Jumanne, 19 Septemba 2017

USIANGALIE KINACHO ONEKANA.






Ni kawaida ya dunia kuwa kitu chochote chenye sifa ya kuonekana basi ni sharti kiangaliwe na kama akionekani kwa njia moja basi kuna njia zingine, na pindi unapoangalia kitu kuna matokeo yatazaliwa hapo; unaweza ukaona kawaida, hama ujasiri ukaimarika ndani yako au hofu na mashaka vikaongezeka ndani yako!

Mara nyingi kitu chochote chenye mvuto machoni pako ni wazi tu moyo wako utavutiwa kuangalia pasipo kujali matokeo yatakayo kupata mara tu baada ya kuangalia!

Ni kweli vingi vinaoneka lakini si vyote vyenye sifa ya kuangaliwa sawa na unapoona moto umekolea sana ukasema ngoja niweke mkono wangu dakika moja nijue unaunguzaje! Kitakacho tokea kitaweka alama katika mikono yako na utakuwa umejifunza kitu japo ni kwa maumivu.

Usiangalie Mazingira!

Tafsiri fupi ya mazingira ni kitu chochote kinachokuzunguka mathalani miti, bahari, wanyama na vitu vingine vingine vikijumuhishwa vitu vinavyoonekana na visivyoonekana.

Lakini mimi sizungumzi mazingira hayo, naongelea mambo ambayo yanayo kutokea na hata kuweza kubadilisha kabisa mfumo wako wa kufikiri, maamuzi, hisia zako na hata mtazamo wako na mwisho hata kupelekea kubadilisha mwenendo wako mzima.

Mazingira hayo yanaweza kuwa ni ugonjwa, kazini hapako sawa, kukosa utulivu katika familia na mengine mengi.

Ni kweli jambo linaweza kukujia na ukaona aibu yako, kushindwa kwako lakini tambua aliyeliruhusu anakazi nawe.

Macho ya mwili yasitoe maamuzi katika mambo yanayokukabili lakini yako macho yenye nguvu yanatoa njia ya namna ya kutoka hapo ulipo kama tu utayatambua na kuyapa nafasi. 

Katika biblia kuna kitu ninge penda ukielewe:

Kutoka 13: 21 Basi wakapanda wakaipeleleza nchi toka jangwa la Sini hata Rehobu, mpaka kuingia Hamathi.

25 Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi, mwisho wa siku arobaini.

 26 Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi.

 27 Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake.

 28 Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.

 29 Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani.

 30 Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.

 31 Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.

 32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.

 33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

Hauwezi kushinda vita dhidi ya mazingira yako kwakua uko karibu na mtu unaye muamini au anayeaminika? Bali utayashinda kwasababu ya wewe ni nani! Uwezo gani ulionao binafsi katika kuyamudu mazingira yako.

Mazingira magumu ni mitihani katika dunia, hivyo lazima uwe mwanafunzi unayeweza kujitegemea ili mtihani ukija usipepese macho kutafuta msaada wa ahueni.

Njia rahisi ya kutoogopa mazingira ni moyo wako kumshiba Mungu.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………0764 018535

Jumanne, 5 Septemba 2017

UNAHITAJI NEEMA YAKE!







Uhitaji ni swala lisiloweza kuachwa nyuma katika hali yoyote, tukikubaliana wote kuwa ili maisha yaweze kuendelea hatuna budi kutimiza uhitaji wa kitu husika mathalani binadamu ili aendelee kuishi hana budi kutimiza uhitaji wa mwili na moja la hitaji ni chakula, mbali na hilo hata gari ili liweze kwenda linahitaji vitu vingi pamoja na vyote moja ya kitu muhimu ni mafuta ( petrol au diesel) , kama mafuta yakiwa yamekwisha hata ukiwa mtaalamu kiasi gani hama dereva unayesifiwa kijiji kizima bado utashindwa kuliondoa gari hapo kwa kuliendesha.

Ukiangalia mmea ili ukue unahitaji vitu vya msingi kama vile mwanga, hewa, maji na udongo kwa kupata mahitaji hayo itarahisisha katika ukuaji wake vilevile katika mwili wa binadamu una mahitaji mengi lakini kimojawapo ambacho ni muhimu ni MAJI, tukiachana na hilo wataalam wanasema binadamu ana mahitaji makuu matatu: chakula, maradhi na mavazi.

Hivyo uhitaji ni kitu kisichoweza kukwepeka!

Karibu……………………………………………..
Hakuna kitu kizuri kama unapo kuwa na uhitaji wa kitu uka kipata kwa wakati muhafaka maana najua kuna raha inazaliwa pindi unapo kipata kitu unachokipenda, mathalani unapokuwa na kiu ya maji utapenda upate maji ili kiu kiondoke na kawaida uhitaji ndo uzaa matamanio na hapo jitiada na mikakati uweza kuzaliwa.

Na ni kipindi hiki ambacho unaweza usimuelewe mtu pindi mtu anapo sumbuka katika kukizi uhitaji wake mathalani wanandoa wanaotaka kufunga ndoa na siku zimeisha na mambo ya msingi hayaja kaa vizuri unaweza usishangae kukutana nae kila eneo utakalopita mjini, barabarani na hata maeneo mengine, sio kwamba anapenda kurukaruka ila uhitaji wa kitu unamsukuma kufanya hivyo japo jambo hili sio hitaji la msingi ( kwa maana hauwezi kuishi bila kufunga ndoa) ila ni matwaka yaliyo ambatana na taratibu za jamii fulani.

Unahitaji neema ya Mungu na sio watu ili kukamilisha uhitaji wako!
Watu sio kwamba hauta wahitaji bali watapatikana ndani ya neema ya Mungu, maana Mungu atakupa watu wakukamilisha uhitaji wako, uwa katika picha ya haraka haraka sio rahisi kuona umuhimu wa neema ya Mungu hasa jambo unaona linawezekana kufanyika katika hali ya kawaida ,

Ila mara nyingi tunaona umuhimu wa neema jambo linapoanza kuwa gumu hama kuwa na picha ya kushindikana hapo utaanza kuona umuhimu wa neema ya Mungu, ni muhimu kutambua kila jambo linalokutokea linahitaji neema kwa kiwango kikubwa hama kwa lugha nyepesi unahitaji neema ya Mungu kwa asilimia zote.

Kikubwa kutambua watu wanaweza kukuacha hama kukusahau lakini sio neema ya Mungu ikikuambata haita kuacha kamwe kwa kifupi neema ya Mungu ni hitaji la dunia ukiikubali utaona utofauti wake uki kutofautisha katika utendaji wako.

Ni muhimu kuruhusu utawala wa kweli ya Mungu katika maisha yako ili neema yake uzidi kuiona ikiongoza akili yako na kukupa wepesi katika utendaji wako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………0764 018535