Jumanne, 23 Januari 2018

ACHA YAWE YAO!





Katika ulimwengu tulionao, mambo mengi yanafanyika na yanaweza onekana mazuri au mabaya kutokana na mtazamo wa mtu husika lakini sio kila jambo lazima na wewe ufanye au uache atakama linaonekanaje! Au limesaidia wangapi? Kila tendo utegemea majira yake, namna yake pamoja na aina ya watu husika.

Kuna mvutano mkubwa na mwingiliano wa mfumo wa dunia na wa Mungu, kwa maana yale yanayo endelea kwa watu wasiookoka kwa kiasi kikubwa ndio yale yanayo watokea wale waliookoka! usiniulize kwa nini kwani hata mimi nashangaa!;

Mathalani,

Ø  MAHUSIANO YA KIMAPENZI

(a)   Kuangalia muonekano kama chanzo cha mvuto wa kimapenzi .
-          Sifa zote hana lakini muonekano wake tu unaweza kummaliza mtu kabisa.

(b)   Anajulikana sana nami nitajulikana
-          Ukitembea na waridi nawe utanukia! Inategemea waridi la wapi?

(c)    Nitadumu nae kama mfuko wake hauta pungua.
-          Imekuwa kama ulimbo kivutio kwako , anapokuwa vizuri basi hapo tabasamu ataliona tofauti na hapo itakuwa sawa na chozi la samaki majini( hataliona tabasamu lako ).

(d)   Niko nae lakini bado natafuta.
-          Na hisi kama bado sijafika ngoja nizuge naye kwanza lakini akitokea mwingine aliyekizi vigezo vyangu kumwaga ni jambo la kawaida tu/ lisilopingika au kuhitaji mjadala.

-          Sina uhakika kama tunaendana sana ngoja niangalie kwanza.

-          Jinsi tunavyoenenda tukifika mwezi mmoja sijui! Maana dalili zinaonyesha muda wowote lolote linaweza kutokea.

Mambo haya yote yamekuwa ni mfumo wa dunia ( mwenendo wa watu katika dunia) na yamekuwa na nguvu hata katika maisha ya watu waliookoka na kupelekea kupoteza radha na ushawishi wa wengine kuokoka.

utendaji wa watu wengi unafanana hakuna utofauti wa utendaji picha ya kristo katika maisha ya wengi inapotea,

Ni kweli ili mradi unaishi katika dunia mambo yanayoendelea duniani utaendelea kuyasikia na pengine hata kukuathiri katika mwenendo wako.

Katika mambo yote usipoteze asili yako!

I petro 1: 23 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.

Kuyaona mambo au kuyasikia na hata kuyafahamu mambo hautakiwi kupoteza dira au mwelekeo wa maisha yako kama umeokoka kweli, jua tayari unao misingi mizuri katika maisha yako juu ya kila kitu kwa kuwa mwenye asili ya vyote yuko ndani yako.

Luka 1: 37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.

Ni muhimu ujue;
(a)   Katika mwingiliano wowote hatupo kustarehe tu au kuonyesha matambo bali tupo kulitekeleza/kulikamilisha kusudi la Mungu pamoja.

-          Raha na furaha inakuwepo tu kwakuwa mleta raha yuko ndani yenu haijarishi mna nini au hamna nini?

(b)   Jambo la msingi kwa Mungu kwa mwanae uwa ni kumstawisha kwa majira yake na hakuna msamiati “ Nimechelewa” kwa Mungu.

-          Unapokuwa wake yeye anaanza kushughulika na maisha yako.

Unapopita katika hali yoyote yeye anakuwa pamoja nawe.

Zaburi 23: 4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………….. 0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni