Jumanne, 22 Agosti 2017

NGUVU YA UTULIVU.







Utilivu ni moja ya hali inayopendwa na watu wengi kama sio wote, hutoshangaa ukisikia maneno toka katika kinywa cha mtu akisema  “ ningepata sehemu nzuri yenye utulivu wa kutosha ni pumzike nafikiri akili yangu itakuwa vizuri ”….. watu wengi wamekuwa wakiamini kuwa kama wakipata eneo zuri la utulivu na hatimaye akapumzika anajua mwili wake utakuwa katika hali nzuri na kuzidi kuimarisha afya yake.

Na wako wanao jikuta hawa pumziki vizuri sio kwa sababu sehemu sio nzuri bali ni kwa sababu ya kukosa utulivu unawezekana ukawa ni utulivu wanje au wa ndani,

Ni muhimu kutambua kuwa na UTULIVU katika jambo lolote sio lazima mazingira yawe yametulia, mazingira yanaweza kukosa utulivu kabisa yaani yamechafuka sana lakini wewe unaweza ukawa na utulivu wa kutosha sana endapo tu utatambua SIRI ILIYO KATIKA UTULIVU.

Ina aminika kuwa jambo lolote linalokukabili unapoingia katika utulivu kuna utatuzi/maamuzi ya busara yatatoka hapo, japo sio kila utulivu utapelekea maamuzi ya busara au ya maana kwakua wakati mwingine utegemea kinachoendelea ndani yako na kilicho ujaza moyo wako.

UTULIVU KATIKA MUNGU KAMA NJIA SAHIHI YA KUFIKIA HATMA YAKO?

Ni muhimu kutambua kuwa hatuwi watulivu kwasababu tunashida au tuna uhitaji fulani, huu sio msingi mzuri wa kutulia bali tunakuwa na utulivu ndani kwakuwa Mungu anataka tuwe watulivu maana yeye ndiye mleta utulivu.

Unapofanya utulivu kuwa ni maisha yako unakuwa na nafasi nzuri katika utatuzi uliobora kuliko kuanza kujikunja na kutafuta utulivu katika hali mbaya au mazingira magumu hali hii uwezi kushangaa mtu kuibuka na maamuzi ambayo Mungu, shetani na hata wanadamu watashangaa.

Tunapozungumzia utulivu  ni kitu cha kawaida sana, lakini neno hili unaweza usione maana pindi utakapo kosa sababu kutulia katika jambo fulani, na wakati mwingine unaweza kuona njia nyingi za kufanya kuliko kutulia japo baadae zinaweza kukugharimu,

Hali ya kutulia mbele za Mungu katika jambo lolote alijarishi hilo jambo ni kubwa hama ni zito kiasi gani Mungu atakupa njia rahisi ya kutoka hapo!

Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

Mungu akishikilia hisia zako na kukupa utulivu katika akili yako na kuweka mwanga katika macho yako moyo wako ili uweze kuona ile picha kamili iliyojaa utoshelevu wako katika yeye.

Eneo atalikiwa ni la namna gani aliwezitoa utulivu ulio bora kama utulivu ulio jikita katika Mungu maana yeye atakupa utulivu wake, akili yake na hatimaye kupata njia ya kupita.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni