Ijumaa, 25 Mei 2018

MAISHA MENGINE




Japo sote tunaweza sema/ ona tunaishi katika sayari moja ila ni muhimu kutambua kila mtu anaishi maisha yake sawa na utashi wa akili yake.

Na ukumbuke kuwa kila hatua katika maisha yako, unayoipiga ujue ina namna tofauti tofauti ya jinsi ya kuishi na ni mbali na hatua ya awali uliyotoka au unayotoka mathalani mwanafunzi aliye sekondari ni tofauti kabisa na mwanafunzi aliye chuo kikuu japo wote unaweza kuwaita kuwa wanafunzi, katika dunia kuna watu walio na hatua tofauti tofauti katika maisha japo wote ni wanadamu.

Kitu kimojawapo kinachoweza kuleta tishio katika akili za mtu ni katika kuyakabili mazingira mageni mathalani unaweza ukawepo marekani alafu ukatamani kuishi maisha ya kitanzania…. Pindi utakapoona mambo yamekuwa tofauti na namna ulivyofikiria unaweza kumuona shetani asiyekuwepo.

Kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayejua hatua fulani atakayoipiga katika maisha ili kufikia hali fulani ya maisha yake na  mwingine kujua natakiwa kuishi tu katika hali ya utayari pamoja na uvumilivu (subira) kuwepo ndani ya maisha yake pasipo kujua nini kitafuata. Japo kesho ni fumbo ila unaweza kuitengeneza kwa upande wako.

Katika maisha ya kusoma ni tofauti kabisa na maisha ya kufanyakazi binafsi au kuajiriwa na maisha kabla ya ndoa ni tofauti na maisha ya ndoa, na maisha ya ndoa kabla ya kuwa na watoto ni tofauti baada ya kuwa na watoto japo yote ni maisha na maisha yanaendelea tu, lakini utofauti uko pale pale ni kama 1 haiwezi kuwa 5 ndivyo hivyo utofauti utaendelea kuwepo.

Ni vizuri utambue kila hatua ya maisha uwa unajitengenezea mfumo wake na wala wewe hautengenezi mfumo wake japo unaweza kuweka kwa namna utakavyoona inafaa kwa namna yako ni sawa na nguo watu wengi/wote lazima tuvae nguo japo zote ni nguo ila utofauti unakuja pale namna unavyoivaa au namna ilivyoshonwa ili iendane na muonekano wake.

Pasipo kutambua kila hatua ina maisha yake hali hii imepelekea baadhi ya watu kujuta na hata kuhisi wana mikosi kwa kuwa yale wanayo yafikiria au waliyokuwa wanafikiria sio yale walio yakuta.

Kutambua kuwa kuna MAISHA MENGINE sio ishara ya kuanza kuogopa au kununua makabati makubwa au kufanya jambo lolote kuonyesha unahofu maisha yajayo bali kubwa ni akili kutambua au kuwa tayari kuikabili/kuyakabili maisha mengine.

Na ni muhimu utambue kiumbe chochote kina hatua zake na endapo kisipokuwa na hatua kitakuwa kinakufa, hivyo nawe kuwa na hatua nyingine ni ishara ya uhai tena ni jambo la kheri na furaha katika familia na ukoo pamoja na jamii inayokuzunguka na ni ishara kubwa kuwa unajitambua.

Kuwa na hatua nyingine katika maisha yako ni jambo lisilo kwepeka maadam tu unaishi lazima ujue kuna hatua itakuja baada ya hii, ni mimi kuitambua na kujiandaa kiakili.

Unaweza kuwa fundi wa kukimbia mambo mengi lakini kamwe hauwezi kuikwepa hatua inayofuata haijalishi una uzoefu kiasi gani katika mambo ya kukwepa.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………….........0764 018535  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni