Ijumaa, 25 Mei 2018

MAISHA MENGINE




Japo sote tunaweza sema/ ona tunaishi katika sayari moja ila ni muhimu kutambua kila mtu anaishi maisha yake sawa na utashi wa akili yake.

Na ukumbuke kuwa kila hatua katika maisha yako, unayoipiga ujue ina namna tofauti tofauti ya jinsi ya kuishi na ni mbali na hatua ya awali uliyotoka au unayotoka mathalani mwanafunzi aliye sekondari ni tofauti kabisa na mwanafunzi aliye chuo kikuu japo wote unaweza kuwaita kuwa wanafunzi, katika dunia kuna watu walio na hatua tofauti tofauti katika maisha japo wote ni wanadamu.

Kitu kimojawapo kinachoweza kuleta tishio katika akili za mtu ni katika kuyakabili mazingira mageni mathalani unaweza ukawepo marekani alafu ukatamani kuishi maisha ya kitanzania…. Pindi utakapoona mambo yamekuwa tofauti na namna ulivyofikiria unaweza kumuona shetani asiyekuwepo.

Kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayejua hatua fulani atakayoipiga katika maisha ili kufikia hali fulani ya maisha yake na  mwingine kujua natakiwa kuishi tu katika hali ya utayari pamoja na uvumilivu (subira) kuwepo ndani ya maisha yake pasipo kujua nini kitafuata. Japo kesho ni fumbo ila unaweza kuitengeneza kwa upande wako.

Katika maisha ya kusoma ni tofauti kabisa na maisha ya kufanyakazi binafsi au kuajiriwa na maisha kabla ya ndoa ni tofauti na maisha ya ndoa, na maisha ya ndoa kabla ya kuwa na watoto ni tofauti baada ya kuwa na watoto japo yote ni maisha na maisha yanaendelea tu, lakini utofauti uko pale pale ni kama 1 haiwezi kuwa 5 ndivyo hivyo utofauti utaendelea kuwepo.

Ni vizuri utambue kila hatua ya maisha uwa unajitengenezea mfumo wake na wala wewe hautengenezi mfumo wake japo unaweza kuweka kwa namna utakavyoona inafaa kwa namna yako ni sawa na nguo watu wengi/wote lazima tuvae nguo japo zote ni nguo ila utofauti unakuja pale namna unavyoivaa au namna ilivyoshonwa ili iendane na muonekano wake.

Pasipo kutambua kila hatua ina maisha yake hali hii imepelekea baadhi ya watu kujuta na hata kuhisi wana mikosi kwa kuwa yale wanayo yafikiria au waliyokuwa wanafikiria sio yale walio yakuta.

Kutambua kuwa kuna MAISHA MENGINE sio ishara ya kuanza kuogopa au kununua makabati makubwa au kufanya jambo lolote kuonyesha unahofu maisha yajayo bali kubwa ni akili kutambua au kuwa tayari kuikabili/kuyakabili maisha mengine.

Na ni muhimu utambue kiumbe chochote kina hatua zake na endapo kisipokuwa na hatua kitakuwa kinakufa, hivyo nawe kuwa na hatua nyingine ni ishara ya uhai tena ni jambo la kheri na furaha katika familia na ukoo pamoja na jamii inayokuzunguka na ni ishara kubwa kuwa unajitambua.

Kuwa na hatua nyingine katika maisha yako ni jambo lisilo kwepeka maadam tu unaishi lazima ujue kuna hatua itakuja baada ya hii, ni mimi kuitambua na kujiandaa kiakili.

Unaweza kuwa fundi wa kukimbia mambo mengi lakini kamwe hauwezi kuikwepa hatua inayofuata haijalishi una uzoefu kiasi gani katika mambo ya kukwepa.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………….........0764 018535  

Ijumaa, 11 Mei 2018

ULIMWENGU WANGU!





Ulimwengu ni dunia tunayoishi, sote wanadamu pamoja na wanyama bila kusahau na viumbe hai wengine………!

Ndani ya dunia wapo wanaofurahia katika nyakati au majira fulani na wapo wanahuzunika katika majira fulani,

Na uwa kuna picha inayotokea katika kichwa cha mtu pindi utakaposikia mtu akisema “ hii ndio dunia yangu au huu ndio ulimwengu wangu” japo maneno haya tafsiri yake utegemea sana lugha ya mwili ( body posture ) pindi maneno hayo yanapotoka katika kinywa cha mtu.

Muonekano udhihirisha hisia za mtu.

Maana rahisi inaweza kuja kichwani unaposikia mtu akisema “ ULIMWENGU WANGU”  unaweza kupata tafsiri ya mambo yanayo mkabili mtu husika inawezekana kuwa kiuchumi, mahusiano na hata mambo ya kijamii kwa ujumla wake!
Katika watu wenye imani zao, wanapozungumzia ulimwengu wao uweza kumaanisha mahali ambapo macho ya nyama hayaoni bali huo ulimwengu upo katika hali ya kufikirika japo unaweza kubebwa katika uhalisia wake lakini mtamkaji wa hilo neno anaweza akawa analitambua.

Unaposikia mtu mwenye akili timamu anasema neno hili “ ulimwengu wangu”  akimaanisha maneno haya toka moyoni mwake katika udhihirisho vionjo vya mwili wake vikiongozwa na sura yake hilo neno linakuwa limebeba maana kubwa kwake kuliko kitu chochote utakacho fikiria.

Wako watu wanalia usiku na mchana lakini wakitambua mambo wanayo yapata ni kwasababu/ asili yake ni ulimwengu anao ujua yeye uweza kujikuta kichwa kinakubali japo moyo hauko tayari kwa hali hiyo inayodidimiza ndoto au matarajio yake.

Lazima utambue unaweza kuishi katika ulimwengu ulio na uweza nao au katika ulimwengu unaokushinda inategemea NGUVU na MAARIFA ULIYONAYO.

Hakuna kitu kibaya kama kuishi katika ulimwengu unaokutesa, inakuwa sawa na mtanzania kuishi uarabuni uku umenyang’anywa kibali cha kuishi huko.

Ni muhimu kutambua  mnaweza kuishi watu wawili katika nyumba moja lakini kila mtu akaishi katika ulimwengu wake hivyo unaweza kukuta mmoja analia na mwingine anafuraha kupita maelezo.
Kuishi katika ulimwengu mwingine wakati mwingine ni uchaguzi wako kwani unaweza kuyaruhusu mawazo yako hama kuto ya ruhusu mawazo yako kuishi huko.

Usipokuwa vizuri unaweza kuishi katika ulimwengu unaokula na kumaliza furaha pamoja na matumaini yako.

Unahitaji kujua kuwa ulimwengu hupo kwa ajili ya kuwezesha maisha ya mtu yaende ni sawa na uwepo wa maji kwa ajili ya viumbe hai kuishi naku pafurahia. Ila unaishije inategemeana na uwezo wako wakukabaliana na hali ilivyo.

Ni muhimu kutambua huko ulimwengu uliotengenezwa na wewe ukajikuta uko huko pia uko ulimwengu ulio utengeneza uka kuweka vile ulivyo na yote haya yote yanadhihirika katika uhuru wako au utekwa, katika yote la msingi nafanyaje ulimwengu wangu kuwa bora au natokaje mahala hapo.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………0764 018535

Ijumaa, 4 Mei 2018


MUNGU HAONGWI


Moja ya kitu kinachoweza kukuonyesha kuwa wewe ni wakisasa ni uwezo mkubwa wa kupata fursa pasipo kujali hizo fursa unazipataje? ( unatoa rushwa au hautoi ).

Imekuwa ni mtindo wa kisasa na kukubalika kwa haraka kama sio kwa wepesi katika jamii kwa kundi la watu fulani, vitu vingi ili uvipate utahitaji lazima ulainishe viwe rahisi kuvipata au kuvimeza, ndomana kukaibuka na misemo mingi iliyo na maana iliyo wazi au iliyo jificha kama vile, ili ule lazima nawe uliwe, mtaka cha uvunguni sharti ainame, ukitaka……………..penyeza rupia, ukipenda boga  penda na ua lake na misemo mingi, na hii yote ni katika kujirahisishia ili mambo yako yaende.

Imekuwa ni kawaida kana kwamba ni mafuta kwenye gari kwa kuwa gari aliwezi kwenda pasipo mafuta ndivyo imekuwa bila ya kuongwa au kuonga maisha hayaendi sawa, hivyo ndomana mtu akitaka kitu/mtu ( msichana au mvulana ) lazima aonge kama njia ya rahisi ya kupata uhitaji wake sio hilo tu hata mtu akitaka kazi anaweza kuweka uwezekano wa kutoa ongo, na hii imeenda mbali kidogo hata unapotaka ( haki yako ) utoshangaa mtu akitoa ongo au kudai/akitaka ongo.

Imekuwa kwenye akili ya watu kiasi kwamba mtu akipata huduma/ kitu pasipo kutoa ongo uweza kupata wasiwasi na kujiuliza hii hali/jambo linawezekana vipi? Kwa hiyo anapotoa hivyo uweza kujisikia vizuri na kupata uhakika zaidi kuwa hicho kitu atakipata au ni chake.

Hali hii imetawala na kuzidi mpaka inatisha na kuonekana ni kitu cha kawaida na kufanya rangi nyeusi kuonekana nyeupe, kitu ambacho si halali sasa kimehalalishwa.

Naam hali hii imefunika macho ya watu mpaka kuona mtindo huu unaweza kutumiwa hata kwa Mungu.

Pindi mtu anapokuwa na shida au uhitaji unaenda na kitu kwa Mungu, ukitazamia jicho la Mungu likuone huruma na kunyosha mambo yako na hivyo hali hii imepelekea hata watumishi kushawishiwa na kuona njia rahisi ya kuwapata watu na fedha ni kubuni utaratibu fulani kwa kuwatoza hela kwa kila tatizo na ukubwa wa tatizo ndio wingi wa hela na kushawishi hata kusema ili utoke kwenye shida/tabu yako ni lazima utoe kitu.

Sauli “ bwana upendezwa na dhabiu kuliko kuitii sauti ya bwana”

I samweli 15:22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

Ni muhimu kutambua sio utaratibu wa Mungu kuwa lazima utoe pesa ili upokee bali anataka maisha yako kwa ujumla umpe yeye…………………..japo na kubaliana kabisa Roho mt. anaweza kukugusa utoe kitu ili uweze kutoka katika shida/maangamizi yako.

Hii hali ya kutoa ili upokee pasipo kujua unatakiwa kupokea nini? Hali hii ni hatari sana katika maisha yako na Mungu, kwa maana usipoiona au kupata vile ulivyotegemea kuacha wokovu ni jambo linaloweza kutokea wakati wowote.

Ni muhimu uhitaji wako kwa Mungu ujengwe katika PENZI ( itokee au isitokee ) isikupe shida ili mradi penzi lipo usiwe na hofu ustawi utakuwepo tu.

Usipende sana kuwa makini katika kuona uhitaji wako unatatuliwa bali elekeza umakini wako katika penzi lenu linakuwa siku kwa siku.

Ndani ya penzi kuna kukidhi mahitaji yenu pasipo msukumo wa nje yenu ( kila mmoja uwajibika kwa ajili ya mwenzake ) wala hakuna kutegemeana/ kutegeana.

Kunatofauti kubwa kati ya kuomba Mungu kukidhi uhitaji wako ukiwa ndani ya penzi na inje ya penzi.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………….. 0764 018535