Ulimwengu ni dunia tunayoishi, sote wanadamu pamoja na wanyama bila kusahau na viumbe hai wengine………!
Ndani ya dunia wapo wanaofurahia katika nyakati au majira fulani na wapo wanahuzunika katika majira fulani,
Na uwa kuna picha inayotokea katika kichwa cha mtu pindi utakaposikia mtu akisema “ hii ndio dunia yangu au huu ndio ulimwengu wangu” japo maneno haya tafsiri yake utegemea sana lugha ya mwili ( body posture ) pindi maneno hayo yanapotoka katika kinywa cha mtu.
Muonekano udhihirisha hisia za mtu.
Maana rahisi inaweza kuja kichwani unaposikia mtu akisema “ ULIMWENGU WANGU” unaweza kupata tafsiri ya mambo yanayo mkabili mtu husika inawezekana kuwa kiuchumi, mahusiano na hata mambo ya kijamii kwa ujumla wake!
Katika watu wenye imani zao, wanapozungumzia ulimwengu wao uweza kumaanisha mahali ambapo macho ya nyama hayaoni bali huo ulimwengu upo katika hali ya kufikirika japo unaweza kubebwa katika uhalisia wake lakini mtamkaji wa hilo neno anaweza akawa analitambua.
Unaposikia mtu mwenye akili timamu anasema neno hili “ ulimwengu wangu” akimaanisha maneno haya toka moyoni mwake katika udhihirisho vionjo vya mwili wake vikiongozwa na sura yake hilo neno linakuwa limebeba maana kubwa kwake kuliko kitu chochote utakacho fikiria.
Wako watu wanalia usiku na mchana lakini wakitambua mambo wanayo yapata ni kwasababu/ asili yake ni ulimwengu anao ujua yeye uweza kujikuta kichwa kinakubali japo moyo hauko tayari kwa hali hiyo inayodidimiza ndoto au matarajio yake.
Lazima utambue unaweza kuishi katika ulimwengu ulio na uweza nao au katika ulimwengu unaokushinda inategemea NGUVU na MAARIFA ULIYONAYO.
Hakuna kitu kibaya kama kuishi katika ulimwengu unaokutesa, inakuwa sawa na mtanzania kuishi uarabuni uku umenyang’anywa kibali cha kuishi huko.
Ni muhimu kutambua mnaweza kuishi watu wawili katika nyumba moja lakini kila mtu akaishi katika ulimwengu wake hivyo unaweza kukuta mmoja analia na mwingine anafuraha kupita maelezo.
Kuishi katika ulimwengu mwingine wakati mwingine ni uchaguzi wako kwani unaweza kuyaruhusu mawazo yako hama kuto ya ruhusu mawazo yako kuishi huko.
Usipokuwa vizuri unaweza kuishi katika ulimwengu unaokula na kumaliza furaha pamoja na matumaini yako.
Unahitaji kujua kuwa ulimwengu hupo kwa ajili ya kuwezesha maisha ya mtu yaende ni sawa na uwepo wa maji kwa ajili ya viumbe hai kuishi naku pafurahia. Ila unaishije inategemeana na uwezo wako wakukabaliana na hali ilivyo.
Ni muhimu kutambua huko ulimwengu uliotengenezwa na wewe ukajikuta uko huko pia uko ulimwengu ulio utengeneza uka kuweka vile ulivyo na yote haya yote yanadhihirika katika uhuru wako au utekwa, katika yote la msingi nafanyaje ulimwengu wangu kuwa bora au natokaje mahala hapo.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni