Jumanne, 16 Januari 2018

ANZA NA MWANZO!






Sio vibaya kupenda kitu kinachoonekana vizuri maana chochote kinachoonekana vizuri basi kitavutia hama kushawishi kuangalia japo si lazima uwe nacho.

Mara nyingi kitu kilichofanyika pasipo kuhusika hama kuhusishwa, uhuru na kujiamini unakuwa mdogo sana maana ujui uimara wake utadumu kwa muda gani hama kujigharimu kwa hao watu waliofanikisha jambo hilo?

Kuanza mwanzo kunakuwa ni jambo la kupendwa na watu wengi lakini shida inakuja pale unapoona hakuna haja ya kuanza upya hama ushirikiano mdogo katika kukutia nguvu katika kuanza upya au unawaza ni kuchelewa tu katika kuanza upya!

Moja ya changamoto inayowafanya watu kuona ugumu katika kuanza upya ni namna ya utofauti uliopo/ utakaojitokeza kati yake na watu wengine walio tangulia hapo unyonge na uzito uweza kuchipuka ndani ya mtu na hapo ukashindwa kuanza upya kwa kuhofia nitaonekanaje?

Jambo lolote linalokutokea haijarishi upana wake au limepelekea uharibifu kwa kiasi gani? Jenga hali ya utayari wa kuanza upya ili ufanye kitu katika hali ya ubora.

Hauhitaji kuhisi umechukua au itachukua muda mrefu kiasi gani kurudi katika hali uliyokuwanayo awali ( usijipe uzito mwenyewe au usifanye mambo kuwa magumu ) ni muhimu ujue nafanya hivi ili kupelekea kesho yako yenye kishindo zaidi.

Haupaswi kuangalia sana watu bali jali sana hatma yako ( ubinafsi wa maana ) maana ni wewe utatengeneza ubora wa ustawi wako na kizazi chako na sio mwingine maana hakuna anayeweza kukutengenezea maisha yako kama wewe mwenyewe ukiyashindwa.

Akili yako iwe katika hali ya kufanya vizuri na sio kushindana na wala watanionaje? Uwa wanakuona kama unavyoonekana!

Hata watu waliotengeneza au kufanya mambo makubwa yaliyosaidia katika jamii na ulimwengu tulio nao mathalani umeme, taa, meli na hata ndege walijali sana kile wanacho kifanya kuliko wanachokisikia kutoka kwa watu.

Mwanzo 6: 22 Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.

Na hapo ndipo utakapoona / kujua upekee wako na kuona kuwa haina haraka sana kufanya kitu maadam wengine wanafanya.

Kufanya kitu kitakacho kuonyesha wewe kwa uhalisia wako haijarishi kitachukua muda gani hiyo inakuwa ni ishara kubwa ya kujikubali na kujiamini kwa kuwa wewe nawe uliumbwa duniani kwa kusudi maalum nalo ndilo unalolitekeleza.

Unaweza kufanyika baraka katika mazingira uliopo kwa wewe kufanya jambo lenye manufaa katika jamii yako haijarisha hilo jambo au hicho kitu kili kugharimu kiasi gani hama kuchukua muda gani la msingi tu umetimiza ndoto yako.

Kubali kuanza mwanzo katika jambo husika maana hatima yako haiko katika muda bali iko katika mikono ya Mungu kama wewe ukizidi kuwa wa Mungu.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………… 0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni