Ijumaa, 31 Januari 2020

HII PINGU NI KWA AJILI YAKE!




Pindi unaposikia neno “ PINGU” akili yako inaweza kukupa tafsiri/picha ya kifungo kinachotokana na kosa fulani ambalo mtu amelitenda inawezekana kwa kujua hama kutokujua au kwa kukusudia hama kutokukusudia au kwa kusizingiwa hama ni kosa kwa uhalisia alilolifanya mtuhumiwa.

Na ni jambo linalojulikana kuwa maisha ndani ya kifungo ni maisha yasiyo na uhuru bali utumwa na mateso uwa ndio fungu lake.

Japo sio kila vifungo vinafanyika kwa watu ni bahati mbaya bali yapo baadhi ya makosa ambayo mtu anayafanya kwa kujua kabisa kuwa baada ya tukio hili ambalo na kwenda kulifanya kifungo ni haki yangu mathalani unaweza kukuta mtu/watu wanasema “ kwa kosa/jambo hili nililofanyiwa wachanifanye haya japo najua kifungo na mateso ndicho kitakachofuata “

Ukiangalia kwa mapana zaidi wakati mwingine ukweli kifungo akimtesi mfungwa tu bali hata wale wanaouhusiana karibu naye wanateseka, kwani mbali na kukosa uwepo wake kwa karibu pia inawezekana hata jamii yake kukosa huduma ulizokuwa unawapatia, hivyo jamii yake ikiyakumbuka yote hayo majonzi na huzuni itatawala mioyo yao na hatimaye maji adimu yakaanza kutiririka machoni ( machozi ).

Pia unaweza kuingia kifungoni pasipo kujua kwanini yamekukuta hayo na kukuingiza hapo lakini mwisho wa jambo inaweza kuwa funzo kwako au kwa mtu mwingine na wakati mwingine hilo jambo linaweza kuwa faida kwa mtu mmoja au familia, jamii na hata taifa kwa ujumla wake.

Mwanzo 45:5………… Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu.

Haya ni maneno ya yusufu baada ya kutoka gerezani na kuwa na nafasi ya juu katika ufalme wa farao, yeye alikuwa na uwezo mzuri kutambua sababu ya kifungo chake!

Na ni ukweli kuwa uvumilivu unaweza kuzaliwa ndani yako pindi unapojua najigharimu hivi kwa sababu ya hiki au kile hama kwasababu ya mtu au watu pia wanaweza wasiwe na uhusiano nawe wa damu au WAKAWA NAO! Mathalani mzazi anapohatarisha maisha yake hata kujiingiza kwenye shughuli zitakazo athiri afya yake napengine hata utu wake ili kuhakikisha yule anayemtegemea anapata mahitaji yake inawezekana mtoto/ndugu au mtu baki tu.

Yohana 10:15……….. kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.

 Naam wako wazazi wanalala njaa ili kuhakikisha mtoto anaenda shule na kupata mahitaji yake muhimu.

Wakati mwingine ili kitu kimoja kizaliwe lazima kimoja kife, mathalani ili upate kuvuna mahindi ni lazima mbegu za mahindi uzifukie zioze chini alafu mmea uchipuke na hatimaye upate mavuno yake mbali na hilo pia hata mdudu kinyonga pindi anapozaa anapoteza uhai wake ili kiumbe kingine aina yake kiweze kutokea.

Ni muhimu usitushwe na hali ngumu unayoipitia au hali inayokuzunguka bali tishiwa/ogopa na matokeo yajayo baada ya hali ngumu iliyokuwa inakukabili au inayokukabili.

Wafilipi 3:14………. nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.

Wafilipi 3:13…………Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;

Kwa asilimia kubwa inaaminika kwamba “ Hakuna ukombozi bila kujigharimu “ ndomana hata ukombozi wa nchi nyingi za afrika ulipatika baada ya mtu mmoja kujigharimu ( kuhatarisha maisha yake ) mathalani Tanganyika-hayati.Mwl. J.K.Nyerere, Afrika ya kusini-hayati. Nelson Mandela na wengine wengi.

1 Yohana 3:16…….. Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.

Na kuna msemo unasema “ ili upate lazima utoe “

Furahia sana pindi itakapo kubidi kuvikwa pingu kwa ajili ya usalama wa mtu mwingine.

Pingu  yako ya LEO ndio fahari yako ya KESHO!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni