Jumanne, 4 Aprili 2017

ANAONDOA ILI UMTEGEMEE



ANAONDOA ILI UMTEGEMEE


Isaya 54:7 Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.

Sio kitu rahisi kutambua kuwa mtu huyu ananifanyia hivi ili na mimi baadae nijitegemee binafsi hasa inapokuwa katika mtazamo usiopendeza machoni mwako unaweza kuwaza kuwa anakuonea, amekuchoka hama hakuhitaji sawasawa na mwanafunzi anapoadhibiwa kwa ajili ya utovu wa nidhamu au jambo lolote ambalo mwalimu ataona njia nzuri ya kumrekebisha mtoto huyu ili baadae aweze kuwa mtu wa maana katika jamii basi uamua kumuadhibu kwa fimbo, lakini katika kipindi hiki picha zinakuwa tofauti kati ya mwalimu na mwanafunzi, mwalimu anaweza kukusudia jambo jema lakini kichwani mwa mwanafunzi anaweza kuwaza mambo mengi kamavile mpenda sifa, mnoko, hama uweza kumwita mwalimu wa mahasira.

Ila inapotokea unatambua kuwa yote ananifanyia mimi ili kwamba nami wakati ukifika niweze kujitegemea na hasa inapokuwa katika upande unao onekana vizuri mathalani unafanya na mtu kwenye kampuni(mmilki) akakwambia jitahidi kufanya vyema maana muda si mrefu nitakuachia hii kampuni iweze kuendesha maisha yako, kwa maana rahisi wewe utakuwa ndio mmilki wa hii kampuni na mimi nitaenda kufanya shughuli zingine!

Siku zote mtu anapokuwa katika kipindi cha mpito na asijue kuwa hiki ni kipindi cha mpito inakuwa ni shida sana, lakini kwa yule anaye pita katika kipindi cha mpito na akaelewa kwanini anapitia hapo inakuwa ni ahueni kubwa kwake……..mathalani mtu anajinyima kwasababu ya kutaka kufanya jambo kubwa hama kuna kitu amekianza hivyo anajinyima ili kukamilisha hicho kwanza, inawezekana kuwa anajenga hivyo hali hiyo upelekea kupunguza matumizi ya family/binafsi ili kukamilisha alilokusudia,

Unaweza ukajikuta una uhaba wa fedha(fedha hazitoshelezi mahitaji) ukapashida lakini uwezi jua inawezekana kuwa ni  Mungu anataka kukupeleka katika kiwango kingine cha kumtegemea.

KARIBU!

Mungu kama baba hama zaidi ya baba na hasa kwa mtoto wake ampendaye hawezi kukaa na kuwaza jambo lisilo na faida kwa mtoto/mwanae, fahari ya mzazi ni kuona mtoto anakuwa vile anavyotamani kuwa tena wakati mwingine ujitahidi kufanya kila anachofanya ili kuhakikisha anatimiza ndoto ya mtoto wake kwa gharama yoyote ataikibidi yeye kusimamisha mipango yake yote.

Luka 11:11 Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?

             12 Au akimwomba yai, atampa nge?

             13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?

Tatizo kubwa kwa Mungu sio kukupa bali ni namna anavyokuandaa kuweza kukupa kitu kitakachokuwa faida kwako na sio tatizo kwako, kitu kinaweza kuwa ni hichohicho lakini usipokuwa  na uwezo wa kukitumia vibaya kitakuwa akina thamani na hapo Mungu apendi kufanya jambo kwa hasara.

Kumbuka wanaisraeli walikuwa watoke misri kwenda kwa kanani kwa muda wa wiki mbili tu! 
 Lakini kutokana uwezo wao mdogo wa kuweza kumilki na kutumia tunu iliyopo kanani ilibidi wachukue miaka 40 wakiwa safarini kuelekea kanani badala ya wiki 2,
Kinachosumbua watu wa Mungu ni namna Mungu anavyokuandaa hama kuongeza hatua ya kumtegemea yeye kwa hiyo hapa panakuwa na mtihani sana kwakua baadhi ya vitu uweza kuviondoa kwanza kuipima akili yako je! Itafanya nini? Mathalani kukatwa mshahara, kufukuzwa kazi, kipato kushuka katika biashara zako.

Na wakati mwingi Mungu anavyokuandaa sio vile unavyopenda wewe hama vile mwingine alivyoandaliwa bali inakuwa ni yanamna yako kwahiyo usipojua kuwa ni Mungu anakuandaa unaweza kulaumu watu! Kuchukia na hata kusengenya.

Katika mazingira hayo hapo uweza kuona mtu bidii yake kwa Mungu inapungua na asipokuwa makini uweza kujikuta inapotea kabisa, lakini hali haitakuwa na nguvu sana katika kuendesha maisha yako kama kweli UTAMJUA MUNGU!

Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.

Mtu anayemjua Mungu asumbuki kwasababu tu kipato kimeshuka hama pesa hakuna bali upata tabu sana kuona Mungu hayupo. Ujitia nguvu kuona kama Mungu ninaye basi vilivyo vyake vitakuja kwangu!

ANAITWA MUNGU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni