Ijumaa, 6 Desemba 2019

UZURI WA KUSUBIRI




“ subira yavuta heri” ni msemo uliozoeleka katika jamii! Na ulio na funzo ndani yake, japo ni kweli kwamba sio kila kitu unachosubiri kinakuwa na heri! Lazima utambue hicho unachosubiri kinasifa yakusubirika………….maana usije ukawa unasubiria yai viza ili upate kifaranga!

Karibu……………pindi unapomuona mkulima anachukua mbegu mathalani za mahindi na kuzifukia chini ( kupanda ) na kuondoka nyumbani kwake,pasipo kuwa na hofu au mashaka bali uwa na furaha sana hata katika uchovu wake, uweza kusikia raha katika mifupa na nafsi yake akijua subira yake itakuwa na matunda yatakayo rudisha nguvu yake na muda wake alioutumia.

Pia tunapomwangalia kuku ( wa kienyeji ) baada ya kutaga kwa hiari yake mwenyewe anayaatamia hayo mayai siku ishirini na moja ajali kuchelewa wala kuwai bali utegemea/kugonja miito ya watoto wake ( vifaranga ) pasipo kuchoka.

Vilevile uwa sipati picha kwa mwanamke wa kwanza kushika ujauzito sijui alikuwa katika hali gani aliyokuwa nayo kwa kile alichokibeba. ( kwakuwa apakuwa na muda maalum wa kusubiri, kwahiyo akujua wakati gani sahihi wa kukitoa kiumbe duniani )!

Napenda kukubaliana kuwa kusubiri sio jambo dogo , kwa maana wako watu walisubiri sana hata hatua ya mwisho lakini akakosa kile alichokuwa anasubiria naam hata asione tena maana ya kusubiri na wako waliosubiri mpaka mwisho lakini akashindwa kuvumilia hatimaye akakosa muujiza wake.

Moja ya sababu inayosababisha kushindwa kudumu katika kusubiri, ni hali ya mtu kuwa na subira yenye matumaini katika mwili mathalani hali ya kisasi-ngoja naye yampate tuone huo ujasiri ataupata wapi,  au wakati mwingine mtu kuwa na matarajio fulani kwa mtu mfano nilijua yeye atanioa hivyo inabidi nimvumilie hatakama hananidham amejaa kiburi wala anipendi najua atanioa maana najua moyo wangu umempenda,uwezekano wa kufanikiwa unakuwa ni mdogo.

Hama, Nimeishi katika ndoa miaka mingi nilijua ipo siku atatambua thamani yangu na kuanza kuniheshimu lakini wapi?

Nikubaliane kuwa moja ya kitu kinachoweza kufanya kushindwa kufika kileleni ni hali ya kushindwa kusubiri.

Naam sasa tuingie kwenye kiini cha somo “ uzuri wa kusubiri “ jambo lolote unalolisubiri lazima pawepo na raha ndani yako iliyobebwa na uhakika na maarifa uliyonayo au amani inayotokana na imani yako ( Ni muhimu iwe sahihi ).

Lazima uwe na uhakika wa furaha ya kweli kwa kile unachokisubiria na sio kwa wasiwasi wala mashaka.

Uzuri wa kusubiri ni njia rahisi ya kupata kitu sahihi kwa wakati sahihi japo kuna wakati mambo mengi yanakuzonga lakini moyo wa furaha katika hilo jambo ukupa maamuzi sahihi.

Hakuna raha katika kulazimisha jambo/mambo yatokee sawasawa na kuchuma  embe changa na kulivundika na uku ukitegemea liive na kuwa na radha nzuri.

Ni muhimu katika hali njema ya kusubiri utembee katika maongozi sahihi ( Mungu/Mtu ) ili ikurahisishie kufikia kile unachopaswa kuwa hama kuwa na hatua au nafasi unayotakiwa kuwa nayo!

INAITWA SIKU!BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………..0764 018535


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni