Ijumaa, 6 Machi 2020

JICHO LA MUNGU




Moja ya kitu kinachoweza kufanya uyafurahie mazingira kwa kusema ni mazuri ni baada ya kuona “ kazi ya jicho “ 

Natukumbuke kuwa kuna kuona kwa aina mbili, kuna kuona kwa macho pia kuna kuona kwa akili mathalani unaweza pewa hesabu iliyofungwa fungwa sana na ukiangalia kwa haraka unaweza ukakosa jibu lakini pindi akili yako ikapata utatuzi wake basi hapo wewe utakuwa unaangalie jibu tu maana ugumu umeshapotea.

Utofauti mkubwa wa jicho la Mungu na la mwanadamu, jicho la mwanadamu uangalia kilichopo na uweza kubashiri kile kinachoweza kutokea lakini sio jicho la Mungu lenyewe uona mwisho wa jambo ulio na uhakika na sio kubashiri au kubahatisha.

Kwa mtu unayetaka kutembea na Mungu hama kuona mkono wa Mungu, basi unahaja ya kuhakikisha jicho lako linaona kama la Mungu, nje ya hapo itakuwa ni vigumu tu kwasababu mtakuwa hamja ambatana.
Unapotaka kuifurahia dunia kama wanadamu  wanavyoifurahia basi tembea katika jicho la kibinadam lakini pindi utakapotaka kuifurahia dunia kama vile ulivyokusudiwa basi hakikisha jicho la Mungu lina nafasi ndani yako.

Hata unapokuwa katika hali ngumu kiasi gani katika uchumi, ugonjwa au mahusiano lakini utakapotembea katika jicho la Mungu ni lazima uone kesho yenye faida iliyo jaa utatuzi wa shida ya leo.

Kuna baadhi ya mambo yanayoweza kukuta ghafla ukajiona thamani yako haipo lakini pindi utakapo jiona katika mtazamo au jicho la Mungu thamani yako itarejea kwa kasi ya ajabu.

Unahitaji kujiona katika jicho la Mungu ili uweze kulitumikia kusudi la Mungu vizuri lililoko ndani yako, maana katika utumishi kuna misukosuko mingi nje ya jicho la Mungu unaweza kupoteza mwelekeo sahihi.

Maisha ya Mungu yanazaliwa ndani yako pale utakapoishi katika mwelekeo wa jicho la Mungu.
Unapoyatazama mambo kwa jicho la Mungu ni vigumu sana upate kushikwa  mikono na watu hasa wanaona kwa jicho la wanadamu.

Unapoyatazama mambo kwa jicho la Mungu hata waliokaribu nawe na kutegemea watakuunga mkono watakuona umepotea.

( Nuhu-safina )!
Mwanzo 6: 13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.
                    14 Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami.
                22 Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.

Hatua ya awali ya kuanza kuona kama Mungu ni kuanza kujifunza kuisikia sauti ya Mungu na kukubaliana nayo kwa umakini wote kuliko chochote.

Uwa hatuoni kama Mungu anavyoona kwa kuzaliwa bali kuna hatua mpaka kufika hapo ndomana mtu azaliwi tu akawa chuo kikuu lazima kuna hatu za awali ambazo ni muhimu sana katika kukupeleka uko juu!

INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey  Nelson………………………………………………. 0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni