HAUHITAJI KUMLAUMU
unaweza kuwa binadamu wa ajabu sana hasa katika Dunia ya sasa,
pindi utakapo dhulumiwa au kukosewa hama kusababishiwa kukosa jambo fulani
ambalo unaweza ukahisi kama ungelifanikiwa pale basi ungelikuwa mbali au
usingelikuwa pale ulipo sasa hama wengine kusalitiwa na kujikuta kuishi maisha
ya lawama.
Kulaumu kwa kiasi kikubwa yamekuwa ni maisha ya watu wengi kwa
ujumla wao waliofanikiwa hata wasiofanikiwa, katika ulimwengu wa sasa ni watu
wachache sana utakao kutana nao ambao wasiweze kumlaumu mtu na mbaya zaidi wako
watu wameenda mbali zaidi wanawaza kumlaumu hata MUNGU.
Wako watu wanamlaumu Mungu wakisema ni bora nisingelizaliwa
kuliko kupata aibu hii kutoka kwa mtu huyu au kwa watu hawa kwani kule
ningekuwa salama ninge kuwa na wewe(Mungu) na mimi tu maisha yangeenda sawa
kwakua najua kamwe nisinge kuumiza kwa maana yote ungenitendea ni mema tu hivyo
moyo wangu unge furahi siku zote kuliko kuwepo katika dunia hii iliyo jaa
machafuko ya kila namna yasiyochafua moyo tu bali hata ngozi kudhoofika/kukunjamana.
Kikawaida neno hili kulaumu limekuwa kama haki ya mtu
aliyekosewa hama kuonewa na pindi ukianza kumlaumu mtu aliye kuumiza watu
hawawezi kukuona kuwa umekuwa MJINGA bali zaidi sana watakuonea huruma na
kukupa moyo wakisema leo imepita ujui kesho Mungu amekuandalia fungu gani
katika maisha yako hivyo uwe na moyo wa subira.
Pasipo kuficha uwa naona kuna mateso makali na maumivu makali
sana pindi mtu anapoingia katika maisha ya lawama, kwani kiu ya maji inaweza
kutoweka ghafla, njaa ikakimbia pasipo kujua imeelekea wapi? maana unaweza
kuitafuta pasipo kujua hivi kwanini imetoweka mbona sijaiambia iende, pasipo
kujua hayo ni matokeo ya lawama kuota mizizi katika moyo wako.
Na hakika naweza kusema kuwa hakuna kitu cha maana sana kama
kuishi pasipo kuweka misingi ya lawama, kwani yanafanya maisha yako kuwa rafiki
wa furaha,amani na upendo hivyo yanapelekea kuwa ni rahisi kutimiza lengo
katika maisha kwakua bidii na ufanisi kutokana na utulivu wa akili katika
utendaji upelekea urahisi wa kutimiza lengo lako katika njia iliyo salama.
Najua swali kubwa ni
kwanini nisimlaumu wakati yeye amechangia kuharibu maisha yangu?
Ni swali nzuri na kwa mtu mzima yeyote lazima ajiulize swali
kama hili? Lakini nami naweza kukuuliza hivi ukisha mlaumu nini unafaidika
katika maisha yako kitakacho kupa hatua bora katika maisha yako ya rohoni au ya
mwilini.
Unaweza kusema nitaishi maisha ya kumlaumu ili niirizishe
nafsi yangu je! ni kweli ndio njia sahihi ya kuirizisha nafsi yako?
Nikubaliane jambo lolote ambalo aliupendezi moyo wako basi ni
wazi litaumiza moyo wako na hatimae kukupa sababu ya kumchukia au ya kumlaumu
kwa kitendo alichokufanyia.
Yesu alipokuwa anapigwa mijeledi na kuteswa mpaka kufa
nafikiri huyu alikuwa na sababu ya kuwalaumu watu tangu alipo mkamata hata wakamjeruhi
mwili kwa mijeledi iliyo lalua mwili wake na kufanya kuwa kitu kisicho
thaminika, kumbuka yesu alikuja kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu lakini hao hao
wanadamu walimjeruhi na kuhakikisha mpaka anakufa,
Lakini katika yote …………. Yesu
akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake,
wakipiga kura.( Luka 23:34).
Ni kweli kuiga kitu kinachofanywa na watu wengine ni jambo
baya lakini sio kila kitu cha kuigwa ni sawa kwako hata kama stori zenu
zinafanana kwa kiasi gani kila mtu kuna mahali alipotokea anachimbuko lake na
anauelewa wake hivyo anautatuzi wake.
Niseme kuwa hakuna kitu kizuri kama uhuru wa ndani kwani
uhuru ndio matunda mazuri yanayoonekana nje yanayooshesha kushamiri na kunawiri
kwa nje! Niseme uhuru wa ndani unatuzwa na mtu husika kwani kama furaha
anaipata mtu binafsi na maumivu anayapata binafsi hivyo sio kila watu wanavyo
fanya ndio usahihi wa kufanya zaidi ya kutenda katika kuhakikisha uhuru wa
ndani unakuwa ni maisha yako.
IPENDE HATIMA YAKO KWA KUUTUNZA MOYO
WAKO NA UTUNZE MOYO KWA KUMPENDA MUNGU WAKO BINAFSI!
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni