Yohana
14:27
“Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama
ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga”.
Moja
ya bidhaa/kitu adimu katika ulimwengu wa sasa ni AMANI, maana palipo amani
ndipo radha ya kitu unachokifanya unakiona,mtu uliye naye au mahali uliopo
upafurahie na siku zote uona sababu au umuhimu wa kuwa hapo.
Moja
ya kitu ambacho mtu angetamani awe nacho siku zote za maisha yake ni Amani ya
kudumu ndani ya maisha yake, na kizuri zaidi amani ikiwepo udhihirisho wake
utaonekana ila amani inapotoweka viashirio vyake utaviona na hapo unyonge na
ukiwa pamoja na hali ya kutoendelea uweza kujitokeza na hata kupelekea kupoteza
mwelekeo.
Tatizo
sio kuwa na kitu bali ni namna utakavyo kitunza ili kiendelee kuwepo “ uki
kitunza kitadumu “
Namna
unavyokaa nacho kinaweza kuzidi kukita mizizi yake au kupoteza utawala wake.
Wako
watu amani yao inatunzwa na kazi nzuri aliyonayo, rafiki mwenye uwezo wa
kumsaidia apatapo shida, mchumba au mali alizonazo n.k , inapotokea vitu hivyo
vikipotea/kuondoka uwa vinaondoka na amani yake kwakuwa vitu hivyo ndivyo
vilivyo shikilia amani yake hama ndicho chanzo cha amani yake ( hivyo
vinaondoka na amani yake ).
Sio
rahisi kujua msingi wa amani wa kila mtu unayemuona ( hasa jamii ya waaminio/
waendao kanisani ) uwa wengi upenda kusema “ amani yangu ina Mungu” huna haja
ya kubishana nao, subiri vile vitu halisi/ hasa vinavyoshikilia amani yake
pindi vitakavyopata mtikisiko utoshangaa hata ratiba za kanisani zitaanza
kupungua na kuanza kambi za ghafla ghafla pamoja na maombi yasio kuwa na
mpangilio maalum bali yanasukumwa na hisia pamoja na msongo wa mawazo.
Kujua
kuwa “ amani yako inatunzwa na Mungu “ na kuifanya “ amani yako itunzwe na
Mungu “ hivi ni vitu viwili tofauti ni sawa sawa na mbingu na nchi, uwezi
kuirahisisha kimawazo ukasema mbingu na nchi vinafanana ukaachana na uhalisia
uliopo!
Natambua
kuna vionjo vya mwili vinavyobebwa na matukio mazuri yanayomtokea mtu mathalani
kuifikia/kuikamilisha ndoto yake, moyo uweza kuchangamka na kusababisha
tabasamu kwenye uso.
Hatua
ya kwanza ili uwe na amani iliyozaidi ya amani zote jambo muhimu lazima umpate
Mungu kwanza ili akupe amani yake hiyo AMANI hainaga mbadala, uwezi kutamani
amani ya mtu wakati mtu mwenyewe umtaki! Lazima umpate mtu hapo ndipo utaanza
kuiona amani yake.
“
palipo na yeye amani yake ipo”.
Usikubali
“ kujitekenya na kucheka mwenyewe ” huku ni kupoteza muda unapoamua kuwa na
amani ya Mungu basi hakikisha unampata Mungu kwa ukamilifu wake.
Hii
itafanya/kuzidisha mng’ao wako kuzidi wala usififie maana uko katika amani
inayonawirisha.
INAITWA
SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa
na:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni