Ni kawaida ya dunia kuwa kitu chochote chenye sifa ya kuonekana basi ni sharti kiangaliwe na kama akionekani kwa njia moja basi kuna njia zingine, na pindi unapoangalia kitu kuna matokeo yatazaliwa hapo; unaweza ukaona kawaida, hama ujasiri ukaimarika ndani yako au hofu na mashaka vikaongezeka ndani yako!
Mara nyingi kitu chochote chenye mvuto machoni pako ni wazi tu moyo wako utavutiwa kuangalia pasipo kujali matokeo yatakayo kupata mara tu baada ya kuangalia!
Ni kweli vingi vinaoneka lakini si vyote vyenye sifa ya kuangaliwa sawa na unapoona moto umekolea sana ukasema ngoja niweke mkono wangu dakika moja nijue unaunguzaje! Kitakacho tokea kitaweka alama katika mikono yako na utakuwa umejifunza kitu japo ni kwa maumivu.
Usiangalie Mazingira!
Tafsiri fupi ya mazingira ni kitu chochote kinachokuzunguka mathalani miti, bahari, wanyama na vitu vingine vingine vikijumuhishwa vitu vinavyoonekana na visivyoonekana.
Lakini mimi sizungumzi mazingira hayo, naongelea mambo ambayo yanayo kutokea na hata kuweza kubadilisha kabisa mfumo wako wa kufikiri, maamuzi, hisia zako na hata mtazamo wako na mwisho hata kupelekea kubadilisha mwenendo wako mzima.
Mazingira hayo yanaweza kuwa ni ugonjwa, kazini hapako sawa, kukosa utulivu katika familia na mengine mengi.
Ni kweli jambo linaweza kukujia na ukaona aibu yako, kushindwa kwako lakini tambua aliyeliruhusu anakazi nawe.
Macho ya mwili yasitoe maamuzi katika mambo yanayokukabili lakini yako macho yenye nguvu yanatoa njia ya namna ya kutoka hapo ulipo kama tu utayatambua na kuyapa nafasi.
Katika biblia kuna kitu ninge penda ukielewe:
Kutoka 13: 21 Basi wakapanda wakaipeleleza nchi toka jangwa la Sini hata Rehobu, mpaka kuingia Hamathi.
25 Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi, mwisho wa siku arobaini.
26 Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi.
27 Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake.
28 Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.
29 Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani.
30 Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.
31 Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Hauwezi kushinda vita dhidi ya mazingira yako kwakua uko karibu na mtu unaye muamini au anayeaminika? Bali utayashinda kwasababu ya wewe ni nani! Uwezo gani ulionao binafsi katika kuyamudu mazingira yako.
Mazingira magumu ni mitihani katika dunia, hivyo lazima uwe mwanafunzi unayeweza kujitegemea ili mtihani ukija usipepese macho kutafuta msaada wa ahueni.
Njia rahisi ya kutoogopa mazingira ni moyo wako kumshiba Mungu.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni