Ijumaa, 1 Novemba 2019

ISHI KATIKA NDOTO YAKO!



Kuishi ni neema ambayo Mungu ametoa kwa kila kiumbe kilichokua hai.

Ninapozungumzia NDOTO! Katika muktaza huu Uwa sina maana mawazo yako ya siku nzima yanayojifunua usiku wakati umelala, bali ninazungumzia matarijio kamili ya Mungu katika kukufikisha kilele cha ustawi wako katika jambo Mungu ameliweka ndani yako.

Ni muhimu utambue kuwa kuna kuishi maadam unapumua, Napia  kuna kuishi kwa maana ya kuitumikia ndoto yako.

Hakuna maisha ya furaha kama ukiishi ndani ya ndoto yako, ni maisha yenye raha ni zaidi ya majigambo ya samaki akiwa majini.

Kama binadamu unaweza kutamani ndoto za wengine lakini kamwe usikubali kuishi humo kwani uwezekano mkubwa na kuangamia hapo upo! bali jifunze katika mema yenye mchango katika ndoto yako.

Unapoamua kuishi ndani ya ndoto yako hapo hakuna kushindana, manung’uniko wala majuto bali siku zote utaona deni la kufanya tu pasipo kuchoka.

Kuna maisha unayoweza kuishi ikapelekea ndoto yako kufa au kushamiri katika mwenendo wako wa maisha kila siku.

Moja ya kuwa faida katika dunia ni kuishi katika ndoto yako maana kwa kufanya hivyo itapelekea maana ya wewe kuishi duniani na utakuwa msaada kwa wengi.

Hauhitaji kuishi katika ndoto za wengine,kwani hali hiyo itapelekea kukosa mwelekeo unaweza kujikuta unafanya kitu ambacho akikuzaliwa ndani yako.

Moja ya sababu watu kuishi maisha ya mateso ni kuishi nje ya ndoto zao.

Ni muhimu utambue sio kila kitu unapaswa ufanye, bali ni kile kilichozaliwa ndani yako chenye tija katika ndoto yako na sio kuleta majeraha katika maisha ya wengine.

Mtu anayeishi katika ndoto yake uwa ajui nini maana ya kuchelewa katika hatma ya ndoto yako.
Usiruhusu jambo lolote hata liwe zuri kwa namna gani endapo utagundua litakutoa nje ya ndoto yako usifanye hata iki kugharimu kiasi gani au hasara ya muda fulani?

Unahitaji kujua kwamba maana ya wewe kuumbwa ni pale utakapoanza kutembea katika ndoto, utafanya Mungu ajivunie kwa kukuruhusu uje duniani.

Mungu afanyi jambo kwa hasara au kwa kumkomoa mtu bali ufanya yote ili kuhakikisha ufalme wake unaimarika.

Mungu anataka uwe faida kwa wengine kwa wewe kujizatiti katika kuishi ndani ya ndoto yako!
Nafuu usingezaliwa kuliko ukazaliwa alafu ukaishi nje ya ndoto yako inakuwa sawasawa na mtu ( mwanafunzi ) aliyefanya mtihani akaona kuwa ulikuwa rahisi baadae akagundua amefanya kinyume na swali linavyotaka/hitajika kwa kifupi ameenda O.P (Out of Point) na matokeo yake yaka gharimu maisha yake.

Unaweza kuwa na kila kitu ambacho binadam anapaswa kuwa nacho lakini ukiwa nje ya ndoto yako hivyo vitu hautaona radha ya maisha iliyokamili kuwa navyo japo unaweza kucheka, kufurahi na kujirizisha nafsi yako kwa maneno au kwa kufanya vitu vingi lakini kamwe haitasaidia.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni