Jumanne, 29 Agosti 2017

TATIZO TUNDA!






Katika dunia ya sasa sio ajabu kwa mambo haya kutokea;

Ø  Watu walioamua kuwa mwili mmoja na kuapizana kuwa ni kifo tu ndicho kitakacho watenganisha lakini sio ajabu baada ya muda si mrefu unaweza kuta wameachana!

Ø  Unaweza kukuta vijana wenye lengo la kuoana ( wachumba) walio tayari na kutambulishana kwa wazazi wao na hata kuwekeana viapo kuwa mimi ndo wewe na wewe ndio mimi (upendo wa hali ya juu-kama kweli kinachosemwa kinatoka moyoni na kimebeba dhamira njema) na unaweza ukute wamepelekana makaburini, milimani, maporomoko ya ajabu na hata kwenye maji yenye kina kirefu wakidhihirisha upendo wao lakini utoshangaa kufumba na kufumbua upendo umekwisha wamekuwa kama mtu na jirani yake!

Ø  Pia unaweza kukuta watu ni marafiki tu wazuri(walioshibana) wanashirikiana katika hali zote lakini pamoja na hali hiyo sio ajabu muda si mrefu wakawa maadui wa kubwa.

Ø  Mbaya zaidi unaweza kukuta mzazi anamfukuza mwanae aliye mzaa na kumwambia “ sitaki ni kuone katika macho yangu” katika ulimwengu wasasa hili jambo ni swala linaloweza kutokea tu.

Sote tunatambua hakuna jambo linafanyika pasipo sababu labda mtu awe amejawa na mapepo na yana mwendesha katika kufanya mambo mbalimbali, miongoni mwa sababu hizo ni hali ya mtu kutopata kile anachokita ( matunda), inawezekana ni katika ujinga hama usahihi.

Kwani wako watu walio kuwa katika ndoa waliona fahari hama kupenda kuwa na watoto na ikatokea watoto kuchelewa hama uwezekano wa kuzaa kukosekana kabisa basi hapo uweza kuona hakuna maana ya ndoa, mbali na hilo pia kuna watu waliokuwa marafiki/ wapenzi wakiwa na matarajio fulani labda kusikia maneno mazuri kutoka kwa mwenzake hayasikii hama vitu na zaidi sana kujaliwa(kupetiwapetiwa) vyote hasipo vipata anaona bora awe na gogo kuliko kuwa na mtu kama huyo.

Katika karne ya sasa uwepo wako unatambulika baada ya watu kuona matunda yanayotokana na uwepo wako sio nyumbani tu, hata ofisini kile unachozalisha kinaweza mfanya mwajiri wako awaze mtu mwingine au kukuwekea mazingira bora ya wewe kuzidi kufanya kazi kwa ufanisi.

Hivyo popote ulipo/ mtu uliye lazima hautamani uwepo wako kwa yale yanayo zalishwa baada ya wewe kuwepo, hakika thamani yako inaongezeka kutokana na kile unachokizalisha.

Karibu ……………………………………………………………

Mungu naye unapokuwa katika himaya yake atapenda kuona matunda yake aliyo yaweka ndani yako yakitoka na kuwa faida kwa ulimwengu wote sawa na kusudi lake.

Na hii imekuwa tatizo kwa watu wengi hasa jamii ya waaminio kuona utofauti ulio miongoni mwao na kuibua chuki baada ya kujifunza/kusaidiana……..wapo watu wana onyesha uhai wao mbele za Mungu kwa kutumika kwa faida ya kristo hivyo Mungu husika sana na maisha yao kwakua wana ugusa moyo wake na wengine wanaona kama wanakandamizwa pasipo kujua kuwa wanapaswa kutoa matunda yanayo faa .

Hata Mungu upenda kuona mtu anatoa matunda ambayo yeye aliyaweka ili aendelee kukutunza na kama hautoi matunda aliyo kusudia anaweza asione haja ya kuendelea kukutunza na hapo ndipo unaweza kuona hali ngumu ukiwa kama mwamini.

Yohana 15:1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
                   2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
 
Ili ukae mahala popote na mtu yeyote hasa mwenye akili njema jaribu kuzalisha matunda ambayo yeye anayategemea toka kwako ili azidi kuufurahia uwepo wako na kuzidi kuhusika na maisha yako,
 
INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………........……………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni