Jumanne, 19 Aprili 2016

NGUVU YA HAZINA



NGUVU YA HAZINA

Unaweza kuona mtu upenda kuchelewa katika mambo mbalimbali, unaweza usijue kwanini mtu anachelewa? mathalani Ukiona mtu ananunua bidhaa alafu anasema chenji ibaki ukouko hakuna shida,ukabaki na maswali kichwani?  Au Unaweza kuona mtu anaangusha kinywaji alafu anakiacha na kwenda kuchukua kingine, unaweza kuwa na maswali mengi pamoja na majibu yako binafsi unaweza kuona mtu huyu ajaona alichododosha au aibu hama anajiona?

Sikatai Ana B yanaweza kuwa majibu lakini kuna uwezekani kuwa NGUVU YA HAZINA, kwa kiasi kikubwa inawezakana kuwa siyo yeye bali NGUVU YA HAZINA inampa ujasiri wa kufanya kile anachokifanya pasipo kuogopa huku akiamini kuwa kile anachofanya ndicho anachotakiwa kukifanya na sio kingine ambacho wengine wanaona kuwa ni sahihi.

Unaweza kuona mtu anasumbua mtaa, anachosha watu, anaboa watu analeta maswali katika kichwani mwa watu lakini kubwa kumbe inaweza kuwa ni nguvu ya hazina inayomsukuma kufanya kile anachokifanya na kuona ni sawa watu kumuongelea kwakua yeye anazo fedha na wengine hawana(maskini) hivyo wacha wamuongelee yeye azidi kupeta, kwa kawaida mtu wa namna hii upenda sana kupigiwa magoti na kumuona kuwa yeye anastahili sana kuliko asiye hadhi yake!

Ukitaka kupata shida kutana na mtu mwenye hazina yenye nguvu alafu hazina inamwendesha au inamtaalakisha au inamsukuma kufanya mambo………….unaweza ona ni bora ukutane na simba akakutafuna basi historia ya maisha yako ikaishia hapo kuliko kuishi na mtu wa namna hii inakuwa ni zaidi ya mateso.

►Asante karibu………………………….!!!

Tunafahamu kuwa hazina ikiwa njema bila shaka maisha yanakuwa njema! Na furaha itokanayo na utoshelevu utazani kumbikumbi wakati wa mvua basi bila shaka inaweza kuchomoza furaha inayoambata na uwepo wa fedha.

Bila shaka namna unavyoishi kwa kiasi kikubwa uweza kuamliwa na hazina uliyonayo ukiona mtu huyu anapanda katika gari lake na huyu anapanda daladala hapo kunatokana na utofauti wa uchumi kati ya mtu husika na kwa kiasi kikubwa kinachoamliwa hapo sio kupenda bali hazina ya mtu.
HAZINA ni usalama wa mtu katika kumudu mahitaji yake, hivyo ukubwa wa hazina ndio ukubwa wa kuimarika kwake. Na bila shaka kila mtu upenda kuona hazina ikiongezeka na sio ikipungua.

Upaswi kupatashida kuumia kuwa matumizi yamekuwa mengi bali ni vizuri kutambua kuwa shida yote unayopata kwa kiasi kubwa ni kutokana na hazina kutotosheleza mahitaji husika. Hivyo ni vizuri usipange safari ya kutoka kawe kwenda gongo la mboto (700) wakati nauli yako ni kutoka kawe kwenda kariakoo tu (400).

Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

Mathayo 7:25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.

Nazungumzia hazina ambayo ambayo haijawaitokea ikakupoteza au kukuacha bali hii hazina inaweza kukupa fedha, uzima, nguvu na maarifa na yote ambayo dunia haiwezi kukupa kwakua yenyewe imebeba ukamilisho.

Hii hazina ndio asili na ustawi wa hazina zote maana inakuwa imeshikwa na Mungu mwenyewe na hakuna hawezaye kuharibu.

Mathayo 6:20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………0764 018535

Jumanne, 5 Aprili 2016

NGUVU YA JICHO



UNAONA NINI?


Moja ya milango mitano ya fahamu ambayo mwanadamu  uitumia katika shughuli za kila siku ni JICHO(MACHO) ambayo kazi yake kubwa ni kuona japo inakazi nyingine kama njia mojawapo ya mwili katika kutoa taka mwili na kazi  nyingine nyingi!

Katika maisha ya mwanadmu utendaji wake mkubwa umebebwa na KUONA jambo au tukio unaweza kukuta huyu ameacha mwenzi wake, hawaongei tena, hawashirikiani tena, na hata kuwa hawapendani tena inaweza kuwa ni matokeo baada ya mtu kuona kitu  akikifanya mwenzake  na hatimae mwingine akaamua kuchukua maamuzi ya kuwa mbali naye!

Kuona jambo au tukio huu ni ushahidi ambao unapewa nafasi kubwa katika himaya ya mahakama, pindi unaposema ushahidi wangu ninao utoa ni ushahidi unaotokana na kuona mwenyewe na sio kusimuliwa na mtu basi bila shaka huo ushahidi unakuwa na uzito wa kipekee kuliko ushahidi wa kusikia.

Katika uwanja mzima wa KUONA kuna kuona  kwa macho kunakohusishwa na ufahamu wa mtu na uko ndiko jikoni kwa mtu katika kuchukua maamuzi ya haraka au ya muda, bila shaka ufahamu wako ndio unaoamua utendaji wako mara baada ya kuona japo kuna wakati hisia uweza kuchukua nafasi na hatimae watu wakashangaa hata wewe umeamua jambo hilikwakua sio kawaida yako.

Ni wazi kabisa vile unavyo ona ndivyo unaweza kujiamini na kuchukua hatua katika jambo husika, wako watu wamekuwa wakiamua jambo baada ya kuona kitu fulani kikitendeka au kutokana namna anavyoamini, alivyoona kwa wengine alivyoshaurika au shawishika binafsi.

Yako mambo mengi yanawatokea watu ni kutokana na vile wanavyoona na hatimae kuamini mathalani mtu anaweza kuingia ulingoni katika mashindano ngumi baada ya kumuona mpinzani wake anaweza kuona kuona kuwa nafasi ya kushindwa hipo kubwa kuliko ya kushinda……..na baadhi yao wanaweza kuathirika na kumbukumbu ya mpinzani wake kuwa katika mapambano yake hajawai kushindwa au kashindwa pambano moja na kama alishawai kushindwa basi aliyemshinda ameshakufa hivyo huna hata wakupata mbinu zitakazo kukuwezesha katika kupigana na mtu huyo.

Wako wengine wanapoitwa kwenye usaili wanapoingia mahali pa usaili anaweza kujiona hapo yeye astahili hivyo hata ujasiri wa kujibu maswali wote unapotea kama sio kuisha kabisa na uwezekano uweza kuwa mkubwa wa yeye kukosa kazi kuliko kupata kazi, sio hilo tu bali wako hata wanafunzi wanapojiandaa na mitihani uwa uweza kuona mimi hapa katika somo hili mimi siwezi kupita hivyo hata maandalizi yake yanakuwa sio yaliyo ubeba umakini na bidii sana kwani uamini hapa kushindwa ni haki yangu.

Mbali hilo kuna jambo ambalo ni la hatari sana hasa kwa wagonjwa wengi katika nguvu ya kuona uwa kinacho wa maliza ugonjwa sio ugonjwa bali ni namna wanavyouelewa huo ugonjwa na hatimae KUONA kuwa huu ni ugonjwa hatari sana hivyo wakati wowote kuna mahali pana nihita tu iwe isiwe.

Hakuna kitu kibaya kama kuona vibaya kwani uwezi kufika salama kama unaona jambo katika mtazamo tofauti na vile ulivyopaswa kuona  mathalani mtu anaweza kumwitaji mwenzi wa maisha anaweza kuwa na maswali mengi hivi mimi nitaweza kweli? Hivi anaingilika? Akinikataa itakuwaje? Hivi huyu simcharuko kweli? Hivi atanipenda kweli mimi? Hivi ndugu zake watanikubali kweli? Mtu huyu uweza kushtukia yule anayempenda kaolewa au kaoa pasipo kupata jibu sahihi katika akili zake.

Niseme kunanguvu kubwa katika KUONA vyema kwa katika kuona vyema unaweza kubadili hali isio faa ika faa inategemea na mtazamo wako kwa kiasi kikubwa: 

Mtazame ezekieli,
Ezekieli 37:3 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe.

 Muhimu kutambua Mungu yuko kwa ajili ya kukung’arisha na wala sio kukuabisha hakuna zito atakalo liruhusu litakalo kukushinda wewe kwa maana aibu yako itakuwa aibu yake kama ukiwa wake!
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………0764 018535