Ubinafsi ni matokeo ya mtu aliye na NAFSI.
Kibinadamu kila mtu upenda mambo yote mazuri yaanzie kwake, hapo nafsi uweza kujisikia vizuri na fahari kama sio majivuno.
Hali hii uweza kutawaliwa/kuzibitiwa na kitu kinachoitwa penzi! Na uelewa pamoja na umuhimu kitu/mtu uweza kupelekea kuvunja ubinafsi wake.
Ubinafsi unavunjwa kwa ridhaa ya mtu sio kwa ukali au kulazimishwa!
Neno ubinafsi limekuwa likipewa picha mbalimbali wengine wakiashiria hali nzuri kwa maana ukiishi maisha ya ubinafsi ni rahisi kuendelea na wengine wanaposikia neno ubinafsi kichwani mwao uweza kutengeneza kitu kibaya hama kisichofaa katika maisha ya wanadamu kwa maana wana amini ndani yake kuna kujiangalia yeye tu, kujifikiria yeye tu, kujitanguliza katika mambo yote hasa yale mazuri.
Kwa kifupi ubinafsi hauna sura nzuri katika jamii hasa afrika na zaidi hasa katika jumuhia za wa kristo ( waenda kanisani) japo kuwa tunaweza kukubaliana kwa asilimia kubwa kitu chochote chenye faida uwa kina hasara basi pia tunaweza kukubaliana kuwa kitu chenye hasara kinaweza kuwa na faida.
Muhimu sana katika ubinafsi uweza kuvunjwa na mtu husika tena kwa ridhaa ya mtu husika kutokana na sababu zilizo nje ya yeye au zilizo zaliwa ndani yake baada ya kupata uelewa fulani alio ukubali katika moyo wake, na hatimaye akaamua kuvunja ubinafsi wake.
UBINAFSI WA MAANA…………………………………………………………………!!!
Ubinafsi wa Mungu ndani yako ni muhimu sana…………kama maisha ya ukristo yangekuwa ndege basi hali hii ya ubinafsi na Mungu ningesema ni engine ya ndege, kwa maana usalama wa ndege hauko katika mapambo ya inje bali upo katika ubora wa engine!
Sio jambo la kushangaza aina zote za ubinafsi zina kikomo na pengine mwisho wake ukawa ni aibu lakini sio ubinafsi wako na Mungu uliobeba hatma njema yote ya maisha yako, na amini kitu ukikifanya kuwa ubinafsi wako basi hapo utakipenda, utakisikiliza na kitazidi kuimarika katika mishipa ya damu yako,
Wafilipi 1:21 Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.
Uwa nafsi yako ikitawaliwa na kitu inapoteza matakwa yake,na isipo kitekeleza sawa na kilicho tawala nafsini mwake hilo linakuwa deni litakalo kusumbua
Kitu chochote unachokifanya kilicho jaa ndani ya nafsi yako unakuwa kama kipofu kwa lugha ya mtaani unaweza sema nafsi inapoteza nguvu mbele ya hicho kitu, kwa maana rahisi uwa haioni kama kuna hasara anaingia kutumika kwa kitu kilicho tawala au kushika nafsi yake.
Dalili kubwa kama hichi kitu kimetawala nafsi yako uwa hakuna aibu wala uwoga, hama neno itakuwaje? Hama itajulikanaje inakuwa haipo bali kila siku unasikia kufanya na pindi inapotokea ujafanya kitu unaona kama siku bado haijaanza…………… inakuwa ni wewe na uwandani wako (Mungu),
Ø Usalama wa nafsi yako ni kuhakikisha roho yake inampenda Mungu!
- Marko 12:30
INAITWA SIKU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………… 0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni