Jumanne, 30 Januari 2018

MAONGOZI YA ROHO MTAKATIFU






Moja ya tatizo kubwa linalowakabili watu wengi hata kupelekea kushindwa kuelewana, kuwa pamoja na hata kushikamana ni UBINAFSI. Uwa tatizo la ubinafsi linazidi kuwa tatizo pale mtu anaposhindwa kutambua kuwa  mwenendo wake kuwa ni tatizo. ( hali ya mtu kuwa na tatizo na kushindwa kujua kuwa hilo ni tatizo na kuona ni maisha ya kawaida ili mradi nafsi yake ina jisikia raha ni hatari ).

Hautashindwa kukuta ugomvi/kutoelewana kwa watu wanaoishi katika nyumba moja kama kila mmoja akiangalia na kufanya vile anavyoona sawa machoni pake pasipo kuangalia mwenzangu ata athirika au atachukuliaje?

Yohana 6: 38  Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka

Wakati mwingine kukubali kujikana kwa ajili ya mwenzako ni ishara kubwa ya kuheshimu na kupenda ushirikiano pamoja na kutunza umoja thabiti ulio kati yenu.

Ni muhimu kila mtu aone jinsi gani mwenzangu atafaidika nae kuliko mtu mmoja angoje kupata mambo mazuri kutoka kwa mwenzake! ( mimi kwanza-ubinafsi).

Kama unataka kujivunia wokovu na kuona fahari basi kwanza hunabudi kujitathmini na kuona ni kweli utendaji wa Mungu ndani yako ndio una nguvu au utendaji wako ( ubinafsi ).

Moja ya raha ambayo Mungu anaiona kwako pindi anapokuona ni pale anapoona utawala wa Roho mtakatifu unaoshamiri ndani yako. Na hapo ndipo kauli ya kusema wokovu ni mgumu itaanza kukosa nguvu kwako, kwakuwa kama yeye alivyoweza kuushinda ulimwengu ndivyo atakavyo yashinda yote kupitia wewe.

Nikubaliane tu kuongozwa na Roho mtakatifu sio lelemama/kitu chepesi kwani kinahitaji uhuru wako upotee kwa kiasi kikubwa japo hakuna kitu kizuri kama hiki.

Kama hautakubali kupoteza uhuru wako basi sahau maongozi makamilifu ya Roho mtakatifu.
Na pindi utakapokosa kuwa tayari kwa ajili ya Mungu ( Roho mtakatifu ) sahau kupata raha ya Mungu iliyo kamilifu.

Kuruhusu utawala wa Roho mtakatifu kuchukua nafasi ndani yako hiyo ndio ishara kubwa ya KUMPENDA MUNGU.

Unapokubali kuongozwa na Roho mtakatifu maisha ya wokovu hayakuumizi kichwa kwakuwa yatakuwa yakiongozwa na kusukumwa na PENZI LAKE hivyo uzito na kutojisikia hakuta kuwa sehemu yako.

Ni muhimu unapoongozwa nawe ukubali kuongozwa kuliko kutoa njia zako hama kuona njia zako zinaweza kukusaidia.

Mithali 14: 12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

Ni kweli unapokua ndani ya wokovu unakuwa hunatofauti na mtu mwingine kwa maana ya mahitaji ( chakula, mavazi na makazi ) lakini maongozi ya Roho mtakatifu ndio funga kazi itakupa kila kitu upasacho kukipata maana yeye ndiye anayejua ulikotoka na kule unako kwenda.

Uwa inakuwa haina maana sana kama ukiwa na marafiki wengi wazuri wenye uwezo na busara na hekima za kutosha kama hauna urafiki nae maana hao wote wanaweza fanya sawa na uelewa wao ulio na kikomo na hata kubashiri kesho yako namna itakavyokuwa lakini sio Roho mtakatifu yeye abahatishi anachokwambia ndicho kinakuwa!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………. 0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni