Jumanne, 5 Desemba 2017

UHITAJI WANGU!



UTATUZI KATIKA UHITAJI

UHITAJI! UHITAJI! UHITAJI

Hakuna kitu kizuri sana kama uhitaji na hakuna kitu kibaya sana  kama uhitaji lakini vyote ukutegemea wewe!

Unaweza kuona mtu akilia baada ya kupata kitu na unaweza sikia akisema  “ ilikuwa ndio hitaji na lilisababisha nitoe machozi kila siku”………………………………!

Na mwingine unaweza kukuta anasema “ uhitaji wangu ndio ulioniponza”

Amani hama tumaini la uhitaji utegemea sana uhakika wa utatuzi,

Sio kila njia unayoitumia katika kutatua tatizo ndio njia sahihi ya kutatua tatizo wakati mwingine unaweza hisi unatatua hama unalimaliza jambo kumbe ndio unaanzisha jambo jingine ambalo linakwenda kuwa zaidi ya tatizo na hata kufuta maana ya wewe katika kujitahidi.

Moja ya kitu kinachodhihirisha kwamba huyu mtu anajielewa ni namna anavyoshughulika na uhitaji wake.

Mtu mwenye akili au mtu aliyepitia hatua hiyo pindi anapomuona mtu anavyo shughulika na uhitaji wake uweza kugundua na kusema kuwa sasa huyu mtu anajielewa hama anapotea.

Japo katika uhitaji ( kwa maana ya jumla ) kuna uhitaji katika mambo ya msingi ( basic needs ) na uhitaji katika mambo yasiyokuwa ya lazima ( luxury needs ).

Namna unavyoshughulika na uhitaji wa aina zote uweza kuonyesha uimara/ uwezo wa akili yako katika kuyamudu mambo yanayokukabili.

Uhitaji wa watu wengi umefanyika maafa kwao, kwani watu wenye uwezo wa kukupa/ kutoa hama kusaidia watu, wengi wao wametumia nafasi hiyo kuumiza maisha ya wengine katika kuweka maslahi yao zaidi.

Kama ni mtihani basi utakuwa ni mtihani utakao endelea kuwa sumbua watu wengi duniani namna ya kupambana na uhitaji wao, kwakuwa unaweza ukakidhi leo uhitaji wako kwa njia moja lakini kesho kwa njia hiyohiyo ukashindwa (fail) na hapo ndipo panic na kichwa kuuma uanzia hapo ( mawazo yasiyo kuwa na kikomo ).

Ni muhimu ufahamu wako uwe umenolewa vizuri ili kukusaidia kumudu changamoto zilizopo na zitakazo kuja kwakuwa utatuzi wa kesho ni bora zaidi kuliko utatuzi wa leo. ( kama ulishiba jana alafu leo kukawa hakuna chakula basi hapo ujue shibe ya jana hauta ikumbuka/ kuionea ufahari )

Kwakuwa haiwezi kuwa na maana kama jambo ulitatua jana alafu leo likakushinda mathalani unaweza kukuta binti anasema mimi mwanzo nilikuwa makini sana atanikaweza kumudu vishawishi nisipate mimba lakini alitokea kijana mwenye maneno ya ajabu yakanivutia hatimaye nikapata mimba baadae yule kijana akanitelekeza ( ni kweli inakuwa ni stori lakini inakosa maana sana kwakuwa haionyeshi ushujaa wako).

Kama unataka kuwa na maisha yenye ushuhuda/ yenye kumdhihirisha Mungu usipende vitu vilivyo rahisi rahisi, penda kutumia vizuri akili yako ( akili ni pana sana na kuongezeka kwake inategemea namna unavyoishughulisha ). Ili baadae ujivunie jasho lako.

“ uwa hakuna maana ya jana kama leo haionyeshi ushuhuda wako “

Uhitaji upo kwa kufanya akili aliyokupa Mungu ikusaidie na Roho mtakatifu kuonyesha ubora wake na sio kuleta maangamizi.

“ mtihani haupo ili ufeli (ushindwe) bali kupima uwezo wa akili yako katika kukumbuka, kuchanganua na uelewa wako!”

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………..0764 018535


Jumanne, 28 Novemba 2017

NGUVU YA KUJITAMBUA.






Uweza wa kufanya mambo na ujasiri unaozaliwa/ kutokana na kujitambua.

Kuna kujitambua kunako zaliwa na vitu vingi mathalani kujitambua kunakotokana na mila na desturi katika jamii husika kujua majukumu yake na kuyatekeleza, mara nyingi utegemea miaka ( rika na umiliki) pamoja na nafasi ya mtu katika ukoo na hata jamii husika.

Pia mtu uweza kujitambua hama kuanza kujitambua kutokana na elimu ( rasmi au isiyo rasmi) au baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu au wazee wenye hekima.

Ni ukweli usiopingika kuwa uhuru mkamilifu unakuja baada ya kujitambua na bila shaka kuonewa na kuteseka kunakuwa ni maisha yako baada ya kuishi maisha ya kutojitambua au kukubali kuishi maisha ya kutojitambua. 

Maisha ya kutojitambua hayana tofauti sana na maisha ya utumwa japo kwa kiasi kikubwa inaweza kuwa ni zaidi ya utumwa, kwani njia rahisi ya kuchukua haki ya mtu mfanye tu asijitambue.

Wagalatia 4: 1 Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa,  angawa ni bwana wa yote;
                       2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.

  Kujitambua kwa namna zote ( mila na desturi, elimu n.k) vinakikomo chake na kwa kiasi kikubwa haviwezi kukupa maisha uliyokusudiwa kuishi mathalani unaweza kuwa mtu fulani kama vile msomi mwenye daraja la juu sana katika masomo yako na zaidi ukawa unajitambua kutokana na elimu uliyonayo , unajipenda , unajielewa lakini maisha yakaenda pasipo kuona yale uliyotegemea mfano. 

Ukosefu wa kazi unayotaka hivyo ukajitahidi kuvumilia kutokana na masharti magumu yakupata kazi unayoitaka lakini mwisho ukakubali aibu ya mwili ( rushwa ya ngono) ili maisha yaendelee.
Pia inawezekana ulipata kazi kwa neema tu ya Mungu ( kwa uhalali) lakini ghafla pakatokea na mtikisiko kazini kuwa bila ya kutoa rushwa ( kwa ujumla ) kibarua kitaota nyasi! Hama kujiingiza katika mfumo fulani.

Karibu……………………!!

Nguvu ya kujitambua kunakotokana na Neno la Mungu!

Ø  Unaweza kushangaa kuona mtu anaogelea katika bahari kama samaki badala ya kuzama.

Ø  Unaweza kushangaa mtu anakula vizuri na kuishi vizuri na zaidi kunawiri wakati ulitegemea ameze vidonge afe kwa kile kilicho mkuta.

Ø  Unaweza kushangaa pia mtu uliyetegemea asuse kula na aondoke lakini ukakuta anajiachia zaidi na kupafurahia na huku akila kwa nafasi.

Kujitambua huku ni zaidi ya kulalia/kumiliki madini ( almasi/ tanzanite n.k) maana ubora unaotokana na hali hii hakuna mfano wake.

Unapojitambua kutokana na hali hii hapo ndipo unaanza kuishi maisha aliyokusudia ( maisha uliyotakiwa/ unayotakiwa kuyaishi ) na unapoliishi kusudi la Mungu kwa ukamilifu unakuwa Mungu duniani ( Mungu kuishi kupitia wewe) na udhihirisho wa Mungu unakuwa juu yako.

Kama kweli unataka kujitambua wewe ni nani basi liruhusu neno la Mungu linalokaa ndani yako likutambulishe. Na sio biblia inayokaa chumbani hama sebuleni pasipo kuwa kiongozi wa maisha yako bali kuwa moja ya pambo la nyumba na zaidi sana wakutambue kuwa wewe ni mkristo.

Huu ni utambulisho usiochuja bali unaongezeka siku kwa siku ( utambulisho unaotokana na Neno la Mungu).

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………..0764 018535

Jumanne, 14 Novemba 2017

USIPOTEZE MWELEKEO ( USIJISAHAU)






Moja ya vitu vya msingi sana vya kuzingatia ili ufike unakotakiwa kufika ni kuto poteza mwelekeo, ingawa mara nyingine unaweza kuupoteza kwa kujua hama kutojua!

Unapo poteza mwelekeo uweza kusababisha hali ya kuchelewa kufika katika safari yako hama kutofika kabisa! Na muhimu kujua atutimizi ndoto zetu kwakuwa tuna akili nyingi bali kwa kufuata maelekezo yaliyo sahihi.

Baadhi ya vitu vinavyoweza sababisha  kupoteza mwelekeo ni ugumu wa safari  unao onekana kwenye akili au hali ya kushiba ukasahau njaa.

Mara nyingi mtu anapolianza jambo au safari ( mwenye akili njema) anakuwa ana matarajio fulani au ana matarajio au analengo fulani lakini mambo yote haya yanaweza kutimia tu kama hutopoteza mwelekeo.

Ni muhimu kutambua ufanisi wa jambo utegemea sana umakini ulionao katika kufuata mwelekeo sahihi.

Ishara kubwa ya kupenda kule unakotaka kwenda/ unakotakiwa kwenda uwa aishii katika kupania na maandalizi ya kutisha bali ubwebwa na umakini pamoja na utayari wa kufuata mwelekeo unaotakiwa.

Kuendelea kudumu katika mwelekeo ulio sahihi bila shaka kuna gharama/ kujigharimu kwingi na hata kuchoka au kuishiwa hivyo kukubali hali hizi zote ni ishara ya kutokuwa tayari kupoteza mwelekeo na kuipenda ndoto yako.

Watu wengi wamekuwa wakitamani mambo mazuri na ya maana katika maisha yao pasipo kutia bidii au kujikita katika mwelekeo sahihi wa kumfikisha katika ndoto yake .

Muhimu kuliko yote kufuata mwelekeo kwa moyo wote hilo ni jambo sahihi na lina husisha mtu binafsi wala alinakufahamiana sana wala kujuana (atanionaje au watanionaje?- uwa wanakuona kama unavyojiona) 

Unapokua makini katika mwelekeo wako inapelekea hatua bora katika maisha yako kwa kuwa neema ya uwezesho inakuwa juu ya maisha yako.

Nini maana ya kupoteza/ kutopoteza mwelekeo?

-          Ni muhimu kujua kupoteza mwelekeo sio kutofanya kitu sahihi, unawezafanya kitu sahihi kabisa lakini ukawa umepoteza mwelekeo (wrong direction).

Mathalani mtu anaweza akaamua kulima mpunga ( kilimo cha biashara) baada ya kuvuna magunia ya kutosha akaanza kuwasaidia wahitaji  baada ya kuingiwa na huruma mwisho bidhaa zikaisha na mtaji ukafa.

Hivyo unaweza kufanya jambo sahihi kabisa lakini ikatokea ukapoteza mwelekeo basi usishangae kuona hicho kitu kikafa au kikienda mwendo wa taratibu sana.

Kutopoteza mwelekeo hauishii kufanya kitu/ jambo sahihi tu bali inahusisha katika namna sahihi + wakati sahihi + watu sahihi.

Hali hii sio lazima pawepo na mlipuko bali ni namna nguvu ya ndani inavyoweza kukuwezesha kuendelea katika mwelekeo sahihi wenye kukupa mpenyo.

Kujua na kufuata mwelekeo sahihi hii ni kwa faida yako na vizazi vyako!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535

Jumanne, 17 Oktoba 2017

UTULIVU WAKE NDIO UBORA WAKE?





Utulivu kama ungekuwa ni bidhaa basi kila mtu angependa kuwa nayo! 

kwa namna yoyote utulivu umekuwa ni kitu adimu katika ulimwengu tulio nao, na hivyo imepelekea kutafutwa sana na watu wengi……………! Na kwa kawaida bidhaa adimu inapelekea gharama kuwa juu.

Maana katika dunia ya sasa wazazi/ walezi hama ndugu wana penda wawaozeshe/ kuwaoza watoto wao na watu ( wenzi)  waliotulia, hivyo kutulia imekuwa sifa ikiangaliwa kwa namna ya pekee kutokana umuhimu wake wanao ufikiria, wengi wana amini kuwa wakimpata mtu mwenye utulivu ( aliyetulia) itapelekea kuwa na ndoa nzuri yenye maelewano na hatimaye kupelekea mafanikio katika maisha yao, mbali na swala la ndoa hata inapotokea unapokuwa na rafiki aliyetulia bila shaka watu wenye akili njema watakupongeza na kukushauri usimwache.

Japo kwa asilimia kubwa imetafsiriwa kuwa utulivu wa mtu ni ishara ya ubora wake, basi ni muhimu kutambua utulivu wa kweli na wa muda (feki).

Na hapo ndipo swali linakuja nini maana ya utulivu? Namjuaje kuwa huyu ni mtulivu? Bila shaka majibu unayo kutokana na mtazamo wako maana binadamu anayo fulsa ya kuwaza!

Japo wengine wanaweza kutafsiri neno utulivu katika hali inayompelekea hama kuonekana kuwa mzito katika kuongea na kutenda nadhani kwa wengi wazo hili linaweza kuja kwa haraka pindi unaposikia kuwa mtu huyu/yule ni MTULIVU, Na kwa watu wengi mtu mwenye sifa hizi ( mzito katika kusema na kutenda) awapendelei sana kwa kuwa wanaona anaboa.

Bali mtulivu kwa maana ya mtu anayeweza kutumia akili kiufasaha na katika hali ya wepesi na kusababisha matokeo makubwa na mazuri ni hali iliyo kivutio na inayopendwa na watu wengi kama sio wote.

Utulivu katika hali ya kimahusiana maana inayokuja hapo kwa wepesi ni mtu asiye mcharuko anaye maanisha anachosema anayemuheshimu na kumpenda mtu mmoja maalum mwenye nafasi maalum katika maisha yake na hali hii kila mtu uvutiwa nayo sio mkristo au mwisilam hama asiye na dini na pengine hata mcharuko mwenyewe apendi apate mcharuko mwenzake.

Ø  NI KWELI MTU ALIYE TULIA NDIYE BORA?

Ni muhimu kujua nini maana ya neno bora! Na ni kweli kila kilichotulia kina ubora ndani yake? Na huo ubora ndio unao uhitaji? Asante kwa majibu mazuri yanayoendelea katika kichwa chako sasa tunaweza kuendelea…………………….!

Japokuwa wakati mwingine utulivu unakosa maana pale tu kama hakuna kinacho kuvutia ( ubora) mathalani mtu anaweza kutulia kwa muda mrefu katika ndoa hama urafiki lakini ukosefu/uhaba wa fedha hali hiyo kwa watu wengi uwa inakosa maana kwakuwa hakuna kitu ( ubora) unaofanya afurahie utulivu wake.

Lakini unaweza kukuta mtu anazo hela za kutosha lakini pindi ukiwa naye ujisikii utulivu japo kuna ubora ( fedha) unaweza kushangaa mtu anajitahidi kuwa hapo hata kwa gharama yoyote.
Unakuwa wa maana sana kama kwako utulivu na fedha vinapatikana basi hapo unaweza kuwa lulu kwa watu wengi; wamama, wababu, vijana na hata kwa watoto ( unakuwa kipenzi cha wengi kwasababu…..) 

Utulivu ni kama nyumbani kwenu, unaweza ukapakimbia kwasababu uoni umuhimu wake wakati fulani lakini pindi yatakapo kufika utatamani tu urudi nyumbani ( nyumbani ni nyumbani).
Nakubaliana kuwa utulivu ni bidhaa adimu sana na watu walioambatanisha : UTULIVU+ NIDHAM+ UAMINIFU + BIDII= walifika mbali sana.

Utulivu usijifanye/usiwe nao kwasababu haujui bali yawe ni maisha yako yenye kukupa mwanga na hatua bora zaidi.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………….0764 018535