Uhitaji ni ishara kubwa ya uhai wa kitu, kiumbe chochote kilicho hai ili kiendelee kuishi kinahitaji kukizi mahitaji yake ya msingi na mahitaji hayo yana wezekana kuwa ni chakula, maji pamoja na hewa.
Na kama binadamu kuwa na mahitaji ni swala la kawaida sana lakini ni hitaji gani? Na wakati gani? Ni mambo ya kuzingatia! Ili uhitaji wako usiwe maangamizi.
Japo sote ni binadamu na ndomana tuna uhitaji lakini uhitaji utofautiana kulingana mtu na mtu, hivyo ukimwangalia mtu kwasababu ni rika moja hama jinsia moja usifikiri mtakidhi uhitaji kwa njia moja mathalani unaweza kukuta mtu analala mchana nawe ukasema ngoja nami ni lale mchana labda usingizi utakuwa tofauti pasipo kujua yeye kulala mchana labda anaumwa au usiku alikesha hama usiku ana kazi kubwa hivyo analala mchana ili kujiandaa kwa kazi baadae!
Ni kweli kulingana na kuwa na rika moja wote mnaweza mkawa na uhitaji sawa lakini mkawa tofauti wa kila mmoja katika kukidhi uhitaji wake.
Changamoto kubwa katika wanadamu wengi inakuja pale katika kukubali kuwa japo sote ni tuna rika sawa mwenzangu amepata ila mimi wakati wangu bado ujafika hama majira yangu bado hivyo ni kubaliane tu na hali yangu kwa sasa.
Unaweza kumuona mtu anaendesha gari barabarani ukaona ni kazi ndogo ( kama kushika usukani na gari utembea lenyewe tu ) lakini ukweli unaweza usiujue mpaka uende kujifunza, mbali na hapo unaweza kuishia kutamani kutokana na urahisi wake unauona kwa macho na hata kushangaa kwanini watu hawaendeshi gari! Na ikatokea siku moja ukathubutu kuliendesha gari ukiwa katika akili hiyo hapo ndipo utaona yale unayoyawaza na yaliyopo!
Yako maumivu mengi yanayozaliwa kwa watu wengi katika kuangaikia mahitaji yao pasipo kujua wakati upi sahihi!
Kuangaikia jambo pasipo kujua wakati wake hali hii ni zaidi ya mateso, kwani unaweza kuhisi upendwi, unanyanyaswa au kuona kuna watu wanakuzibia riziki. Mathalani mtoto mwenye miaka 10 akawa anawasumbua wazazi wake anunuliwe nyumba kubwa ili aweze kuishi mwenyewe katika hali hii atakama mzazi ana uwezo wa kununu ndege hawata thubutu kununua nyumba kwa ajili ya mtoto wake hata kama anampenda kiasi gani? Kwa kuwa wanajua haita msaidia kwa wakati huo ingawa katika hali hiyo mtoto anaweza kuhisi apendwi hama ana nyanyaswa na mengine mengi, lakini sio kweli ( mzazi mwenye akili anajua wakati sahihi wa kila kitu cha kumpa mtoto wake ampendaye).
Unapokuwa mikononi mwa Mungu ( mikono salama) huna haja ya kuumia na kuteseka kwa kukosa mahitaji yako kwa wakati unaofikiria wewe bali ni muhimu kutambua uko wakati wa Mungu wa kudhihirisha penzi lake kwako pindi atakapotaka kujivunia na kuonyesha kuwa hawezi kukusahau.
Kuna watu wamekimbia/ kupishana na baraka zao kwa kuchoka kusubiri, na wako hata waliotaka kujinyonga na hata waliojinyonga kwa kuona nafasi haipo tena.
Watu wanaweza kusema! Wakati utaonyesha uhalisia (ulistahili au ukustahili) huna haja ya kuona wakati umechelewa.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………… 0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni