Jumanne, 9 Januari 2018

NAREJEA!





Mahali / wakati ambapo unaweza kuona tabasamu la mgonjwa ni pale anapoona anaanza kurejea katika hali ya uzima wake aliokuwa nao awali na hii furaha uwa inaenda mbali hadi kwa wanao muuguza mgonjwa, kwani nao uwa na furaha na matumaini uweza kuzidi kuimarika.

Na uzuri katika dunia tuliyonayo hakuna jambo ulilolipoteza au uliloliona umelikosa lisiweze kurejea tena katika hali ya ubora zaidi na mvuto wa kipekee maadamu tu unaishi.

Hichi ni kipindi ambacho majeraha na machozi ya moyoni yanaanza kuwa adimu na furaha kuanza kuchipuka kwa namna nyingine.

Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;

Na ni vizuri kukubali kuanza upya hata kama iki kugharimu kitu gani kuliko kuendelea katika kukosea na maumivu.

Ni kama asubuhi yenye kuchipua tabasamu lililoadimika hama kupotea kwa muda mrefu itakapo chipua hadi nywele na ngozi uweza kuhisi furaha.

Hakika ni kipindi kinachopendwa na wengi japo mchakato wake usipokua mwangalifu unaweza usione kama kuna siku itafika ile raha uliyoipoteza muda mrefu itarejea tena!

Kila mtu anarejesha furaha yake kutokana na jambo husika na sio kila jambo tu linalomtokea mtu uweza kusababisha jibu katika maswali ya moyo wake:

(a)   Wako watu waliokosa watoto wakiwa katika ndoa zao kwa muda mrefu lakini pindi dalili za mtoto zilipoanza na hatimaye kupata mtoto basi hapo furaha na shangwe uweza kuwa dhahiri na mengine kubaki historia.

(b)   Pia wapo watu waliosota sana katika kusoma na kupitia changamoto nyingi kiasi cha kupoteza matumaini kama atakamilisha safari yao ya elimu inapotokea kufanikisha hazma yake ( kusudio la moyo wake ) basi hapo furaha isiyo ya kifani uzaliwa.

(c)    Inawezekana mtu alikosa kazi kwa muda mrefu mara tu baada ya kuhitimu masomo yake hama alishawai kupata kazi baadae akafukuzwa au kuacha mwenyewe baadae akapitia msoto mkubwa kiasi cha kupelekea kujuta maamuzi ya awali lakini mwishoe akapata nafasi iliyobora sana na hapo changamko la moyo uweza kuchipuka.

(d)   Sekta ya mahusiano (sekta pendwa ) inawezekana ulipitia katika misukosuko mingi ( uliyoitegemea na usiyoitegemea ) na hata kutembea na wapenzi wako ili wafurahie urembo wako ili waweze kutulia na wewe tu lakini mawazo yako haikuwa nia yao na baada kufaidi uzuri wako waka kuacha solemba ( hewani pasipo kujua/kujali utaangukia wapi ) pamoja na hayo bado ujana wako unaweza kuhuishwa kama tai na kusahau jana, na kuipenda sana leo na kujiandaa kwa ajili ya kesho.

UREJESHO WAKO UPO! NEVER GIVE UP.

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni