Hakuna kitu kizuri kama “ kuishi uku ukiona “ japo unaweza
kuishi bila ya kuona!
Watu wengi uweza kuyafurahia maisha au kuhuzunika ukitegemea
namna wanavyo yaona maisha!
Mwanzo 17:15-22
“ 15 Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai
mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara.
16 Nami nitambariki, na tena
nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na
wafalme wa kabila za watu watatoka kwake.
17 Ndipo Ibrahimu akaanguka
kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia, kwake
atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
18 Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau
kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.
19 Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara
mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya
agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.
20 Na kwa habari za Ishmaeli
nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa
maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.
21 Bali agano langu nitalifanya
imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.
22 Mungu akaacha kusema naye,
akapanda kutoka kwa Ibrahimu.”
Mungu alipokua anaongea na ibrahimu kuhusu kumpata mwanae
isaka na kumuonyesha namna atakavyokuwa
na namna atakavyofanya agano nae.
Mungu anazungumza mambo sio yasio kuwepo tu bali yale yasiyo
kuwa na hata matarajio hama uwezekano wa kutokea kuwa yatatokea na kuwa Baraka
kwake na kwako pia.
Japo ibrahimu alikuwa na imani kwa Mungu ( imani anayoishi )
sara sio kwamba alikuwa amwamini Mungu la asha! Bali aliweka mkazo wake sana
katika uhalisia wa mwili wake “ sara alikuwa amekoma katika desturi ya mwanamke
“
Lakini Mungu angalii kama inavyoonekana bali uangalia mambo
kwa jicho lake linalo tazama hatima ya kitu.
Ni watu wachache sana wanaoishi uku wakitazama kesho, Ndomana
wako watu wenye watoto uweza kuwacheka hama kuwadharau wanawake waliochelewa
kupata watoto au wanawake wasio zaa ( tasa ) ghafla uweza kukuta maisha
yamebadilika ajali imeangamiza watoto wote na yule uliyemdharau amepata
mapacha.
Na ni ngumu kumuona Mungu na wala kuishi vizuri na majirani
zetu kama macho yetu yakiwa yamebaki kuangalia leo zaidi ya kesho.
Mchakato wa Mungu siku zote uangalia hatima ya jambo na
kukufanya uwe mkuu!
Daudi alipokuwa anaandaliwa kumuua goliath na kuwa mfalme,
Mungu alianza naye kwa dubu na mwanasimba “
Moja ya tabia la jicho la Mungu uwa angalii kile
kinachoonekana bali uenda zaidi ya hapo ambapo kwa mtu wa kawaida sio rahisi
kuzama uko.
Na moja ya kitu kinachoweza kukufanya uwe na furaha ni kuiona
kesho itakavyokuwa, hilo jicho lisiishie kwenye elimu ulizonazo au uzoefu bali
linalobebwa na neno la Mungu au kauli ya Mungu.
Ni muhimu kujua unapaswa kuishi sawa na Mungu anavyotaka au
anavyotegemea kwa kuwa wewe ukuzaliwa kwa bahati mbaya bali kwa kusudi kamili
la Mungu, hivyo ni lazima uishi katika uradhi wa mapenzi yake ili uweze
kulitambua hilo kusudi.
Na kufurahia maisha kunaanza hapo baada ya kulijua na
kuliishi kusudi lako, ubora wako na ustawi wako unazaliwa pale tu utapoanza
kulitumikia kusudi.
Jicho la kesho ni jicho linaloonyesha ustawi na hatima yako
na wewe wa kesho vile utakavyokua.
Bora mtu akunyime vyote lakini usiruhusu asizuie kuiona kesho
yako! Na wewe ndio mwenye uwezo na kumpa nafasi hiyo au la! KESHO YAKO IKO
MIKONONI MWA MUNGU.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni