasa katika jamii ambayo watu wengi hawana hofu ya Mungu bali wanaenda kanisani.

Katika dunia ya sasa HESHIMA imekuwa bidhaa adimu na sijui kuwa kama watu wenyewe wana jishushia heshima  au wanashushiwa heshima au heshima yenyewe inashuka? Bado sijapata jibu lakini kwa macho yangu naona heshima ikishuka kwa kiwango kikubwa sana sio mtoto wala mkubwa kila mtu anafanya kadiri anavyoona sawa machoni pake na sio kama inavyopaswa kuonekana kuwa sawa machono pa jamii nzima.

Kwa upande wa watumishi wa Mungu mambo mengi yamekuwa tofauti hasa katika zama za manabii wa kina eliya,samweli na wengi walikuwa kweli wana muakilisha Mungu sasa hivi imekuwa ni tofauti…..watumishi wengi wamejiusisha na utapeli waweze kuendesha maisha yao na sio kufanya kazi ya Mungu wengine wamethubutu hata kutumia nguvu za giza katika kutaka watu wawaamini na kuwaogopa.

Sina ugomvi na watumishi wa Mungu mimi na waamini sana na ninawapenda sana hasa wanaojua wajibu wao na kumtumikia Mungu katika kweli tupu na katika udhihirisho wa Mungu mwenyewe!

Sisemi uahache kumwabudu Mungu kutokana na mambo yanayo endelea katika dunia ya leo niseme usalama wako sio kumwamini sana mtumishi wa Mungu bali ni kufahamu kweli ya Mungu ambayo itakutunza na kukulinda na kukupa mwendo mwingine katika Mungu.

Msikilize mtumishi wa Mungu kwani yeye ndiye amewekwa kwaajili yako ili akuongoze katika kweli ya Mungu lakini yeye anasehemu yake lakini wewe unasehemu sana ya kufanya ili uone matunda unayokusudiwa ……………kwani mtumishi wa Mungu anakupa mbegu na maelekezo yake lakini kutafuta shamba, jembe ni wewe mwenyewe na kupanda kwa kufuata maelekezo yake ni muhimu sana! Lakini kumjua Mungu binafsi ni jambo la msingi sana kuliko yote!

Hakikisha moyo wako haujabeba chuki wa kisirani katika yote bali umuone Mungu katika kila jambo naye akupe raha ya kudumu au ya milele…………….mwamini Mungu naye anaweza kukutoa wewe pale ulipo na kukuweka katika hatua nyingine iliyo bora zaidi.

Nibora wakuone uendi na wakati kuliko kwenda na wakati huku unabeba historia mbaya!! Ambayo itakutesa katika kesho yako………………………….!

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………….0764 018535

                           MUNGU AKIKUBARIKI HAKUNA ATAYE KULAANI                          

Jumanne, 1 Septemba 2015

KUMTEGEMEA MUNGU



KUMTEGEMEA MUNGU


 Mathayo 15:8

“ watu hawa uniabudu kwa kinywa tu lakini mioyo yao iko mbali nami”

Hakuna jambao ambalo Mungu analitafuta/mtu anayemtafuta kama mtu ambaye anamtegemea yeye!!

Mshangao Mungu katika dunia ya sasa!

Ni sawa baba aliye na mtoto ambaye rika la mtoto bado linatakiwa liwe chini ya uangalizi wake lakini yeye anataka ajitegemee mwenyewe pasipo kujua au kuwa na upeo wa kujua kuwa maisha ni nini? Bila shaka hilo litakuwa swali kubwa ndani ya moyo wa baba kwa kutaka kujua kinagaubaga kwa nini mwanangu anafikiria aanze kujitegemea wakati bado rika lake linaitaji kuwa chini ya uangalizi wangu.

Nikubaliane kuwa yako mambo mengine yanatokea katika maisha yetu ambayo sio mpango wa Mungu kabisa lakini tumekuwa tukijifariji tu……..lakini ukweli tumekuwa tukitegemea kitu ambacho akipo au hatukijui vizuri hama ambacho hatuna uhakika sana na mwisho tumekuwa katika mazingira tofauti na ndoto zetu.

Kumtegemea Mungu sio jambo lelemama ukiwa hapa duniani kwani dunia inahitaji uitegemee yenyewe ili ikupe kile inachofikiri kukupa……..nguvu ya dunia imekuwa ikiwavuta wengi  na kusahau kwamba imetupasa kumtegemea Mungu kwa asilimia zote hivi sasa wako watu wanawategemea wachungaji wao, marafiki na mtu ambaye anaamini kuwa atanisaidia lakini uwezi ukalinganisha mtu anayemtegemea Mungu na mwingine asiye mtegemea bali anategemea vitu vingine.

Nyimbo nyingi zime imbwa na kupendwa na watu wengi  katika ujumbe wa kuonyesha faida ya kumtegemea Mungu lakini ukweli baada ya kuimba na kucheza na hatimae kutoka jasho tukaacha hapohapo kwa kujua kuwa kumtegemea Mungu ni nyimbo na wala sio maisha ( nyimbo kugusa hisia zako sio kumtegemea Mungu).

Ukweli katika dunia ya sasa wako watu ambao kwa muonekano na  wingi wa maneno yao unaweza kuona au kuamasika na hata kushawishika kuwa watu hawa wana mtegemea Mungu lakini ukweli muonekano wa mtu na namna mtu anavyojieleza sio dalili au ishara nzuri ya kuonyesha kuwa huyu anamtegemea  Mungu na huyu amtegemei Mungu.

Ujumbe huu hauko katika kuwapima watu na kutambua nani anamtegemea Mungu na nani amtegemei Mungu, bali ni kuonyesha maisha ya sasa yalivyoenda mbali na kumtegemea Mungu hivyo na kukuhatarisha kuwa makini sana katika dunia ya leo hivyo kutambua kwa uhalisi au kwa uhakika namna ya kumtegemea Mungu.

Ukweli kumtegemea Mungu kupo na kunawezekana na kunatenda kazi ni wewe kuamua sasa na anza kumtegemea Mungu kwani hapo ndipo kunazaliwa mkristo ambaye kwa uhakika Mungu ndiye anayemtaka na anamtafuta ili amfanyie ibada ambayo anajua kwa uhakika itampendeza yeye na kuimarisha mausiano yao.

Niseme tu hakuna maisha ya ushindi kwa uhakika mbali na kumtegemea Mungu na kwa namna hiyo ukristo unakuwa wa maana na tishio kubwa katika upande wa giza kwa wewe kuishi maisha ya kumtegemea Mungu.

Lazima ujue uwezi kuondoka katika maisha ya utumwa kwa kuombewa tu au kutabiriwa tu japo mambo yote sio mabaya lakini jibu la uhakika ni kuishi maisha ya kumtegemea Mungu kuliko na udhibitisho wake na sio mtu mwingine.

Kumtegemea Mungu ni kuishi na Mungu kwa namna anavyokukuelekeza au maisha yasiyo na uhai wa akili ya kibinadamu,maisha yaliyo jaa kiu ya kutembea na hatua za Mungu. Haya ni maisha ambayo hayafuati watu waliishije bali mimi ninatakiwa niishije!

Yoshua 1:1-9

Kumtegemea Mungu tunaona yoshua wakati anaachiwa kijiti na Musa…… kipindi cha Musa alipewa fimbo na wingu lilikuwalikimuongoza katika safari yake na Israeli lakini yoshua alipewa neno la Mungu liwe dira yake katika utendaji wake na katika muongozo wake. Yoshua alikuwa na mwendo mwingine na Mungu katika kuyafikia malengo ya Mungu aliyaweka katika maisha yake….!

Uwezi ukamtegemea katika hali ya kubahatisha lazima pawepo na muongozo wa uhakika ukikuongoza kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine inabidi iwe ni ya uhakika na muongozo ulio salama usio sitasita………………..!

Kama kweli unataka kuondokana na changamoto zinazokukabili basi tafuta kwa bidii namna sahihi ya kumtegemea Mungu! Maana hapo ndipo palipo na tulizo lako na furaha ya kudumu.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………0764 018535

Jumanne, 25 Agosti 2015

UPANDE ULIO BEBA USALAMA WAKO



UPANDE ULIO BEBA USALAMA WAKO



Moja ya vitu vinavyopendwa na watu wengi ni usalama!

Kwakua katika usalama kuna utendaji katika uhuru na nafasi ya kufanya jambo lenye ubora wake.tuna fahamu kuwa moja ya kazi ya vyombo vya ulinzi ni kulinda mipaka ya nchi ( kuhakikisha usalama wa nchi wakati wote)

Na hichi ndicho kitu ambacho watu wengi ukitamani sana…..usalama wao pamoja na mali zao, kwakua wanajua katika usalama basi mambo mengi uwa rahisi kufanyika pasipo na ugumu usiokuwa na lazima.

Shida kubwa moja ya watu wengi wanapenda sana kuwa na usalama lakini namna wanavyoenenda wanaufukuzia mbali usalama wao na vitu vyao……….sawasawa mtu anayetumia dawa(dozi) katika hali mbaya lakini bado mtu anatumia kilevi kikali lakini katika hali hiyo bado anaamini Mungu atamsaidia.

Niseme wazi siku inapande mbili yaani usiku na mchana……..na hata dunia inapande mbili yaani uliosalama na usio salama, na hakuna ambaye apendi usalama lakini ugumu uko katika  kudhihirisha kuwa wewe unapenda usalama katika maneno tu au pia katika mfumo mzima wa maisha yako.

Kibinadamu yako mambo mengine mtu anafanya akiwa ametiwa giza akiamini anaona kumbe haoni sawasawa na mtu kuamini anajua kumbe ajui! Ndani ya dunia kuna mtindo ukiishi ambao utaondoa usalama wa maisha yako na kusababisha mambo mengine yazidi kukukabili.

Unahitaji kujua kwamba binadamu wewe ni sahihi kwamba uhuru ulionao unapaswa usifanane na wanyama katika utendaji wako na katika kutimiza hisia zako inakupasa ujue kuwa viumbe vyote vya dunia vinapaswa vijifunze kupitia wewe na sio wewe ujifunze kwao unaweza kukataa kabisa lakini ukweli ni kwamba mambo mengi tunayoyafanya yanafanana na wanyama kwa asilimia kubwa mathalani kupigana hadharani na matendo mengine yanayofanana na hayo.

Kuna maisha ya mengine mtu anaishi unaona mwisho wake wa maisha yake umebebwa na maumivu, kukataliwa na hata kutengwa lakini bado mtu anakuwa anakaza mwendo kuendelea, na ukiwasikiliza wanasababu nyingi wengi wakisema maisha magumu, nilikataliwa na wengine wanasema nimetendwa vibaya hivyo staili ya maisha haya ndio niliyoichagua hivyo na ishi maisha haya sio kama napenda bali inanilazimu.

Niseme kwamba kwa namana yoyote ulivyo, jua yuko mmoja tu ambaye atakupenda vile ulivyo na kutopenda aibu yako iendelee kwakua kwa yeye ulitoka na kwake utarejea, hivyo niseme wazi katika maisha yoyote unayoishi bado Mungu aliyenipenda mimi basi anakupenda nawe tena upendo uleule hakika ni baba mwema.

Niseme maadamu unaishi tu haijarishi uko katika hali gani nini kimeathiri mwili wako, akili yako na kuona kuwa umeharibu mstakabali wa maisha yako napenda ujue kuwa bado unayo nafasi kubwa kwa Mungu aliyekuumba anaweza akainawilisha tena ngozi yako na kuwa zaidi ya ulivyokuwa jana! Huna haja ya kulia na kusononeka sana bali yuko Mungu ambaye kwake yeye kila kitu kina nawilishwa na kuzidi kwa bora.

Mungu anasubiri maamuzi yako tu katika kurejea kwake naye akufanye kuwa mtu wa maana katika viwango vyake. Mungu awezi kukurahumu wala kukuchoka bali anajua kuwa kwa wewe unaweza kuwa mtu mwingine kupitia yeye.

Hivyo Mungu anasubiri umpatie maumivu yako,teso lako na dhihaka yako ili yeye achukue na kukuacha ukiwa huru mbali na mateso…………maana salama yako ndio furaha yake.

Giza katika dunia japo ni sehemu ambayo watu wengi upenda kufanya mambo yao kwasababu kuna maficho yao lakini hawapendi kujua kuwa ndani ya giza kuna upofu uharibifu na mateso yaliyobebwa na huzuni isiyokoma.

Nuru ya Mungu katika dunia hii……… hapo ni sehemu salama japo watu wengi hawapendi kwenda katika njia hiyo kwani haina mvuto lakini niseme kwamba katika nuru kuna nguvu na uimara uliobeba stara ya mwanadamu.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………0764 018535