Duniani kuna watu ni wapenzi sana wa safari, yaani ujisikia raha tu kusafiri haijarishi hiyo safari ni ya kwenda wapi? yeye anaposikia safari tu basi hapo moyo wake unarukaruka hata pasipo kujua hiyo safari atafaidikaje nayo? Na wako wengine ambao si wapenzi kabisa na mambo ya safari pindi wanapo jua kesho wanasafiri raha yote moyoni inapotea na wakati mwingine hata kushindwa kutoa maamuzi aende au asiende…………na hata pengine kufikiria sababu gani nitoe ili niepukane na hii safari.
Kwa binadamu mwenye akili timamu anapowaza safari uwa anajua ni hali ya kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya lengo maalum pamoja na kujua umuhimu wake kwake hama kwa jamii husika.
Na hakuna kitu kizuri kama mtu kufika katika kilele cha safari yake ( kutimiza ndoto yake ) na kwa upande mwingine ni maumivu ya mtu aliyepanga na kudhamiria kufika katika safari yake akashindwa kufika.
Kwa maelezo mafupi kutamani kuwa mahali fulani/ mtu fulani ni jambo moja na kufika au kulikamilisha ni jambo lingine na lina maana sana kukamilisha, ni muhimu kutambua kuwaza/ kutamani sio kutekeleza hama kulikamilisha bali ni hatua ya kwanza.
Na ni kawaida jambo lolote unalolifanya katika hali ya ulimbukeni au kujifunza linaweza kuteteleka japo wakati mwingine kwa kiasi kikubwa jambo ulilojifunza linaweza kuacha alama fulani katika maisha yako kiasi kwamba ukitazama ile alama inarudisha akili yako katika tukio lililopelekea hiyo alama mathalani mtu aliyekatwa mguu pindi anapoangalia ulemavu wake bila shaka akili yake itamrudisha katika chanzo au jambo lililopelekea hali hiyo au maisha ya ujana ukakuta mabadiliko ya mwili yakakushawishi kufanya mambo mengi mwishoe ukapata/ukampa mimba baada ya hapo ukakosa mwelekeo wa maisha yako naam pindi utakapo amua kutathmini utatambua na kujua kwanini uko vile ulivyo.
Ni muhimu kutambua kuwa safari isiyo na kikomo haina maana kuwa ni safari isiyo na vikwazo hama isiyo na mwisho bali ni safari itakayotimiza ndoto yako haijarishi vikwazo vilivyopo ndani ya safari haviwezi kukwamisha safari yako.
Japo vikwazo haviogopi maandalizi yako ata ukiwa umejiandaa vipi bado utapata changamoto lakini pamoja na hayo bado unahitajika kuitambua/ kuyatambua mahitaji ya msingi katika safari yako ili bahari inapochafuka isikushtue sana bali ikupe wepesi wakutumia ile hadhina iliyo ndani yako na hatimaye kumudu hayo mazingira au kuyashinda.
Na mara nyingi katika safari mwanzoni mnakuwa na watu wengi lakini kadili safari inavyokuwa ikiendelea watu watakuwa wakipungua na inawezekana kwa wale wanaopungua wakiwa njiani wanaweza jisikia vibaya ila ndo hivyo hamna namna……..na hali hii unaweza kuiona japo kwa uchache katika uwanja wa elimu, riadha na hata mafunzo ya taasisi n.k
Ni muhimu kutambua kuwa kila hatua ya safari kuna mabadiliko hivyo usipoenda sawa na mabadiliko unaweza sababisha safari kuwa ngumu au kushindwa kufika kabisa mathalani akili za darasa la kwanza ukaingia nazo darasa la pili na kuona haiwezekani kubadilika na ukasema “ mimi ndivyo nilivyo” hakika darasa la pili litakuwa gumu kwako.
Safari wakati mwingi inategemea vitu viwili AKILI na UTAYARI, akili isipokuwa na mipaka uweza kuona kuendelea mbele kunawezekana, utayari wa hali ya moyo kuwa tayari kubadilika ili mradi safari iendelee.
INAITWA SIKU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………… 0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni