Jumatatu, 20 Julai 2015

HARD DECISION IS MY LIFE



MAAMUZI MAGUMU NI MAISHA YANGU


Maamuzi magumu kwa maana nyepesi ni uchaguzi wa kujigharim!

Uwa hakuna furaha katika maamuzi magumu katika kila hatua ya awali ya mwanadamu anayoipiga ila matokeo yake yanaweza yakazalisha furaha, naamini kila binadamu anatawaliwa na maamuzi katika utendaji wake ya sasa na hata ya baadae yanabebwa na maamuzi.

Kwa sababu unaishi basi swala la maamuzi uwezi kuliepuka, yapo Maamuzi tunayo yafanya kila siku tunayaita kuwa haya ni maamuzi ya kawaida ambayo baadhi unajigharim kidogo na hata mengine haujigharim kabisa………kwa maana yako mengine unakuwa na wasiwasi sana na mengine unakuwa huna wasiwasi kabisa.

Tuna amini katika maamuzi magumu tunaweza kufanya jambo kuwa kubwa tena kwa wepesi zaidi katika muonekane wake, ni jambo la kawaida sana kwa wale walifanya mambo ambayo yamekuwa msaada sana katika maisha yetu mathalani waliotengeneza ndege,meli na mengine mengi sio ajabu wengine walitumia muda wao mkubwa katika shughuli hizo kuliko hata na familia zao,ndugu zao na pia hata marafiki zaohatimae wakafanikisha ile ndoto yao.

Niseme kuwa katika maamuzi haya magumu hapa ndipo tunaweza kufanya mambo katika mafanikio makubwa japo wako watu wanafanya maamuzi madogo huku wakitegemea kupata mafanikio makubwa…..sio kila jambo rahisi kama hivyo bali tambua kuwa kazi kubwa katika maamuzi yako ndio yanaleta matokeo makubwa.hivyo utakiwi kuogopa sana katika maamuzi magumu hasa yakiwana tija katika maisha yako na mbele za Mungu.

Ukweli hatua yako ya mbele inategemea sana maamuzi yako kwani maamuzi yenye kujigharim kidogo basi hiyo ni hatua ndogo lakini maamuzi yenye kujigharim sana basi hiyo ni hatua kubwa katika maisha yako.

Katika maisha tuliyonayo uwa hatuwezi kufika katika maamuzi yasiyo na kina mathalani serikali yetu na mambo mengine yafananayo na hilo mengi sana yamekubwa na mfumo ambao kwa kiasi kikubwa hauja beba haki au usawa bali katika kila jambo jambo walitendao limejaa udhalimu na ubadhilifu wa mali ya umma katika hili ni seme tu wazi tunahitaji mapinduzi magumu yanayobebwa na dhamira ya dhati katika kuleta mabadiliko chanya.

Tukianza na maisha binafsi hatuna budi kuhakikisha kuwa maamuzi sahihi yaliyojaa kujigharim ndio chachu nzuri ya maendeleo mathalani wako watu wanaanza na pa dogo lakini mwisho wao wanategemea kufika mbali sana lakini kama ukiangalia mwanzo wao unaweza usione mwisho wenye maana sana.

Lakini watu wengi wanaogopa kuingia katika maamuzi magumu kwani wanaona kama wataonekana wanaanza moja, na hivyo wataonekana kama wajinga hawajui wanachofanya na kuona kwamba hawata kaa wafike japo haya ni mawazo au ni maneno ya kawaida sana lakini yanaweza yakabadilisha  mfumo wa maamuzi wako badala ya kwenda kulia ukaanza kwenda kushoto.

Hivyo imekuwa ngumu sana kwa watu katika kuamua maamuzi magumu na wengi wamekuwa wakiendeleza hata kwa yale wanaona wanaelekea sio salama lakini wamekuwa wakijikaza kisabuni maadamu siku zinaenda na maisha yanadumu basi wanavumilia wakiamaini ipo siku mambo yatabadilika.

Asikudanganye mtu uwa mambo mengi hayajibadilishi bali yanabadilishwa na mtu husika au mfumo husika hivyo kusubiri maji yabadilike ni sawa kusubiri maji ya bahari chumvi ya badilike  alafu maji yawe kama ya mto…………unaweza ukasubiri sana! Lakini matokeo yake yameshatokea na kamwe haya wezi kubadika.

Unaaja kumcheka kinyonga kwa sababu ya mwendo wake bali angalia wewe unapo lala yeye anakuwa wapi lengo lake ni muhimu sana kuliko chochote uwa anajiangalia mwenyewe na kujikubali yeye kama yeye na hatimae anatimiza malengo yake.


Hakuna anayeweza kubadilisha maisha yako ila ni wewe mwenyewe!

Imeandaliwa na;

Cothey nelson…………………………………..0764 018535

Jumanne, 7 Julai 2015

USTAWI ULIOBEBWA NA UTII



USTAWI WA KIMUNGU


Kutoka 19:5
Hakuna kitu hatari sana kama UTII kwakua ndani ya utii mtu uweza kufungua hazina yake ambayo aliiweka kwa muda mwingi……. akitafuta mtu ambaye atamwamini na kuachia mambo yote ndani yake.

Mshikamano, ushirikiano, kuimarika katika yote unabebwa na utii na ni utii pekee ndio wenye kuashiria kuwa wewe una nafasi gani kwa mtu yaani nama unavyo mtii ndiyo ishara kuwa kwake kuwa unamthamini kwa kiasi gani?

Unapaswa kujua kuwa yote unaweza kumfanyia mtu hata Mungu akaweza kukupa neema yake lakini sio kutokutii…….ni ishara kubwa sana kuwa hauko na yeye na uko mbali nae! Tunajua tatizo la watu sio kutokutii tu bali ni namna ya kutii na mambo ya kutii watu wengi wanatii katika baadhi ya mambo tu hivyo kupelekea kushindwa kuonyesha utii uliobeba moyo wote.

Niseme kuwa pasipo utii hakuna mwendo ulio wa maana wa wewe na Mungu, hata na mtu yeyote kwakua ndicho kiunganishi kikubwa katika kufanya mambo ya weze kuwa katika hali yake stahili…kwa hiyo kama hakuna utii hakuna kwenda!

Japokuwa watu wengi wanatamani sana kumtii Mungu ili wafike peponi wakiwa wana maana waweze kuwepo mahali ambapo yeye yuko yaani mahali salama mbali na jehanamu, unahitaji kujua kuwa katika mwendo huo ni vigumu sana katika mwendo wako wa kumtii Mungu katika hali ya kupenda na sio msingi utakao kuweka imara!

Kumtii Mungu hiyo ni ishara ya pekee kuwa wewe ni wake, kwani kile unacho kipenda kweli ni wazi hauwezi kukitii kinafiki kwakua kwakua unakipenda au unampenda Mungu anataka umtii kwakua unampenda na unamthamini na kuona yeye ni wa pekee katika maisha yako, kwakua Mungu anataka nafasi ya kutosha ndani ya maisha yako.

Ni seme tu hakuna maana ya kujipaka au kujiweka utakatifu kama hauna utii wa kweli mbele za Mungu, hakuna jambo litakuwa na kibali kwa Mungu endapo tu hutajua thamani ya utii mbele za Mungu.

Udhihirisho wa utii!!!

i.kifo cha matumani ya mwili
kama ibrahimu ilibidi mwili ufe ili aweze kumpata isaka na sio ishamaeli, siku zote mtu yote ana mtii Mungu uwa anapoteza matumaini ya mwili wake kuwa hapo ndipo mtu anakuwa awazi nitavaa nini? 

Nitakula nini? Nitalala wapi? Haya ni maamuzi yanafichwa na mtu ambaye aliye mbeba Mungu kweli kweli na anaye weza kufanya mambo ambayo kwa hakika watu wengi wanaomtazama hawataona maana ya yeye kufanya hivyo.

Hapa mtu anaweza Mungu tu katika staa ya maisha yake hana jambo jingine na wala haiogopi kesho bali kesho inamuogopa yeye.

Ni mtu ambaye anakwenda kinyume na mfumo ulioko katika hali ya dunia bali yeye amebebwa na uweza wa Kimungu unaompa kuona katika hali ya kimbingu na kusimama mahali pasipo simamika kwa mtu mwenye akili timamu.

ii.mateso ya akili

uwa hakuna akili itazalisha jibu katika mazingira ya mtu anayemtii Mungu alikubali kwenda na mbingu, hakika kila siku mazingira hayafanyiki tu bali katika uwepo wake hapo ndipo kunazaliwa vitu vitu vyote vinavyotakiwa kuwepo.

Wakolosai 3:10
mtu huyu hauwezi kukaa nae ukapata/ukauelewa ufahamu wake kwakua ufahamu wake umefichwa ndani ya kristo na kinachoonekana na kristo mwenyewe katika kuyafanya mambo ambayo hayawezekanai kabisa.
Nikweli hauwezi kumpendeza Mungu katika mazingira ya kuonekana ya kawaida ya kila siku na mtazamo wa akili ya kawaida………unahitai kuwa na akili nyingine!

AKILI INAYOANZISHA SIO AKILI INAYOFUATA!!!

Imeandaliwa na;
Cothey Nelson………………………………0764 018535