ULIYE KARIBU NAE
Ni kawaida tu, ili kitu kiwe karibu na wewe, kuna uwezakano
wa kuwa ni kitu kinachokuzunguka au wakati mwingine kinaweza kuwa ni kitu
unachokiona kila siku pindi unapotembea au kukaa na hata unapofanya shughuli
zako.
Ni kweli kabisa kuna mtu aliye karibu na wewe kwa maana
anahusika na moyo wako na mwingine ujamusisha katika moyo wako ndomana jambo
moja linaweza kuwa kuta wote lakini mwitikio wako utakuwa tofauti kwakua utategemea nafasi yao kwako.
Kwakua unaishi katika dunia ambayo ina vitu vingi mathalani
miti, mabonde, milima, mito na maziwa yenye kupendezesha muonekano wa dunia na
wenye tija katika maisha ya mwanadamu kwakua mwanadamu utumia maji na miti
katika shughuli mbalimbali ili maisha yaende.
Japo binadamu tumezungukwa na vitu vingi vilivyopo dunia na
vyeme mchango mzuri katika maisha yetu, lakini athari/matokeo yake haiwezi
kuonekana mathalani katika kubadilisha tabia za mwanadamu kama alikuwa na asila
basi awe na upendo na kinyume chake ni sawa!
Kwa kiasi kikubwa binadamu amezungukwa na wanadamu wenzake
kwakua maisha yake yako mbali na wanyama pori wanapoishi japo wako watu
wachache wanaishi misituni na kuzungukwa kwa kiasi kikubwa na miti, wanyama na
milima na mabonde,
Japokuwa viko vitu ambavyo mwanadamu amezungukwa navyo lakini
kitu pekee kinachoweza kuinua moyo, furaha, kusonga mbele, kuamasika, kupenda
au kuchukia japokuwa viko vitu vingi
lakini kikubwa ni BINADAM mwenzake.
Kwa kiasi kikubwa utakuwa karibu na binadamu wenzako hata
kama utakuwa unapenda mifugo kwa kiasi gani? Hama ulikuwa unapenda kilimo kwa
kiasi gani naam hata gari au nyumba kwa vitu hivyo haviwezi kuongea na wewe
katika lugha ambayo itakuwa rahisi kuielewa kwa haraka kama binadamu mwenzako
akiongea.
Hivyo binadamu kwa kiasi kikubwa atakuwa karibu yako! Hivyo
anaweza kufanyika changamko au huzuni katika moyo na wakati mingine anaweza
kusababisha maswali katika ufahamu wako na kuanza kukufikirisha muda wote
unapomuona na hata usipomuona.
Kama kuna watu/ mtu unatakiwa kuwa makini nae ni mtu uliyempa
nafasi katika moyo wako( sio lazima awe mpenzi) na kumpa mambo yako nimeona
uadui mwingi ukianzaia hapo kwa mtu uliye mwamini sana na hata kumuheshimu na
baadae ukakuta ameweka wazi staha yako( siri) katika hali hii wako watu
wamepata vilema vya maisha kama vile stroke, BP( blood pressure), vidonda vya
tumbo na hata mtu kuwa na kichaa.
Katika michezo yoyote ogopa kucheza na mtu ambaye anakufahamu
kwani uwa atumii muda mwingi anakuwa amesha upata ushindi mapema (ushindi
asubui) na wakati mwingine ataukiwa una mazoezi ya kupambana na tembo au simba
kama ujarekebisha mahali penye udhaifu huyo mtu wakati wote mpinzani wako
atatafuta nafasi akuangushe kwa kugusa mahali penye udhaifu wako.
Mbali na Mungu………..mtu anayekufahamu ni JANGA kwako pindi
mnapotofautiana unaweza kujikuta katika mazingira magumu sana ambapo ukuwai
kuwaza kama utafika hapo mathalani mtu unaye fanya nae biashara kwa shirika(
partnership) baada ya kujuana sana unaweza kukuta fedha zako zilizo kwenye
benki hazipo na hatimae biashara ikafa na malengo yote yakawa mwisho.
Tukienda kwa upande wa usalama mtu yeyote anayesumbua kichwa
sana katika uharifu lazima atakuwa mzoefu wa mahali hapo au mjuzi mzuri wa hayo
mambo ndomana uweza kusumbua katika kupata utatuzi wa haraka.
Mtu anaye kufahamu unaweza kuwa ulipiga hatua kumi lakini
ukajikuta unarudi hatua moja, ambayo kwa kiasi kikubwa itahitaji ukusanye nguvu
tena katika kuanza hatua nyingine.
Kwa hakika aliye karibu nawe anaweza kuwa Baraka kwako au
kuwa huzuni katika maisha yako!
Pamoja na yote bado neema ya MUNGU ipo kubwa sana katika
kukupa mwendo pamoja na yeye kwakua huyo akiwa karibu yako na zaidi sana akiwa
ndani yako basi UTAKUWA SALAMA!
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson………………………………………………………………..0764 018535
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni